Chadema na Mwenendo Wa Wapiga Kura Tanzania

Mchambuzi lengo la mjadala/mada yako ni nzuri sana kuamsha ari ya wanasiasa kutumia takwimu zilizopo kuangalia wapi wakijikwaa, ingawaje nachelea kusema asilimia kubwa ya wanasiasa wahazitumii hizi takwimu. Kuhusu uchakachuaji wa kura, hilo halina nafasi kwa sasa. Takwimu hizi zitabaki kuwa halali kwa sasa na hata tunawaita wafadhili wa nchi hii wanatumia hizo takwimu.
Uchaguzi ni kama mchezo wa mpira, unahitaji ushikiano wa hali ya juu kushinda (team player) na hii ndio iliyokosekana kwa wanachadema kwenye uchaguzi uliopita. Kisingizio cha uchakachuaji wa kura nafikiri uwekwe pembeni na kutafuta ni Wapi walipojikwaa waweze kujirekebisha uchaguzi ujao
 
Last edited by a moderator:
Asante sana Mchambuzi kwa uchambuzi wa kina juu ya mwenendo wa wapiga kura wa Tanzania. Mchangiaji Nicholas ameelezea vizuri sana juu ya factors nyingine ambazo hukuziongeza lakini kwa kiasi kikubwa zinachangia/zilichangia kupata matokeo uliyotumia katika kufanya uchambuzi wako.

Mimi nataka kuchangia kuhusu upigaji wa kura kwa ujumla wake na msisitizo ukiwa kwenye yale majimbo uliyoyataja juu. Kwanza kuna tofauti kati ya vigezo vinavyotumika na wapiga kura kumchagua mgombea ubunge na Rais. Ni vigumu sana kwa mgombea ubunge ( ukiondoa labda Dar es salaam na majimbo ya mijini) kupata mshindi wa ubunge iwapo mgombea ana uasili wa jimbo/mkoa anaogombea. Maana yake nini? Wapiga kura wengi kwenye nafasi ya ubunge pamoja na mambo mengine yote, asili ya mgombea na uhusiano wake na jimbo husika una nafasi yake. Kwa upande wa Rais factor hii itatumika pale kwenye jimbo lake au eneo analotoka (effect ndogo sana kwenye matokeo ya jumla), mfano Kikwete haitakuwa ajabu kupigiwa kura na wanachama wa Chadema wenye asili ya Bagamoyo au mtaa wake hapo Ada Estate, sawa na Dr. Slaa, pale Sinza hata wanaCCM no wonder walimpigia kura. Kwa hiyo kubwa mojawapo kwenye nafasi za ubunge ni ukanda, na hii ilianza zamani za TANU :)

Kingine kwenye uchaguzi wa ubunge, uwezo binafsi wa kujieleza/kushawishi (kwa maneno yeyote yale siyo lazima sera) wapiga kura na hasira ya mbunge aliyepita ina nafasi sana katika kufanya maamuzi (Ushindi wa Mch. Msigwa). Wapiga kura huwa wanakuwa na hasira na mbunge ambaye alishindwa kutimiza matarajio yao, na katika hali hiyo wapiga kura hufanya maamuzi ya kuchagua kwa kuangalia nani mwingine aliyefaa nje ya mgombea aliyepita.

Uelewa mdogo wa wapiga kura juu ya nafasi ya urais na maamuzi ya taifa. Wako wapiga kura ambao waliamini Chadema bado ni chama kichanga na bado hakijajijenga kupata nafasi ya urais, hawa waliwapigia wabunge wa CDM lakini kura ya urais walipeleka CCM kwa msemo wa Zimwi likujalo...... Na sidhani kwenye hili ZZK au Mbowe na wengine wengeweza kufanya chochote kubadilisha.

Mchango wangu umeangalia tu yale majimbo uliyozungumzia hapo juu, bila kufikiria nafasi ya Rushwa, Tume ya uchaguzi, vyombo ya ulinzi na usalama katika kuakisi matokeo.

Hayo machache niliyoyaweka ukiongeza na yale ya Nicholas utaona itakuwa ngumu sana kwa Chadema kufanya utafiti kwa kuangalia matokeo ya 2010, jambo moja lililowazi ni kuhakikisha Chadema inaeneza elimu ya uraia especially miongoni mwa vijana kwani wao hawaogopi mabadiliko na ndiyo watakuwa wapiga kura wengi kama wakihamasishwa juu ya wao kuwa sehemu ya maamuzi juu ya mustakabali wa taifa lao mwaka 2015.

Nje kidogo ya mada yako, unafikiri uchaguzi huru ukifanyika leo kwa wagombea walewale wa urais wa 2010 kutakuwa na matokeo tofauti? Kwanini?
Na je watanzania wangapi wanaelewa tofauti za msingi kisera kati ya CCM na CDM?
 
Mchambuzi lengo la mjadala/mada yako ni nzuri sana kuamsha ari ya wanasiasa kutumia takwimu zilizopo kuangalia wapi wakijikwaa, ingawaje nachelea kusema asilimia kubwa ya wanasiasa wahazitumii hizi takwimu. Kuhusu uchakachuaji wa kura, hilo halina nafasi kwa sasa. Takwimu hizi zitabaki kuwa halali kwa sasa na hata tunawaita wafadhili wa nchi hii wanatumia hizo takwimu.
Uchaguzi ni kama mchezo wa mpira, unahitaji ushikiano wa hali ya juu kushinda (team player) na hii ndio iliyokosekana kwa wanachadema kwenye uchaguzi uliopita. Kisingizio cha uchakachuaji wa kura nafikiri uwekwe pembeni na kutafuta ni Wapi walipojikwaa waweze kujirekebisha uchaguzi ujao

Nashukuru sana kwa kuliweka hili sawa mkuu; natumaini wengi watalielewa hivyo;
 
Babuwaloliondo,

Nashukuru sana kwa mchango wako. Kuhusu suala la uchakachuaji wa matokeo nilitoa majibu yangu kwa nadhani kwa mchangiaji aitwaye babuyao kwamba, nililifikiria sana suala hili kabla ya kuja na mada hii lakini nikaona kwamba kwa ujumla wake, Chadema will play it safer kwa kuyafanyia kazi matokeo haya kuliko kuyadharau kwamba hayana uhalali kutokana na taarifa zilizosambaa kwamba matokeo yalichakachuliwa, hasa kwa vile haijulikani ni wapi matokeo yalichakachuliwa; nikazidi kusisitiza kwamba either way, still Chadema needs numbers za kufanyia kazi as they prepare for 2015, na takwimu za matokeo ya uchaguzi wa 2010 ni moja ya numbers muhimu sana kuzifanyia kazi katika miaka hii mitatu iliyobakia;

Pia nilitoa majibu kwa mchangiaji mwingine i.e. ‘nicholas', ambae nae aligusia suala la uchakachuaji ambapo nilimjibu kwamba, kwamba takwimu hizi ni za kweli au nyingi ni za kupikwa (kwani kuna sehemu ya takwimu hizi ni za kweli), these are the only stats available for us to make sense of what transpired huko majimboni, and unless tuamue kutojadili matokeo ya 2010 kwa vigezo vya takwimu hizi, lakini kufanya hivyo won't make things better for us hasa kama hatutafanikiwa kuja na kitu cha kutusaidia to base our analysis ambacho kitakuwa still a representation of what transpired huko majimboni; ksms nilivyomwomba Nicholas, ningependa pia kusikia kusikia kutoka kwako juu mapendekezo katika hili, ili tuweze kupata picha inayokaribiana na mambo yalivyojiri huko majimboni;

Kuhusu swali lako kwamba je naweka katika kundi gani majimbo ambayo CCM ilishinda ubunge lakini Chadema ikashinda Urais, hili ni swali la msingi sana lakini sikuwa na majibu yake ya moja kwa moja, hivyo nikaamua kuliweka suala hili ndani ya Nadharia Tete kuu mbili; Nadhani watu wengi wame overlook maswali yangu na nadharia tete zangu ambazo nilitegemea ndizo zingetupatia msingi wa mjadala kwani hata mimi natafuta majibu; badala yake, wengi naona wametazama zaidi uchambuzi wangu wa majimbo na kutoa maoni yao mbalimbali; Ningependa kuweka nadharia tete kuu mbili kama ifuatavyo, kwa imani kwamba kwa pamoja tutaweza kupata mwanga zaidi ndani ya mada hii ya kichokonozi:

NADHARIA TETE YA KWANZA:

Wananchi huchagua wabunge kwa matarajio kwamba kiongozi huyo atajuhusisha zaidi na local issues and grievances; wananchi hawategemei mtu watakayemchagua kuwa mbunge wao ajihusishe sana na masuala ya kitaifa, isipokuwa kama masuala hayo yana uhusiano wa MOJA KWA MOJA na majimbo yao.

NADHARIA TETE YA PILI:

Wananchi wa Tanzania huchagua Rais kutokana na mapenzi fulani waliyonayo juu ya nchi yao ya Tanzania ambapo wapo tayari kujitolea kwa hali na mali katika kuilindana kuitetea nchi yao ya Tanzania. Mapenzi haya kwa Tanzania yanahusishwa moja kwa moja na CCM kwasababu CCM ndio imeizaa TANZANIA, tofauti na TANU ambayo iliikomboa nchi ya TANGANYIKA, taifa ambalo lilipotea pamoja na TANU. Mapenzi na Uzalendo wa wapiga kura kwa TANZANIA unaenda sambamba na kuichagua CCM kwani ni kwa sababu ya CCM, wao wanajihisi ndio watanzania, na wanajivunia kuwa WATANZANIA, hasa kutokana na ujenzi wa Taifa uliofanywa na CCM katika maeneo kama vile amani, umoja, udugu na mshikamano.
Mchambuzi: umechambua vizuri sana.

Nadharia zako zijazi overlook nilizipia kwa makini sana ila zinakosa nguvu katika kitu kimoja.Si za msingi, na zimekuwa derailed so easily.Ingawa naona umekataa sana kusikia uchakachuaji,ingawa nami sikuuweka katik factor za msingi kwa vile ni ngumu kuthibitisha ni kiasi gani kiliwekwa.Ila kwa kuanzia nikaweza clue ya uswa wa hayo majimbo CDm waliweka heavyweights.Uchakachuzi ulifanyika kimakosa sana hata sehmu CCM walikuwa wanyonge sana provide palikuwa strategic.Na hii ilikuwa wazi sana na pressure ilivokuwa kali toka nje ,iliwawia vigumu sana kufanya vitu haraka ili figure isilete mushkeli Local na kitaifa.Ima sure ktk majimbo ambayo ningeanzia kufanya forensic ni hayo, kama mimi nitakiwa fanya auditing.


Kuhusu majibu yako.Sikutaka kuwa unfair kihvyo kuanza zijadili zaidi ya kusema zile factors nilizosishuhudia na kwa bahati nzuri kipindi cha kampani nilitembea sehemu nyingi za nchi na kuwasikia watu,vijana,wazee,wanawake, waislam, wakristu,wazungu, waasia na hata wanasiasa wenyewe na wana kampeni wao.

Nadharia ya kwanza.

-sioni ni wapi CDM wangeweza kuwa affected na hilo kwani kila mbunge alikuwa akigombea ubunge tuu, na si ubunge na urais,hata hakika ya kuwa mawaziri.Na hata kam ni issue ya uzawa, idadi kubw aya wabunge walikuwa wa asili ya jimbo husika au hata makazi ya kudu kama vile Lema.Slaa alikuwa huru.

Nadhari ya pili:

-Suala la uzalendo halikutajwa kabisa kwani wote wagombea wote wa urais ni Wazawa,na wote ni weusi.Na kama lingeibuka CCM ndio walitakiwa kuumia nalo kwa vile tayari Kashfa za rushwa zilikuwa hewani na CDM walikuwa vinara wa kutibu Ufisadi, na kauli mbiu ilikuw atuongezeeni wapiganaji ili tukawatoe mafisadi.Huku Zitto na Slaa wakiwa na impressive records za kuibua mijadala makini Bungeni.Suala la TANU halikuibuka sana kama si kabisa.CCM haina hiyo impressive records kama wasomi mnavyojaribu ambia watu ktk media.Pengine hujaona watu vijijini wanavyochukia mabalozi wa CCM, wenye viti wa vijijini waliokuwa wakiamisha watu vijiji,kuwafunga magerezani hovyo,mateso ya kodi ya maendeleo,ufilisi wa mali za vijiji, etc>kwa ujumla CCM ilikuwa basi tuu hakuna mbadala.

Hizi nadharia zako ni za wasomi wa mjini na mara nyingine zimezaliwa na kukua katika midahalo na vitabu vya kijamaa vinavyokimbiliwa na wasomi wa leo.Baadaye wanarudisha habari katika media na kuwaaminisha wananchi kuwa walichokisia ndicho wanachofanya.wakati reality ndio wanafundishwa hivyo.

Pengine inaweza kuwa ngumu kwa watu hapa.Ila kuna hali amabyo katk sayansi ipo, amabpo kuna experiments nyingine ni ngumu kuchukua data kabla hujazichafua.Ubovu wa discussions zetu katika media na uandishi wa habari umefikia mahali naweza sema kuwa watu wanasoma data ambazo si za sample space ila ni zao we wenyewe.Yaani watu wanasoma kivuli/reflection yao wenyewe.Sikiliza midahalo bogus ya kwenye TV na radio yenye kuwahusisha wasomi hasa waadhiri wetu wa vyuo vikuu.Kwanza hawana definitions sahihi za vitu vingi.Halfu minds zao zinazunguka katika imani kuwa ujamaa ulikuwa the best thing in life na TANU was everything that tanzania has always needed to eterenity.mfano wa haraka ni neno "katiba" watu wamekuwa wakiongea vitu tofauti sana kati yao na vya kuchekesha sana.Kutokuwa na clear descriptions za vitu huwa kuna zaa watu wasio watendaji,kwani wakati wa kufanya kitu mtu anakuwa na mashaka na kutoweza fanya decision haraka na kwa usahihi na hii hupelekea guessworks.Baada ya guessworks mtu anakomaa hadi kufa akitetea ujinga wake kwa sababu tofauti tofauti zisizo husiana kujibu kitu kimoja.Tuna guessworks na copy and paste kila mahali tanzania leo.Mimi nimejifunza kwa vitendo namra nyingi nikijifunza kitu huwa naangai unique patterns kwanza kabla yakuja ktik generals.N ahii ni hata kwa wanamichezo kama soka wasipofanyi mazoezi vitu fulani ,basi wengi utakuwa wanapata kigugumizi katika pasi hajui apige au asipige,ampigie nani mwishowe anakuwa force kupiga kwa mashinikizo ya timu pinzani basi napiga pass isiyo clear kwa mwenzie na hivyo kupotea.

TANU ilijengwa kwa ujamaa na ujamaa wenyewe ni uovu kamili.Hakuna mahusiano ya maisha bora na ujamaa, hakuna uhusiano wa usitawi wa taifa na ujamaa.Sitaki kushwishika amini kuwa uchambuzi wako unaweza tumika vibaya kisiasa ila nakuhakikishia kuna watu wengi wataona kuwa unamrengo fulani.Wapenda ujamaa ni wapenda bure wengi walioishi chini ya state support,hata hao wahadhiri wnakumbuka enzi za elimu ya bure, hela za bure za research huku hawanyi kitu.Ila si ukweli wa maisha na big time failures za ujamaa.Mwalimu alikiri,ila alishindwa tuaminisha hivyo kwa vile hatupo tayari kwa hilo.

NI kawaida kabisa siku hizi, mtu wa CCM akaenda katik mdahalo kwa vile hajiamini kwa alichokwenda jadili kwa mtazamo wa CCM basi hoja zikianza kuwa kali ukamwona anahamia upande wa msomi wa chuo,tena km alikuwa mwalimu wake basi, anaishia changia something hakijui,na kama huyo mhadhir naye ana rafiki yake asiye na elimu mbadala basi huishia aminisha wananchi vitu vingi.Na baadaye kwenda vichukua.
 
Nje kidogo ya mada yako, unafikiri uchaguzi huru ukifanyika leo kwa wagombea walewale wa urais wa 2010 kutakuwa na matokeo tofauti? Kwanini?
Na je watanzania wangapi wanaelewa tofauti za msingi kisera kati ya CCM na CDM?

Nashukuru sana kwa mchango wako mkuu; naomba nianze kwanza na maswali yako haya mawili ambayo ni muhimu sana na sidhani kama yapo nje ya mada kwani mada hii nia yake ni kupanuka zaidi kwani inahusiana na mwenendo wa wapiga kura na chaguzi zetu;

Kuhusu swali lako la kwanza, uchaguzi huru ukija leo, bado CCM itashinda kwa sababu, again and again huwa nasisitiza umuhimu wa Chadema kulitazama upya suala la kanuni ya uchaguzi kwamba mshindi ni mshindi; kwani kwa jinsi hali ilivyo leo, CCM (Kikwete) akishinda tena leo kwa 50.9% na Chadema (Dr. Slaa) kwa 49.1%, kwa kanuni ya mshindi ni mshindi, CCM itaibuka kidedea tena; ushindi wa Chadema sana sana utakuwa uundwaji wa serikali ya pamoja kwama ile ya CUF na CCM Zanzibar;

Moja ya masuala ambayo yananipa wakati mgumu kuchambua kwa kina the likelyhood ya matokeo ya 2015 na nini kitafuatia baada ya haya matokeo, hasa given the fact kwamba Chadema hawajaonyesha nia yoyote ya kujiandaa na matokeo yatakayopelekea uundwaji wa serikali ya pamoja iwapo matokeo ya Urais yatakuwa yamekaribiana sana; sielewi iwapo Chadema watakataa au watakubali ingawa this is a double edged sword, hasa kutokana na ukweli kwamba Chadema walishaweka msimamo wao kuhusu ndoa baina ya CCM na CUF zanzibar, hivyo sidhani kama watakuwa tayari kuiga hili, kwani itawapa mtaji mkubwa sana CUF;

Kuhusu swali lako la pili juu ya uelewa wa wananchi juu ya utofauti wa sera za CCM na Chadema (kimsingi), hakuna utofauti wowote kwa kweli, kwani both CCM na Chadema wanatekeleza sera zile zile za soko huria, na hata Chadema ikienda Ikulu, itatekeleza yale yale, tofauti pengine itakuwa ni usimamizi bora zaidi, uwajibikaji zaidi, na kupungua kwa ufisadi, lakini hizi sio sera zenye mashiko, sera zenye mashiko ni zile za kutekeleza matakwa ya soko huria - hasa ubinaifishaji, marketization and liberalization, vitu ambavyo wote CCM na Chadema have fallen in love with, taabani;

Ushindani wa kisiasa nchini umetawaliwa na ombwe la kiitikadi, na hii inapelekea vyama vingi kutokuwa na utofauti mkubwa ki-sera, ukiachilia CUF ambacho ingawa itikadi yake nayo ni ya uliberali kama ile ya Chadema, na kama ile ya CCM ya vitendo (nadharia, itikadi ya CCM bado ni Ujamaa);

Baada ya kujibu maswali yako, naomba nirejee kwenye hoja yako kuhusu hoja ya nicholas juu ya masuala mengine ambayo yali influence matokeo ya uchaguzi 2010 lakini sikuyajadili; suala la upigaji kura based on ukanda, ukabila, n.k, nilijumuisha katika dhana ya LOCALISM, ambayo kwa bahati mbaya nadharia tete nilizoziweka hazijapata nafasi ya kujadiliwa; pia nilipouliza maswali yangu yale manne, hasa lile juu ya PERSONALITIES, hasa kwenye chaguzi za ubunge, humu pia nilipanga kujadili masuala ya udini, ukabila, ukanda, lakini pia kwa bahati mbaya maswali yale hayajapata muda wa kujadiliwa; vinginevyo masuala haya ni obvious, ni kwamba tu sikutoa ufafanuzi;

Mwisho ni hoja yako kwamba wapiga kura wana hulka ya kuadhibu wabunge kwa kutotimiza ahadi zao/matarajio yao; hii ni kweli ila only to an extent kwani matarajio ya wapiga kura yapo mengi sana na yanatofautiana sana; kwa mfano, kwa majimbo ya mijini kama vile Kinondoni, au Ilala, kitendo cha mbunge kuwa karibu na wananchi kama vile kuwaalika kibarazani kwako na kunywa nao kahawa, kwenda magengeni na kunua mandazi kwa mama lishe n.k, inakidhi sehemu kubwa ya matarajio ya wengi kwamba mbunge fulani ni mtu wa watu, huku majimbo mengine masuala haya hayatoshi kukupa ubunge, hasa maeneo ambayo maendeleo ya kiuchumi na kijamii ni duni; ningeomba kama utapata muda unipe mawazo yako kuhusu nadharia tete nilizoweka kwenye my original post;
 
Mkuu Nicholas,

Nashukuru kwa mchango wako kuhusu nadharia; kimsingi nimekuelewa, ila nadhani wewe umezitazama zaidi nadharia hizi kama issues ambazo zilikuwa zinawekwa wazi na wagombea majukwaani; maana yangu nyuma ya nadharia hizi ilikuwa ni kujaribu kupima na pia kubaini mwenendo wa wapiga kura, hasa their decision making process when it comes to voting for wagombea ubunge vis-a-vis urais; zilikuwa ni hypotheses za uchokozi tu and nothing close to academic standards kwani sijafanya research kihivyo, na badala yake im trying to come up with theory from the ground kwani sina existing theoretical framework to aid my analysis;

Kuhusu ujamaa kujaa uovu, sishangai sana kuhusu hoja yako kwani inaeleweka; lakini vile vile ubepari nao umejaa uovu; lakini muhimu zaidi ni kwamba, katika mifumo yote hii, hakuna anywhere ambapo inasema kwamba premise yake itakuwa ni kunyonya, unfair exchange, n.k, na badala yake ikitokea hivyo, ni kutokana na dynamics za mifumo yenyewe, hasa actors involved; ningependa ku-share quote moja ya mwanazuoni aitwaye Green ambae alimjadili Nyerere na Adam Smith kama ifuatavyo:

["Mwalimu's overriding concern in respect of Economics and Political Economy is very similar to one of Adam Smith's main concerns. Smith, who styled himself as a moral philosopher, believed for both practical and normative reasons that no nation could be great and prosperous if the majority of its people were poor and miserable. He contended that it was a primary duty in ‘moral economy' to enable them to escape from what we would not call absolute poverty, and that making this possible is the primary economic duty of the State. On the particular functions of the state, Smith and Nyerere (in very different contexts) certainly did not come to similar conclusions. Even so, Smith's very similar moral distaste for collusive behavior by entrepreneurs of self – enrichment and by economic power clusters turning the state into their tool is almost as robustly and repeatedly states as Nyerere's has been."]

Na mwisho, kuhusu mimi belonging to mrengo fulani, we all do, none of us float as a molecule kwani our beliefs, thoughts, views...definitely have certain ideological inclinations, even though we may not necessarily be aware of that; As of me, i believe in Social Democracy;
 
Mkuu Nicholas,

Nashukuru kwa mchango wako kuhusu nadharia; kimsingi nimekuelewa, ila nadhani wewe umezitazama zaidi nadharia hizi kama issues ambazo zilikuwa zinawekwa wazi na wagombea majukwaani; maana yangu nyuma ya nadharia hizi ilikuwa ni kujaribu kupima na pia kubaini mwenendo wa wapiga kura, hasa their decision making process when it comes to voting for wagombea ubunge vis-a-vis urais; zilikuwa ni hypotheses za uchokozi tu and nothing close to academic standards kwani sijafanya research kihivyo, na badala yake im trying to come up with theory from the ground kwani sina existing theoretical framework to aid my analysis;......
Na mwisho, kuhusu mimi belonging to mrengo fulani, we all do, none of us float as a molecule kwani our beliefs, thoughts, views...definitely have certain ideological inclinations, even though we may not necessarily be aware of that; As of me, i believe in Social Democracy;
Nashukuru kwa majibu:pengine sijaeleweka au kwa vile hatukuweka references ila ndhani tulikuwa wote tunaongelea hizi parameters kwa upande wa wapiga kura na si wagombea.

Nyerere alikuwa smart katika kuwapa watanzania dose ya ukweli wa failures za ujamaa.Ila kwa vile nia yake ilikuwa right na bado alishindwa and it was tool late. Hakuwa na sababu ya kuzilazimisha zifanywe vyema zaidi.Ujamaa unafaa sana kama utawekewa udicator na watu wakiwa na faith.

Ila by nature si practicle kwa vile binadamu ni selfish my nature. Kwa wanoamini dini ni kwamba Mungu kila alipomkabithi mtu kitu alimwambia "chako" si chenu.Kuhimiza utawala. Kwa ujamaa somewhere unatunza wanyonyaji ambao wanakuja jenga kutoaminiana na mwishowe kukolapse.

Ila kila mtu akimiliki mali yake hutumia akili na nguvu nyingi kujenga himaya yake.Kwa ujumla ujamaa hauna motivation, kwani juhudi zako zinavuna sawa n asiyewajibika.

Umewahi jiuliza kwanini wengine wan wake 8 na watoto 30 wakati wengine wana watoto 2 ila wote wakifaulu wanaingia university, wote wanatibiwa hospital, halafu unakuja kuta mwenye watoto wengi kazi wala hana kitu kinachokatwa kodi.

Ila kulipia na kumanage gharama kwa mtu binafsi kunamlazimisha kuzaa kwa mpano,kufanya kzi kwa bidii ili kuweza jikomboa. Namwishowe kutonyonya wengine.

Kuhusu mrengo inabidi nipige kimya kwani jibu la Social Democracy halitoshi sana. Ni kama mtanzania kujiita mwafrica kati ya watanzani.
 
Mchambuzi suala la ukabila sikulitaja kwani CDM wamelivunja sana. Lema kachaguliwa Arusha yeye ni mchaga na waarusha wamekuwa wakililaani hilo tangu enzi ya Mrema,

Mnyika kachaguliwa dar sidhani kama katoka kabila ambalo ni majority, Mr II kachaguliwa mbeya ingawa ni msafa na wasafa wametawanywa na kuwa diluted na maendeleo ya mji huku Wanayakyusa walio wazalendo sana wakiwa tayari wana idadi kubwa mjini.

Katika list Ya wabunge wa CDM kuna mchanganyiko mkubwa sana wa watu wa majimbo husika na wengine ni wageni katik jimbo.

Na hili Pia liliwahi vunjwa na Makongoro Nyerere Arusha.Sehemu za pwani dini na ukabila ungekuwa ni issue ila matokeo yanaonyesha kumfaidisha sana CUF, na CUF walimsaidia Kikwete katik hili .

Sasa hapa localism ni second,ilimnyima CDM ila ilikuwa ikimfaidisha CUF.CUF akapiga transit kwenda kwa KIkwete (CCM).
 
Mkuu Kobello,

Nashukuru kwa mchango wako; unaposema kwamba wapiga kura tanzania hutazama personalities kwa sababu vyama havina itikadi zinazoeleweka wazi, lakini hasa zinazouzika kwa wananchi walio wengi, nakubaliana na wewe kwa hili mia kwa mia; lakini pale Dr. Slaa anaposema kwamba kwa kawaida Chadema inajadili masuala na sio watu, kwa mtazamo wako, Chadema ifanye nini kuboresha kile anacholenga kukijenga Dr. Slaa, hasa katika mazingira ya itikadi bora na sio bora itikadi? Kwani ni dhahiri kwamba kwa Sasa Chadema hawana itikadi bora, bali bora itikadi; same applies to CCM;

Nimependa pia hoja yako kuhusu mwamko wa wapiga kura uchaguzi wa 2005, kwani unazidi kushindilia hoja yako kwamba mwenendo wa wapiga kura wengi Tanzania ni kuchagua WATU, na sio chama wala masuala yanayosimamiwa na Chama; Kuna ukweli katika hili, lakini je, nini mtazamo wako kuhusu upigaji kura kwa wabunge kwa vigezo nilivyojadili vya LOCALISM vis-a-vis vigezo vya NATIONALISM kwa nafasi ya Urais?
Mkuu Mchambuzi ukiangalia kwa undani zaidi, CDM ni chama kinachozungumzia watu kuliko masuala. Hakuna chama kinachotaja watu kwa majina, kina list ya mafisadi, kina list ya kila aina. Wangekuwa ni watu wa kujadili masuala wangetuambia jinsi gani wangeunda mfumo wa serikali unaozuia rushwa, kwani hiyo list wala haifiki 1% ya wala rushwa Tanzania.

watanzania hawachagui wabunge locally, bali ni sheria ndiyo inawafanya wawachague wabunge locally. Mohamed Dewji akitaka jimbo la Kibaha atapata na Slaa akitaka Mvomero atapata.

kwa hiyo mimi nadhani kuwe na chama mbadala (Meanig radically mbadala) hivi vilivyopo ni sawa tu!!
Na watu ni walewale. Angalia voting records zao ndiyo utagundua namaanisha nini.
 
Mkuu Mchambuzi ukiangalia kwa undani zaidi, CDM ni chama kinachozungumzia watu kuliko masuala. Hakuna chama kinachotaja watu kwa majina, kina list ya mafisadi, kina list ya kila aina. Wangekuwa ni watu wa kujadili masuala wangetuambia jinsi gani wangeunda mfumo wa serikali unaozuia rushwa, kwani hiyo list wala haifiki 1% ya wala rushwa Tanzania.

watanzania hawachagui wabunge locally, bali ni sheria ndiyo inawafanya wawachague wabunge locally. Mohamed Dewji akitaka jimbo la Kibaha atapata na Slaa akitaka Mvomero atapata.

kwa hiyo mimi nadhani kuwe na chama mbadala (Meanig radically mbadala) hivi vilivyopo ni sawa tu!!
Na watu ni walewale. Angalia voting records zao ndiyo utagundua namaanisha nini.

umeongea vizuri ila hapo kwenye red,kuna mushkeli...CDM kil awakisema kitu hutakiwa toa ushahidi,N ahuwezi toa ushahidi bila mtaja mtu.Bila hivyo atakuzimisha kwa kauli nyepesi tuu mzushi na mchonganishi.Mara nahatarisha amani. So pia ufikirie hilo.

Ila kw aujumla nasafi zao, na mtandao wao wote ndio unajengwa ushaidi wa jumla kama unavyosikia neno kama "CCM ni mafisadi" yaan unakuwa na ushahidi kuwa watendaji wakuu wote wa muhimu kwa CCM wameshiriki na wanalindana.

Tuwe fair.Hata humu ndani kuulizwa reference au picture ni haraka sana.sasa utaletaje picture bila mtu?Mbaya ni kualala katika huyo mtuu forever hata kama amekiri kuwa kweli alikosa na kuingia katik sheria.
 
Hoja zako ni nzuri sana Mchambuzi. Kama ulivyoainisha kuwa iwe mahali pa CDM kujipanga wakati wa kuelekea 2015, ni vyema pia tukatafakari kwa kina yaliyotokea kwenye uchaguzi uliopita.

Hivi leo tukijiuliza, ilikuwa je, Maalim Seif S Hamadi ashindwe kura za Urais Visiwani, na wakati huo huo Prof Lipumba amshinde JK kwenye kura za Urais za Visiwani?

Kila ninapo tafakari hili, linaniondolea uwanja tambarare wa kusema kweli hizi margins za ushindi wa JK dhidi ya Slaa zilikuwa sahihi. Je, Kweli Lipumba alikuwa Maarufu kuliko JK visiwani na wakati huo huo Shein akawa Maarufu kuliko Hamadi visiwani?

Lkn kama ulivyosema, kwa kuwa hakuna data inakuwa vigumu kuyafanyia kazi. Hii inanikumbusha pale Mzee wa Mapesa alipokosa hata kura za familia yake ya karibu sana (mkewe na wanawe) katika kituo chao cha nyumbani!
 
makala ya mchambuzi liko somo la kujifunza pamoja na uchakachuaji unaosemekana ambao kwa namna fulani unafanya matokeo yalioainishwa na mchambuzi yasiwe katika usahihi wake lakini kwahayo matokeo pawe ndio pakuanzia halafu nanjia zigine zakukabili NAhayo mengine likiwemo na hilo la uchakachuaji isiji ikiwa CCM WAKATUMIA hesabu hizo kuumiza CDM MWAKA 2015
 
Mkuu Mchambuzi nimependa jinsi ulivyowasilisha hii hoja na kutokana na hivyo imenifanya nijue mengi zaidi...kwa mfano mbinu chafu walizokua wanatumia C.C.M kama vile za kuwaaminisha wananchi kua CDM ni chama cha wakristo,ukichagua CDM kutakua na vita,CDM ni chama cha kikabila na nyingine nyingi ambazo kuzitaja zote ni upotevu wa muda.

Kuna ukiukwaji mwingine uliofanywa na CCM ambao ni kutumia vitu vya kiserikali katika kampeni kama magari na naamini hata pesa,kutoa rushwa wakati wa kampeni na uchaguzi,kununua vitambulisho vya kupiga kura kwa wananchi ambao wanasadikiwa wanashabikia vyama vya upinzani.

Pia bila kusahau mapungufu makubwa ya tume ya uchaguzi ambayo ilikua inaelemea upande wa CCM kwa asilimia kubwa huku ikikandamiza upinzani,wakurugenzi ambao walikua ni wasimamiz wa uchaguzi kua upande wa CCM.

Kutokana na hayo yote bila kulizungumzia suala la uchakachuaji wa matokeo ambapo mtoa hoja hakutaka tuliweke hilo kwasababu ambazo zinaeleweka na mimi binafsi nimezikubali inanifanya nifikie kuamini lifuatalo....CHADEMA ILISHINDA KITI CHA URAISI NA VITI VINGI VYA UBUNGE 2010 KAMA UCHAGUZI UNGEKUA HURU NA WA HAKI.

Mwisho...nakushukuru mtoa mada kwa kunifanya niwe na uhakika na kitu ambacho mwanzo nilikua na mashaka nacho...na pia sorry kama nitakua nimekwenda nje na ulivyokua unapenda tujadili.....
 
Kwa Maoni yako mkuu Mchambuzi Chadema wajipange sawasawa kuingowa CCM katika uchaguzi ujao ama sivyo CCM itakuwa inatawala daima.
Nakukubali mchambuzi hilo jina lako limekufaa, uchambuzi wako utavisaidia vyama vyote kuwa na focus nzuri ya 2015. Kutokana na CDM kuwa na mikutano nchi nzima wakati vyama vingine havifanyi mikutano regulary inaweza kuwaderail na kuona kwamba wameshapata ushindi wa urais 2015.

Lakini bado kazi kubwa ipo, kuna mashabiki wengine hawakutaraji kwamba CUF wangeweza kujaza uwanja wa jangwani kutokana na hoja kwamba hicho chama kimekufa. Baada ya mkutano hule ni vema wapinzani wakabuni strategies bora za kukamata nchi amasivyo T2015 CCM
 
Mkuu Nicholas,

Asante kwa mchango wako. Nikianza na hoja yako kuhusu impracticality ya Ujamaa, upo sahihi; Lakini pengine nikuulize, after the demise of Ujamaa: What kind of Country are we building at the moment? Na kama jibu kwa swali hili lipo, Je, vyama vyetu vya siasa, hasa vyama vikuu viwili vya sasa yani CCM na Chadema Vinatekeleza hayo? Binafsi sidhani kama CCM na Chadema wana majibu yenye mashiko juu ya hili, ni kama vile wote wanaendesha siasa za liwalo liwe.

Nasema hivi kwa sababu sioni mkakati kwa mfano wa Chadema unaoashiria kwamba kuna mpango wa kulijenga taifa hili upya from Bottom – up, badala yake kuna kila dalili kwamba utaratibu utakuwa ni ule ule wa Top-bottom kutekeleza matakwa ya neo-liberal policies za wakubwa wa nje ambao wanashirikiana na mafisadi kumaliza nchi yetu hivi sasa. Nionavyo mimi, iwapo Chadema itaenda ikulu 2015, sana sana watakachoweza fanikisha ni kupunguza mianya ya rushwa in the process of further implementation of neo-liberal policies, strengthen dhana ya uwajibikaji, and strengthen the issue of RULE OF LAW unlike now chini ya katiba mbovu ya sasa - which is more based on RULE BY LAW. Nje ya haya, watanzania wasitegemee maajabu kutoka Serikali ya Chadema, ingawa ni dhahiri Chadema will perform better than CCM in terms of governance (not sure about leadership – CCM has failed on leadership, Chadema faces serious challenges on that front).

Rais mstaafu – Benjamin Mkapa made a very fundamental point ambayo kwa bahati mbaya iliishia hewani badala ya kufanyiwa kazi kijamii, kwani kwa mtazamo wangu ilitakiwa izae mjadala wa kitaifa ambao ungetusaidia tujirudi na tujitambue tena kama taifa. Katika semina moja ya viongozi wa vyama vya siasa Mkapa alisema yafuatayo (source – moja ya makala za Issa Shivji):

["I earnestly urge that the market or free economy, together with political freedoms and freedom of the press should not be the beginning of the weakening of our unity, national solidarity, and should not dilute our nationalism, union and udugu. The market economy will result in some of us becoming richer than others. Political freedom has brought many parties and their many honorable leaders. But this should not be the reason for some to feel better than others. We, Tanzanians should remain ndugu.our udugu is not ideological rather it is embedded in our African culture."]

Kuna suala moja muhimu sana that's worth mentioning: Neo – Liberal policies tunazoendelea kuzitekeleza tangia mid 1980s ni moja ya sababu kubwa sana juu ya kwanini watanzania wanazidi kuwa ‘polarized' Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii. Ni muhimu kama taifa, tuanze ujenzi wa taifa letu upya, kabla haijawa too late. TANU ilijaribu kufanya hili kwani harakati za uhuru was a mass movement. Harakati za Chadema leo i.e. M4C, zitakuwa na manufaa sana kwa taifa letu iwapo zitapelekea for a new independence katika nchi yetu, hasa ‘economic independence', vinginevyo tutarudi kule kule kama vile TANU ilivyo fail.

Mara nyingi huwa najiuliza, pamoja na umuhimu ake, Je M4C inalenga kipi hasa kati ya hivi – Social Change? Political Independence? Economic independence? Itakuwa jambo la maana sana iwapo jibu ni both, hasa iwapo Chadema will go an extra mile and ‘lay out' before watanzania, kwa ufasaha kwamba kama Taifa - Tumetoka wapi, Tupo wapi, Tunataka kwenda wapi, na Tufanye nini kufika huko. Chadema ikifanya hivyo kwa ukamilifu, very soon chama hiki kitageuka kuwa a mass movement ya kweli, kwani watanzania wengi sana wanatafuta mbadala wa CCM sasahivi lakini mbadala wa uhakika uahpo. Muhimu pia hapa ni kwamba, Chadema inatakiwa kufahamu kwamba watanzania wengi zaidi (voters) bado wapo in the ‘swing' column in terms of kuunga mkono between Chadema na CCM, kwani total number ya wanachama wa vyama vyote 19 Tanzania sidhani kama inafika hata milioni kumi.

Mkandara kwenye waraka wake kwa uongozi wa Chadema made a very fundamental point. Alitamka kwamba – operesheni ya Vua Gamba, Vaa Gwanda ina mapungufu kwani lengo lake ni kugeuza wanachama wa CCM kuwa wanachama wa Chadema. Akahimiza juu ya umuhimu wa Chadema kuanza kulenga wapiga kura waliojiandikisha, sio wanachama wa CCM. This is true kwani wanachama wa CCM ni kama milioni saba, wakati wapiga kura kwa mujibu wa database ya 2010 wapo milioni kumi na nane. Hii ina maana kwamba katika operesheni vua gamba, vaa gwanda, Chadema inalenga less than one third ya wapiga kura Tanzania i.e. about 27%.

Kwa mwenendo wa demographics za sasa za nchi, haitakuwa ajabu wapiga kura Tanzania mwaka 2015 wakafikia kati ya milioni 20 na milioni 22. Pia ni dhahiri kwamba by 2015, wanachama wa CCM watapungua pengine kufikia milioni tano, nne or less. Sasa tuseme kwamba wanachama hawa wa CCM by 2015 wapungue kufikia milioni nne katia ya jumla ya wapiga kura tuseme milioni 22, ina maana Vua Gamba, Vaa Gwanda itakuwa inalenga only 18% ya wapiga kura kuelekea mwaka 2015. Tuseme Chadema manages to secure wapiga kura wake wa 2010 i.e about 2.5 million; na tuseme kwamba Chadema ikafanikiwa kuvuna 25% ya wanachama milioni nne wa CCM ambao ni watu milioni moja; na tuseme Chadema ikafanikiwa kuongeza wanachama wengine milioni mbili katika kipindi hiki cha miaka mitatu heading towards 2015, ina maana Chadema itaingia 2015 ikiwa na supporters wa uhakika between 5 and 6 million. Idadi hii itakuwa sawa na less than one third ya wapiga kura wa 2015 i.e only 27%. Sasa ikitokea CCM ikaweka mtu ambae ataleta mvuto wa wapiga kura kama ilivyotokea 2005, Chadema itavuka?

Mimi nadhani hata CCM ikiweka mgombea mwenye mvuto wa wastani, kwa mahesabu haya na kwa kanuni ya mshindi ni mshindi, CCM kupata ushindi wa 50.1% dhidi ya Chadema 49.9% ni kitu kirahisi sana. Na hii inaweza pelekea serikali ya umoja wa kitaifa, suala ambalo litakuwa ni msiba kwa Chadema kisiasa. Na wakikataa hili, propaganda dhidi ya Chadema kwamba kimekataa ridhaa ya 49.9% ya wananchi will also finish Chadema. Changamoto kwa Chadema ni kubwa mno.

Moja ya mikakati ya kuisaidia chadema katika hili iwe ni pamoja na matumizi ya dhana za marketing, kwani modern politics sasa zinaendeshwa kisokosoko. In marketing wanasema the most important customer it the returning customer, not the new customer kwani huyu mpya anaweza asirudi tena. Chadema should focus to keep its 2 million or so votes za 2010, huku ikitafuta wateja wapya kwa mtazamo wa mkandara, kwani kwa kweli wapiga kura wengi as I said earlier ni undecided (rejea idadi ya wapiga kura Tanzania versus wanachama wa CCM).

Last but not least, niseme tu kwamba, ni dhahiri watanzania wengi wamechoswa sana na utawala wa CCM, lakini kwa bahati mbaya, hizi neo-liberal policies ambazo ndio zimefungua mlango wa ushindani kisiasa (democracy etc), haven't generated any new National Vision that inspires and mobilizes watanzania SUSTAINABLY. Chadema wakifanikiwa kuja na DIRA yenye sifa hizi, their support, strength, and prominence in Tanzania's politics WILL ENDURE & SUSTAIN. Na njia ya kupata DIRA yenye sifa hizi ni kuja na DIRA ambayo ni Radical (jambo ambalo nadhani hata kobello or someone humu aligusia kidogo), especially one that challenges the current arrangement ya soko huria. Nje ya hapo, tutaendelea kuwa na malengo ya kujadili MASUALA badala ya WATU, lakini baada ya muda mfupi, Chadema itaishiwa MASUALA na kurudi kwenye mijadala ya WATU. Hata wananchi nao wataiga mtindo huo pale watakapoanza kusema "HAWA WATU WA CHADEMA WAMEKAA IKULU MIAKA MITANO/KUMI LAKINI HALI ZETU BADO NI MBAYA.

Ikifikia hatua hiyo, itakuwa ndio the window for CCM to regain utawala wa nchi perhaps for the next 100 years, and Chadema ikitoka ikulu sioni jinsi gani itarudi tena, hasa ikizingatiwa kwamba Chadema na vyama vingine vyote ni vyama vya Tanzania wakati mjenzi wa Tanzania ni CCM. Chadema, TANU (1961-1977), NCCR, CCK…, vyote hivi ni vyama vya Tanganyika. Kauli yangu hii isipoeleweka vizuri, nitaonekana ni mbaguzi na mpinga muungano. That's not the case, bali muungano ni kiini macho kama kaka yangu Tundu Lissu alivyotamka bungeni lakini kama kawaida yetu, akaonekana ni mwehu. Ninaandaa makala ya kuunga mkono hoja ya Lissu kwani hakueleweka na akaishia kuonekana ni mbaguzi, mwehu, na mtu anayepinga umoja, lakini hasa muungano.

Mwisho bwana Nicholas ni juu ya hoja yako kuhusu my ideological orientation. Kwa kifupi, mimi sina ugomvi na ubepari, lakini utekelezaji wake. Mkandara amekuwa pia analizungumzia hili kwa undani sana; Mimi nina amini katika itikadi ambayo ina uwezo wa kulikemea soko linapokwenda mrama au linapotumba na kuleta madhara kwa mwananchi wa kawaida. Na itikadi pekee ya kufanikisha hilo, in my view, ni ile ya social democracy; ukipata muda jaribu soma uzi wangu mwingine kwa kubofya hapa: https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/215953-nape-mnyika-mtatiro-wapi-itikadi-zenu.html
 
...kwa hiyo mimi nadhani kuwe na chama mbadala (Meanig radically mbadala) hivi vilivyopo ni sawa tu!!

Kobello,

Nimevutiwa na hii hoja uliyotoa. Ukipata nafasi naomba ufafanue kidogo kwani inaweza kutusaidia kubaini mapungufu yaliyopo ndani ya CCM na Chadema all together;
 
Nakukubali mchambuzi hilo jina lako limekufaa, uchambuzi wako utavisaidia vyama vyote kuwa na focus nzuri ya 2015. Kutokana na CDM kuwa na mikutano nchi nzima wakati vyama vingine havifanyi mikutano regulary inaweza kuwaderail na kuona kwamba wameshapata ushindi wa urais 2015.

Lakini bado kazi kubwa ipo, kuna mashabiki wengine hawakutaraji kwamba CUF wangeweza kujaza uwanja wa jangwani kutokana na hoja kwamba hicho chama kimekufa. Baada ya mkutano hule ni vema wapinzani wakabuni strategies bora za kukamata nchi amasivyo T2015 CCM

Asante sana kwa mchango wako mkuu. Ni kweli umati wa CUF umeshanganza sana watu; lakini umati wa Mrema 1995 pia ulishangaza watu, na hata Mwalimu Nyerere alishtuka sana. Lakini tatizo umati ule haukuweza deliver for Mrema inavyotakiwa; unadhani ni kwanini?
 
Niwe mkweli tu kuwa nimeisoma lakini sikuimaliza hii thread, so sitasema sana!!!!
 
Mkuu Mchambuzi nimependa jinsi ulivyowasilisha hii hoja na kutokana na hivyo imenifanya nijue mengi zaidi...kwa mfano mbinu chafu walizokua wanatumia C.C.M kama vile za kuwaaminisha wananchi kua CDM ni chama cha wakristo,ukichagua CDM kutakua na vita,CDM ni chama cha kikabila na nyingine nyingi ambazo kuzitaja zote ni upotevu wa muda.

Kuna ukiukwaji mwingine uliofanywa na CCM ambao ni kutumia vitu vya kiserikali katika kampeni kama magari na naamini hata pesa,kutoa rushwa wakati wa kampeni na uchaguzi,kununua vitambulisho vya kupiga kura kwa wananchi ambao wanasadikiwa wanashabikia vyama vya upinzani.

Pia bila kusahau mapungufu makubwa ya tume ya uchaguzi ambayo ilikua inaelemea upande wa CCM kwa asilimia kubwa huku ikikandamiza upinzani,wakurugenzi ambao walikua ni wasimamiz wa uchaguzi kua upande wa CCM.

Kutokana na hayo yote bila kulizungumzia suala la uchakachuaji wa matokeo ambapo mtoa hoja hakutaka tuliweke hilo kwasababu ambazo zinaeleweka na mimi binafsi nimezikubali inanifanya nifikie kuamini lifuatalo....CHADEMA ILISHINDA KITI CHA URAISI NA VITI VINGI VYA UBUNGE 2010 KAMA UCHAGUZI UNGEKUA HURU NA WA HAKI.

Mwisho...nakushukuru mtoa mada kwa kunifanya niwe na uhakika na kitu ambacho mwanzo nilikua na mashaka nacho...na pia sorry kama nitakua nimekwenda nje na ulivyokua unapenda tujadili.....

Mkuu Sarawati,

Nashukuru kwa mchango wako mzuri. Tukianza na suala la udini na siasa, mimi sidhani kama ni sahihi kwa CCM kujivunia kwamba sio chama cha kidini; wanachotakiwa kusema ni kwamba ni chama ambacho kinapigania utanzania bila ya kujali udini, ukabila n.k, na lazima pia kikiri kwamba vita hivyo lakini vimekuwa vigumu na havijafanikiwa kwa asilimia hata sabini; ushahidi upo wazi kwani kati ya masuala ambayo yanafanya muungano wetu kuyumba ni kwamba wenzetu wa visiwani wanahisi hawapewi nafasi za kutosha katika nyadhifa mbalimbali; hii ina maana kwamba pamoja na CCM kuwa na mikakati ya kupunguza udini katika masuala ya siasa na uongozi wa nchi, haijafanikiwa vya kutosha;

Kuhusu suala la Chadema na udini, nini ni kipimo kwa hili - je ni composition ya uongozi wake? je ni uungwaji mkono wake? je ni sera zake? Suala la Chadema na udini lazima lijadiliwe holistically, sio kwa ku brush brush tu; mimi ni mwana ccm lakini mpenda demokrasia, hivyo i share some sympathy na Chadema, hasa pale inaposhambuliwa kwamba ni Chama cha udini. Tukiangalia suala la siasa na udini holitically, CCM, Chadema, CUF, vyote ni vyama vya udini; lakini tukiangalia ki-sera, hasa zile zinazojaribu kuondoa udini katika siasa na uongozi wa nchi, both CCM na Chadema sio vyama vya kidini kwani the way they practice siasa zao haionyeshi kwamba wanalalia dini fulani, sana sana ni interpretations tu kutokana na mtazamo wa mtu; pengine nitaeleweka zaidi hapa kwa kusema hivi: Tanzania ni zao la CCM, lakini Tanganyika ipo, ingawa imefichwa kwenye kabati; Ili uweze kuwa chama rasmi na halali, ni lazima upate wadhamini kutoka TANGANYIKA na ZANZIBAR; lakini CCM ilishawapata hawa baada ya kuungana na ASP, na wengine ambao walikuja ona CCM sio safi, walianza movement yao ambayo ikaja kuzaa CUF; sasa kwa vile CUF ni chama cha taifa (zanzibar) ambalo over 75% ni waislamu, kwanini chama hiki kishutumiwe kwamba ni cha kidini? Je, kusema Zanzibar ni nchi ya watu milioni moja dhidi ya Tanganyika yenye watu milioni karibia 45, which means by default wanachama wengi wa CCM ni watu wa Tanganyika, tena wa vijijini ambako dini ya ukristo ni kubwa zaidi, ni sawa kusema CCM ni chama cha kidini? Kama ni sawa, then CCM ni chama cha kidini kama ilivyo CUF; na kama sio sawa, then sio CUF wala CCM ambacho ni chama cha kidini;

Chadema ni hivyo hivyo - base yake kubwa ni Tanganyika, na kikienda Zanzibar ambayo imeletwa na CCM kuja uwa sehemu ya taifa la Tanzania, basi kwenda zanzibar ni kwa ajili tu ya kutekeleza matakwa ya msajili wa vyama vya siasa; vinginevyo KISIASA, zanzibar ni nchi ya CCM (TANU+ASP), na pia CUF, na ni vigumu sana kwa Chadema kugeuza hili; ukanda wa pwani pia una akisi misimamo ile ile ya TANU, ASP, CUF, na ndio maana Chadema inapata wakati mgumu kidogo kupenya humo; Lakini jitiada za Chadema kupenya humo, kusimamisha wagombea yote ni ushahidi kwamba chama hiki hakina sera za udini;

kwa kifupi, Chadema sio chama cha kidini, lakini by default, lakini hasa kutokana na historia ya nchi yetu na siasa zake, support yake kubwa ipo Tanganyika, hasa hinterland, not along the coast, lakini hata huko hinterland, Chadema ina wanachama wa dini zote wengi tu kama ilivyokuwa CCM; kwahiyo sio sahihi kuiadhibu CCM au Chadema kwamba ni chama cha kidini kwa sababu ya make-up ya electorate inayowaunga mkono; badala yake ni kwa kuangalia deliberate policies kama zina inclinations za kidini;

Huo ndio mtazamo wangu, ingawa sijaupanga sawa sawa na inawezekana nisisomeke kwa ufasaha. lakini nipo tayari kufafanua pale itakapobidi;
 
makala ya mchambuzi liko somo la kujifunza pamoja na uchakachuaji unaosemekana ambao kwa namna fulani unafanya matokeo yalioainishwa na mchambuzi yasiwe katika usahihi wake lakini kwahayo matokeo pawe ndio pakuanzia halafu nanjia zigine zakukabili NAhayo mengine likiwemo na hilo la uchakachuaji isiji ikiwa CCM WAKATUMIA hesabu hizo kuumiza CDM MWAKA 2015

Asante sana Mkuu kwa mtazamo huo,

Nirudie tena tu kwamba, nia yangu kuja na mada hii ni kujenga a ground theory from scratch ambayo ingetusaidia kujua nini kilitokea katika kura za 2010 kwani ni dhahiri kwamba tukitumia muda wa kutosha kuchambua matokeo haya, moja na moja haitakuwa mbili, na soon tutabaini wapi inawezekana uchakachuaji ulitokea n.k; lakini naona wengi hawalioni hili au hawapo tayari ku work backwards towards the solution; Otherwise kung'ang'ania tu kwamba kura zilichakachuliwa bila ya kuwa na reliable framework to analyse hilo muda utazidi tu kwenda, takwimu zilizopo zitapuuzwa, and by the time watu wanagutuka kwamba kuna numbers ambazo ilitakiwa tuzifanyie kazi, its too late;
 
Back
Top Bottom