CHADEMA na UKAWA kuweni wazi kuwa mnatetea mafisadi na si mnapigania demokrasia

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

Binafsi ninashangazwa sana na kauli za hawa viongozi na wafuasi wa UKAWA. Watanzania wengi wakiwemo pia wafuasi wao wa UKAWA wanawashangaa kwa maamuzi wanayofanya. Hakika Tanzania haijapata kuwa na upinzani dhaifu kama kipindi hiki.

Baada ya kujaribu kick zote zikawashinda, sasa wapinzani wamekuja na hoja kuwa wanapigania demokrasia. Hata hivyo, hao wanaosema kuwa wanapigania demokrasia na kupinga udikteta wa Rais Magufuli sidhani kama wana hata chembe ya demokrasia ndani ya nafsi zao na vyama vyao. Nayasema haya kutokana na mifano kadhaa ambayo inadhihirisha kuwa hawana chembe ya demokrasia.

Wakati Zitto Kabwe anafukuzwa ndani ya CHADEMA, Freeman Mbowe alituaminisha kuwa Zitto ni Msaliti na kwamba hastahili kushirikiana kwa lolote na msaliti. Freeman Mbowe akaenda mbali kwa kusema kuwa Zitto anashirikiana na Serikali na CCM kuihujumu CHADEMA wakitoa mfano wa Waraka wa Siri wa Zitto Kabwe. Sina hakika kama Usaliti wa Zitto Kabwe uliishia kule tu CHADEMA na leo tunashuhudia msaliti yule yule akisaidiana na msalitiwa.

Mwaka 2004, Freeman Mbowe alifanya marekebisho ya Katiba ya CHADEMA kinyemela kwa kuondoa ukomo wa uongozi ili awe Mwenyekiti wa kudumu, sifa mojawapo ya kiongozi dikteta. Leo hii kila kiongozi anayetaka kugombea uenyekiti wa CHADEMA ama anakufa kitatanishi ama anafukuzwa uanachama kama ilivyotokea kwa CHACHA WANGWE NA ZITTO KABWE. Yamewakuta pia akina Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.

Zitto Kabwe kajipachika cheo kwa lengo tu la kuendeleza ufalme ndani ya ACT. Leo hii Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira hana nafasi na badala yake unyenyekevu upo kwa Ayatollah.

James Mbatia, chama kimemfia. David Kafulila aliwahi kufukuzwa NCCR kwa sababu tu alionesha nia ya kugombea nafasi hiyo. Ni udikteta ndio uliotumika mpaka James Mbatia amekuwa Mwenyekiti wa kudumu wa NCCR.

Mchakato wa kumpata mgombea wa UKAWA hakika umeacha maswali mengi na wengi wamekuwa na majeraha yasiyopona. Ni sababu ya Dr Slaa kuachia nafasi ya Katibu Mkuu CHADEMA na Prof Lipumba kuachia nafasi ya Mwenyekiti wa CUF. Hakukuwa na ushindani wowote ndani ya CHAMA wala ndani ya UKAWA. Ni udikteta wa Freeman Mbowe ndio uliofanya CHADEMA kumteua Lowasa kuwa mgombea Urais tena akiwa mwanachama wa chama hicho kwa siku zisizozidi 10 tu.

Hawa akina Ben Saanane ambao wanatumwa na CHADEMA kumtukana Rais mitandaoni na kudai eti wapo tayari kumwaga hata damu ili mradi tu wanatetea demokrasia waliwahi kutumiwa na Freeman Mbowe kutaka kumuua Zitto Kabwe. Tuhuma za Ben Saanane kutembea na sumu ziliwahi kuripotiwa humu mitandaoni eti kwa sababu tu Zitto Kabwe alitaka kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA. Sasa niwaulize ndugu zangu wa CHADEMA, je mnafanya demokrasia gani?

Mchakato wa kuwapata wabunge wa viti maalum wa CHADEMA hakika umeacha maswali mengi. Sote tunakumbuka jinsi wanawake wa chama hicho walivyoandamana kupinga kitendo cha uongozi wa CHADEMA kuwateua watu ambao si wa maeneo husika kuwa wabunge wa viti maalum. Tumeshuhudia pia watu kama akina Ruth Molel ambao hawajawahi kuwa wanachama wa CHADEMA waliteuliwa kuwa wabunge wa viti maalum. Kuna kada wa CCM ambaye hadi wakati anateuliwa na CHADEMA kuwa mbunge wa viti Maalum, alikuwa ni kiongozi wa UVCCM. Only in CHADEMA.

Mwisho nimalizie kwa kumkumbusha ndugu yangu Ben Saanane na nduguye Malisa Godlistern, hamtaweza kamwe kupambana na Rais Magufuli. Wananchi wamemkubali na yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu. Kama mlizoea kuchezea masharubu ya Jakaya Kikwete hakika kwa JPM mtagonga mwamba. Endeleeni tu kutumika na mafisadi ila mjue kuwa mwisho wa ufalme wa mafisadi umewadia.

Mnapoanzisha ugomvi wa mawe ilhali mmejificha kwenye nyumba ya kioo basi mtarajie na muwe tayari na yatakayowatokea. CCM ni Ile Ile iliyowashinda watangulizi wenu mpaka wengine wakaamua kukimbia CHAMA
 
Kinachouma zaidi saizi bajeti zinapitishwa wasemaji wetu wa kututetea wanapiga kitwanga mtaani kisa zidumu fikra za mwenyekiti wakati hakuna anayetutetea bungeni angalau tupate keki ya Taifa.
 
Hivi JPM hajakamilisha kuteua maDC? Lumumba wanajitoa kbs ufahamu
 
Mkuu Lizaboni mara zote huwa unaleta hoja za maana. Lakini,hoja zako huonekana ni za kizushi na kipropaganda kwa sababu kuu mbili. Kwanza,kila hoja yako lazima itaje CHADEMA,UKAWA au Lowassa. Pili,huwa hutoi nafasi kwa wengine wenye mawazo yasiyofanana na yako kuchangia. Daima hupenda kujaza uzi wako kwa michango yako mwenyewe. Hufanyi vyema kimjadala binti/kijana.
 
Nilikuwa nawavutia kasi tu washenzi hawa bora umeniwahi, sijui hizi sheria zinafanya kazi gani maana wanavuka mipaka sasa, miaka yote hii wanatuhubiria kuhusu changes, mtu anafanya tuliyokuwa tunayahitaji na yaliyotufanya tuwaamini wanamgeuka, pelekeni vyama vyenu huko sasa mtuache na dikteta wetu.
 
CHADEMA na siasa za nyani haoni kundule. Siku zote tumekuwa hodari sana kuwakosoa wenzetu. Naona yale mafundisho ya Yesu ya Kibanzi na Boriti hayajatuingia

Uzi huu wakiuona mafisadi lazima wampigie simu Maxence Mello

bonge ya sms big up nakupa heko

Tehetehetehe. Wamekamatika hawa. Hawana pa kujiokoa

Ahsante Mkuu. Nimejaribu kuwakumbusha tu wasije wakasema sijawakumbusha

Haaa!!Yaani wewe huoni sehemu nyingine ya kupiga unapiga macho sasa wataonaje

Kaka angu siku hizi unawashika pabaya sana hawa UKAWA. Yaani jinsi unavyowawezea unawachezea kama mwana Sesere.

Akutukanaye hakuchagulii tusi na adui usimchagulie pa kupiga. Wewe tandika tu
Nafasi za uDC hamna tena, fanyeni kazi zingine kujikomba hakujawalipa
 
Back
Top Bottom