CHADEMA na UKAWA waachane na siasa nyepesi, 2020 inakaribia

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,997
20,329
Naleta mada hii chokozi kwenu ili tujenge fikra mpya katika medani ya siasa nchini. Maendeleo yoyote ni matokeo ya msuguano wa kifikra chokonozi ama chochezi na kinzani ulimwenguni.

Chama cha kisiasa ni maungano ya watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au za kifalsafa pamoja na faida kwa ajili ya vikundi fulani faida zao za binafsi. Vyama mara nyingi hutamka mwelekeo au itikadi fulani inayoandikwa katika programu yao.

Katika mfumo wa vyama vingi kila chama kinagombea nafasi za bunge au serikali kuu dhidi ya vyama vingine. Wakati wa uchaguzi kila chama kinapaswa kujieleza, kutetea matendo yake ya nyuma na kuonyesha jinsi kinavyotaka kuboresha mambo tofauti na vyama vingine. Kwa njia hii kila chama huchangia harakati ya kujenga nia ya jamii inamofanya kazi kama inashinda au kushindwa kwenye uchaguzi.

Penye mfumo wa chama kimoja kazi ya chama itakuwa tofauti. Historia ina mifano ya kwamba chama pekee kinaelekea kwenye udikteta kwa viwango tofauti, tafsiri yake ni kuwa chama kilichoshika madaraka kinachoua vyama vingine vya siasa katika nchi ya mfumo wa vyama vingi, ni chama kinachounda na kuongoza dola la kidikteta.

Vyama hutofautiana sana kuhusu kiasi cha tofauti za maoni zinazoruhusiwa ndani yao, uhusiano kati ya viongozi na wanachama, kiasi cha uwezo wa wanachama kuathiri mwelekeo wa chama na umuhimu wa programu au mipango.

Naaam, baada ya somo hilo fupi sasa nirejee kwenye siasa zetu za ubwa. Nipongeze chama cha Chadema na Ukawa kwakushiriki uchaguzi na kushinda kwa kura nyingi japo hakikushinda kutangazwa kushika serikali "urais". Hilo ni mchakato mrefu nitalieliza leo kwa kiasi chake,

Yote yamepita lakini siasa haijapita, bado safari ni ndefu kuelekea kushika dola kwa ridhaa ya umma bila kuruhusu damu ya Mtanzania awaye yeyote kumwagika kisa madaraka, kwa hili hongera Lowasa, Mbowe, Mbatia na Maalim Seif.

Nimezifuatilia siasa za Afrika, karibu zote zinalingana kwa kila kitu, lakini siasa za Asia hazilingani na siasa za Latini Amerika, wala siasa za Amerika hazilingani na siasa za Mashariki ya Mbali.

Ninashawikisha kuanzisha au kuibua vuguvugu la fikra mpya za aina ya siasa nchini nikitaka tubadili mwelekeo wake na kuruhusu AGENDA kuu ziwe mbele, itikadi ifuate kuelekea LENGO kuu la kushika dola. Tofauti na sasa vyama vinashughulika na harakati nyepesinyepesa zinazoisha muda wake mapema na kimsingi hazitupi mwangaza wakutimiza malengo yetu ya kushika dola. Tukubaliane kuwa MALENGO makuu yetu ni kushika madaraka, hili halihitaji mjadala. Ninachojaribu kusema ni zile njia ndogo kuu za kuendea kuyashika madaraka yaani AGENDA KUU.

Aina hii ya siasa ninayoihuisha ndio inayofanywa Amerika na Ulaya ya kati na baadhi ya Asia na Moscow.
Ni aina nzuri ya siasa, watu wanazifia agenda badala ya vyama kwanza au matukio, watu walipende taifa kwanza na agenda kabla hawajampenda mtu au chama.

Tuuondoe mfumo ambao umewafanya watanzania kuwa na uchama badala ya agenda na utaifa.
Tujenge taasisi ambayo wanachama wake wanapotoka kwenda kuongea na wananchi wasiende na uchama ambao kimsingi uchama huo huonwa kirahisi kwa sare na bendera bali watembee na Agenda na utaifa.

Vikwazo vya vyama vya siasa kushika madaraka vipo vipo vinne ambavyo ni vikubwa,

1. Sheria ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo inavifanya vombo hivyo kuwa sehemu ya chama tawala ccm.

2. Tume ya uchaguzi ambayo kimsingi ni tume ya chama tawala kwasababu inachaguliwa na mwenyekiti wa ccm kuanzia mwenyekiti wake hadi karani wake, pia katika ngazi ya majimbo tume ya uchaguzi huwa haisimamii kwa 100% kabisa uchaguzi huo na badaka yake mkurugenzi wa wilaya/manispaa ndie husimamia, zingatia mkurugenzi huyo ni kada wa ccm aliyeshindwa kura za maoni za ubunge. Vivyo hivyo udiwani na uenyekiti wa mitaa husimamia na afisa mtendaji wa kata na afisa mtendaji wa mtaa ambao ni makada kindaki ndakindaki wa ccm.

3. Matokeo ya urais yathibitishwe ama yahojiwe mahakamani.

4. Katiba iweke utaratibu wa namna ya kukabidhiana madaraka.

Ningeshauri Chadema na muungano wake wa Ukawa tuachane na matukio na agenda ndogondogo ambazo kimsingi zinaweza kusimamiwa vizuri na wanaharakati wa kawaida kama akina Mange Kimambi, Sungusia, Maria Sarungi, Kijo Bisimba nk, waachiwe ccm waendelee na viroja vya viwanda kwakuwa hawana fikra mbadala, Chadema na ukawa kwasasa tuelekeze katika kudai mabadiliko ya katiba mpya, na kwakuwa ccm haitaleta mchakato wa katiba mpya, basi wabunge wa upinzani waanze mar moja kuandaa hoja za mabadiliko/marekebisho ya ya katiba ya 1977 katika vipengele nilivyovianisha hapo juu. Hatuwezi kuingia katika uchaguzi 2020 kwa katiba na tume hii na muudo huu wa vyombo vya ulinzi na usalama, itakuwa sawa na kuingiza timu uwanjani huku tayari tuna matokeo yakufungwa.

Hili ni zito ndani ya ccm kukubalika kwasababu linahusu itikadi ambayo ni sawa na dini kwa mtu, lakini tukilijaribu na kulihubiri kwa namna ambayo tunataka watu walielewe kuwa agenda ya katiba ya Tanzania iwe mbele, bila shaka wataelewa. Na wakibana zaidi , njooni kwa wananchi, umma haunaga majadiliano bali nguvu tu ambayo sheria na amri za kirais hazitawazuia.

Nimejaribu kupitia vitabu na machapisho mengi yanayohusu agenda na utaifa, hakika nimeona laweza kuvuta kada zote zikatuelewa hata zile kada zinazozuiwa na serikali kwa minajiri ya kisiasa.

Kwakifupi tuanze kama alivyoamua Mwalimu Nyerere kuachia nyadhifa za Chama na kurudi vijijini kueneza chama kwa agenda ya uhuru bila kuvaa uchama wake. Alikwenda kama mwanautanganyika.

Niwashukuru sana waamabadiliko wenzangu!

Lumumba imepasuka, kuna lumba ya chato na kuna lumba ya chamwino, tuachane na michezo ya vyeti feki, bashite, tumbuatumbua, ndege, nk hivi vyote ni zubaisha bwege tu na sasa imebaki miaka miwili na nusu tu uchaguzi mwingine! Tunataka wabunge wa upinzani waje na hoja bungeni zinazotoa mwelekeo wa kutusaidia kushinda 2020.

Upepo unazidi kuvuma huko Lumumba, uchi wa kuku unakaribia kuonekana!

Na Yericko Nyerere
 
Sitashangaa kabisa kama CHADEMA wakishiriki kikamilifu uchaguzi mkuu wa 2020 chini ya mazingira yaleyale tokea 1995.

Wakishindwa wataanza kulialia na kuanza kudai tume haikuwa huru, katiba iko hivi, na blah blah huku walikubali kushiriki uchaguzi ambao hayo yote wanayoyalalamikia waliyajua.

Na sidhani kama CHADEMA na wafuasi wake wana uwezo wa kuachana na udakiaji wa matukio yasiyo na tija kwenye kutimiza azma yao ya kushika madaraka.

Ili CHADEMA iweze kubadilika inahitaji kubadili uongozi. Uongozi ule ule miaka nenda rudi hautokuja na jipya.

Lakini kwa aina ya uongozi iliyonayo CHADEMA na aina ya wafuasi iliyonao sioni kabisa hicho chama kuweza kubadilika kati ya sasa na 2020.

Naamini hicho chama kitaendelea kuwa chama cha kudaka matukio ya kipuuzi puuzi tu na kuendelea kupiga dili za ruzuku huku kikipokea makapi ya CCM.

CHADEMA bado hakijaonyesha kuwa kipo tofauti na CCM [jambo ambalo ni la msingi kabisa] na hivyo hakipo tayari kushika madaraka.
 
Cheti Cha Makonda kitawapa kura 10,000,000 muingie Ikulu Kiufupi Magufuli kawashika Kila Kona.

Yaani mmebakia na Hoja ndogo ndogo sana kama Kunyimwa Kuongea Misibani, Kumuomba Rais atangaze Siku tatu za maombolezo.

Huku Chama kikimtegemea Mange Kimambi kwa kila Udaku anaupeleka Instagram.
 
Bwana Yeriko naona umeshazeeka na siasa za bongo huziwezi.
Kwanza nakushangaa kwa kuwapongeza kundi ambalo limesababisha upinzani kuua ajenda za ufisadi na mafisadi, kundi ambalo lilikuwa likiwashutumu watu fulani kuwa ni mafisadi nanbaadae kuamua kuwasafisha na kuua nankuzika ajenda za ufisadi!
Pili, nashangaa unahamasisha eti kujiandaa kushinda uchaguzi 2020, kushinda kwa kutumia sera zipi. Maana za kupambana na ufisadi tumezifuta. Nini hasa tunataka kwenda kufanya ikulu. Ambacho kitatofautiana na anachofanya Magufuli kwa sasa na serikali yake. We dont want to waste resources for nothing.! Is it worth it kuchagua watuhumiwa wa ufisadi kwenda tena ikulu ili waendelee kwenda kufisadi? ? hatutaki hata kujaribu kufanya hivyo. Na hatutaki hata mwal. NYERERE alituasa, masuala ya uongozi wa nchi hayajaribiwi kamwe. Na hasa ukijua kabisa kundi linalotaka kwenda ikulu ni lile lile la mafisadi. Viongozi walewale waliokuwa serikali kwa umri wao wote mpaka wamezeeka hao ndio wametufikisha hapa iweje leo watushawishi eti wanaenda kutuletea mabadiliko. Yapi hayo? ? Msitufanye watanzania wajinga, hatupo huko tena. Ni heri kuwapa viongozi ambao wameonyesha msimamo wa kuwakataa mafisadi kama Dr Slaa na Lipumba kuliko kuwapa uongozi watu wanaoweza kununuliwa kwa vipesa vichache nankuuza utu wao. Hatupo tayari. Tafuteni kazi nyingine ya kufanya
 
Sitashangaa kabisa kama CHADEMA wakishiriki kikamilifu uchaguzi mkuu wa 2020 chini ya mazingira yaleyale tokea 1995.

Wakishindwa wataanza kulialia na kuanza kudai tume haikuwa huru, katiba iko hivi, na blah blah huku walikubali kushiriki uchaguzi ambao hayo yote wanayoyalalamikia waliyajua.

Na sidhani kama CHADEMA na wafuasi wake wana uwezo wa kuachana na udakiaji wa matukio yasiyo na tija kwenye kutimiza azma yao ya kushika madaraka.

Ili CHADEMA iweze kubadilika inahitaji kubadili uongozi. Uongozi ule ule miaka nenda rudi hautokuja na jipya.

Lakini kwa aina ya uongozi iliyonayo CHADEMA na aina ya wafuasi iliyonao sioni kabisa hicho chama kuweza kubadilika kati ya sasa na 2020.

Naamini hicho chama kitaendelea kuwa chama cha kudaka matukio ya kipuuzi puuzi tu na kuendelea kupiga dili za ruzuku huku kikipokea makapi ya CCM.

CHADEMA bado hakijaonyesha kuwa kipo tofauti na CCM [jambo ambalo ni la msingi kabisa] na hivyo hakipo tayari kushika madaraka.
tatizo Mbowe ameifanya CHADEMA kama SACCOS yake ya kula pesa za ruzuku na wafadhili na sio chama cha kushika dola
 
Back
Top Bottom