Chadema na slaa mbona mnatuangusha? Changamkeni !!

skeleton

Member
Aug 17, 2010
60
3
Hakuna siri wala ubishi kwamba CHADEMA ndio chama cha upinzani cha ukweli kilichobaki na ndio tumaini la Watanzania wanyonge ambao ndio sehemu kubwa ya Watanzania katika kuwakomboa na hali mbaya ya maisha.

Kinachonifanya nitoe dukuduku langu ni kuona kama CHADEMA na Dr. Slaa wamejisahau sana au sijui ndio wametulia kwanza wanavuta pumzi? Hakika muda hausimami unazidi kwenda na wala hautawasubiri! Nilitegemea ningeona CHADEMA inashughulika na mambo muhimu yafuatayo:

Moja, ni kwa CHADEMA kuanza kufungua matawi sehemu zote za Tanzania ambazo hazina matawi na kuimarisha yale yaliyopo. Tena huu ni muda muafaka kwa Dr. Slaa ambaye sasa hivi hana kiti cha ubunge kusaidiana na wana CHADEMA wenzake kuzunguka nchi nzima na kuimarisha chama. CHADEMA kikumbuke mwaka 2015 sio mbali kabisa na wamejifunza hilo kwenye kampeni za mwaka huu walipojikuta hawana matawi sehemu nyingi na kuhangaika kupata watu wa kukipigia kura. Wamshukuru sana Dr. Slaa kwa uwezo (convincing power), usafi (hana rekodi chafu kiutendaji) na kuwa na uchungu wa kweli na nchi yake kwa kutetea maskini na kupinga ufisadi.

Pili, wapiganie kudai haki yao waliyodhulumiwa wakati wa uchaguzi kwa kura kuchakachuliwa na kuibiwa kura. Najua wengine wanafungua kesi mahakamani lakini kwenye hili suala nilitegemea tungepata ripoti/feedback officially toka kwa Dr.Slaa (mgombea urais aliyeibiwa kura) na chama chake nini wamefanya badala ya kupata vitu in piece meal mara huyu amesema haimtambui rais, mara huyu amesema tunamtambua rais n.k. Nilitegemea chama na mgombea urais, wangewaita waandishi wa habari wafanye press conference na kutoa tamko kwa maandishi pamoja na kueleza hatua zilizochukuliwa na zinazotegemewa kuchukuliwa hapo mbeleni kuhakikisha haki iliporwa inapatikana. Kwani wananchi wengi waliokipigia chama hiki kura hawategemei waliowapigia wanakaa kimya bila kuwapa feedback, itakuwa nikuwadharau.

Lakini naona ndo kwanza migogoro inatokea CHADEMA ya kugombea ulaji wa viti vya ubunge, kutoka bungeni wakati wa hotuba ya rais, n.k. Nilitegemea ningemsikia Dr. Slaa na akina Mbowe leo mara wako Marekani, Kesho Uingereza, UN, the Hague, n.k wakizunguka kama CUF wakati ule (kabla hawajapata ulaji hivi karibuni na kusaliti upinzani) nchi mbalimbali kuelezea uhuni waliofanyiwa. CHADEMA mnatakiwa mzunguke nchi za nje na kwa wananchi nchini kueleza mliyofanyiwa na jinsi wananchi walivyonyimwa demokrasia. Tena muda muafaka ni wakati mkitafuta wanachama wapya na kufungua mashina.

Tatu, ni hilo la kugombea katiba mpya au kupigania hivyo vipengele vinavyohusu uchaguzi vibadilishwe. Hapa sina wasiwasi tutasikia kelele nyingi, lakini kelele hizo nashauri zihusishe sana na nchi wahisani ili waweze ibana serikali kimisaada (potelea mbali kama tutakaa na njaa muda mfupi kwa kukosa misaada lakini katiba ifanikiwe badilishwa.

Nne, kuhakikisha chama chenu hakisambaratishwi na CCM na usalama wa Taifa kwa kuanza kugawanywa kijanja. Mnatisha na hivyo lazima mtaingiliwa humo humo ndani yenu wengine watanunuliwa ili wawasaliti. Dawa ni kutenganisha pumba na mchele kwa kuchambua mawe, kupepeta pumba vizuri na kusafisha vizuri na maji ili mchele (viongozi wa CHADEMA wenye nia njema na Watanzania maskini na wasio na tamaa ya ulaji) ubaki peke yake.

Na mwisho kabisa, muanze panga mikakati ya uchaguzi wa 2015, muanze kufikiria wa kuwasimamisha wanaokubalika, funds mtatoa wapi, mtafute kashfa, uzaifu wa washindani wenu(CCM na vikaragosi vyake), propaganda za kuwafanyia kama wawafanyiavyo nyie n.k.

Kila la heri CHADEMA, mkifanya hayo hakika 2015 ni yenu na msipofanya hayo mtashindwa na mtakuwa mmetuangusha Watnzania. Nasisi wana JF ambao tuko upande wa CHADEMA na Watanzania wanyonge tusiache kuwakumbusha CHADEMA kama tulivyokuwa pamoja nao wakati wa uchaguzi. Tusijisahau na kukurupuka uchaguzi utakapokaribia, kwani sahivi naona tumekuwa diverted na issues nyingine kabisa eg, DOWANS n.k. Lakini napenda kuwahakikishia tutazijadili kila siku lakini zitaendelea kuwepo pamoja na ufisadi daima kama CCM isipong'olewa na kuwaweka Watanzania wenye uchungu na nchi hii na ambao wako tayari kuifia hii nchi kwa maslahi ya wananchi na si matumbo yao.

Pia CHADEMA wajiandae mapema kupambana na mijitu kama akina Lowassa kwani kuna dalili wanajiandaa kuichukua nchi 2015, hawa ni watu hatari sana kuliko waliochakachua kura mwaka huu. Msizubae, nyie ni tumaini letu, changamkeni tunawategemea na tuko nyuma yenu sisi wanyonge.
 
Hayo yanafanyika sana Mkuu wangu ila sema CCM imeshika Media zote ba huwezi kusikia kitu kama hicho.

Pia nina imani kuwa wanapanga mikakati kwanza kujijenga sehemu walizoshinda.

Na hapo ndipo waanza kueneza habari njema kwa wote kuwa CHAGUA CDM na utaendelea.....

Sasa hivi Mkoa kama Tabora yaani hamna kitu kabisa. Maisha ni kama wakati Rage yuko FAT/Simba.
 
Ndugu sikonge sawa sikatai CCM imeshika media zote, lakini hivyo vitu si tungeviona basi hata kwenye gazeti la Mtanzania Daima. Je mbona mambo mengine yanayotokea CHADEMA mazuri kwa mabaya yanarushwa na media zote? CHADEMA tusiwatetee, kweli wakae chini waanze kujipanga na kuhamasisha wananchi mapema kwani wao ndio solution ya ili tatizo la ufisadi na maovu yote ya CCM. Wasipofanya hivyo tutaendelea kukesha(wachukia maovu) ndani ya hii JF kila siku tukijadili CCM wamefanya dhambi hii, mara dhambi ile bila solution! Kwangu mimi mengi yanayojadiliwa na wana JF ni mazuri (yale yanayopinga maovu), ila sasa kipaumbele kiwekwe mbele kui push CHADEMA isilale mpaka kieleweke! Isilewe na viti vichache vya ubunge ilivyopata kwani ukombozi wa kweli wa Watanzania haujapatikana. CHADEMA you are the ultimate solution to our problems. Ningependa kuona baada ya miaka 5 ijayo forum hii iwe inajadili masuala ya maendeleo (badala ya ufisadi wa CCM) na kesi walizofunguliwa mafisadi wa CCM.
 
Back
Top Bottom