Chadema - na mtihani nilioupenda


G

GOTILANGU

Senior Member
Joined
Aug 23, 2013
Messages
182
Likes
0
Points
0
G

GOTILANGU

Senior Member
Joined Aug 23, 2013
182 0 0
Safi safi safi sana mnafanya paper zuri au jaribio sahihi la upimwaji wenu wa fikira sahihi na salama kwa mapinduzi ya maisha ya watanzania safi sana.Jamani jambo hili kwangu nalichukulia kwa fikira chanya ya maamuzi sahihi ya kwetu kama wananchi kukiamini chama hiki na kukipa nafasi kubwa kutuongoza katika mapambano haya ya maliasili na rasilimali za taifa , Utu wa Mtanzania , Elimu yetu ya div 5 nasikia itafika mpk div 7 , Afya zetu na maisha yetu kwa ujumla kwa kauli kuwa upande wa pili walishashindwa liko wazi.

Sababu zifuatazo zinanifanya niseme safi sana na ilitakiwa kuwa zaidi ya hapo

[1].Kuna watu walishapoteza maisha kwa ajili ya mapambano haya kupitia chama hiki hivyo basi chama hiki kinathamini damu hizi au wanaajenda ya Mtaji wa mwanasiasa ni watu na hata ikiwezekana maisha ya hao watu
[2].Je? hawa viongozi wanajua kuwa chama hiki kimefikishwa hapa na wananchi na sio wao au wao wanajua wao ndio waliofikisha chama hapa mwisho wa suala hili jibu litakuwa wazi bila kuhitaji macho matano kama mcheza mpira wa miguu
[3] Waliopewa madaraka kweli wanapaswa kupewa madaraka makubwa ikiwa kweli CHADEMA wakishinda maana hapa ukweli wa yanayoongeleka yatatupa nafasi ya kufanya tathmini sahihi ya ukweli na uwazi maana emotions na provokes zitatawala tu mbona hapa bado zaja sana sisi hapo tutapata fikira sahihi na maamuzi chanya juu yao
[4] Hivi kweli wananchi tuko serious tunahitaji mabadiliko ambayo ni muhimu au tunajidanganya kwa kutembea na taa usiku wa giza na je watu wanaelewa au wana elimu sahihi ya demokrasia ya vyama vingi au wanajiunga na vyama kama fashion tu au kwasababu fulani kafanya mazuri basi anatufaaa milele au fulani kafanya mabaya hatufai milele.
[5] Kama suala hili ni propaganda kutoka kwa master of propaganda na mwalimu wa propaganda ambae hata walioko huko aliwafundisha yeye basi kafanya la maana naamini baada ya hapa CHADEMA itakuwa chama cha mfano wa vyama vya upinzani na kitakomaa maradufu maana usaliti hautakuwepo,ushirikiano utazidi,lengo na sauti itakuwa moja kuheshimiana kutakuwa maradufu na usingizi kwa wapinzani utakuwa mdogo sana
[6] Taasisi imara inajengwa na watu imara na je? hawa ni watu imara sana na je? hawa viongozi wanaakisi na wanajali yale watuambiayo wakiwa majukwani au sisi ndio mitaji yao?

HITIMISHO

Kwa mtu sahihi na ambae kweli ni mwanamapinduzi hapaswi kuchukua uamuzi wowote kwasasa kama kuhama chama, kuandamana,kurudisha kadi maana mtu sahihi husimamia maamuzi yake hata kama ni mabovu kiasi gani? na yeye alifanya maamuzi kuwa mwanachadema maana hakuna mwenye hatimiliki na CHADEMA wananchi waambiwe wao ndio wenye chama watachukua maamuzi. Mwisho wa suala hili mbona bado na tathmini yakinifu mbno bado maana waliotoa maamuzi tumewasikia na ambao waliotolewa maamuzi bado hatujawasikia utetezi wao. Unaweza kuchukua uamuzi sasa halafu mambo yasije kuwa kama ulivyofikiri yaani picha yako itakuwa katika tafsiri yoyote itakuwa ni sahihi kabisa.Nakuwa namashaka na wanaochukua maamuzi yoyote sasa kwa sababu ya hili wananiachia mawazo mengi juu yao.

USHAURI

Tusifanye maamuzi yoyote sasa hivi hasa kwa wanachama wa CHADEMA huu si wakati wao bali ni wakati wa viongozi wao kuonyesha nini kilichopo na mzizi wake ni nini na kwa wanachama watakuwa wa mwisho kufanya maamuzi sahihi kwa manufaaa ya kwao lakini sio sasa.
 
H

Haji Salum

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2013
Messages
1,022
Likes
9
Points
0
H

Haji Salum

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2013
1,022 9 0
Kwa kweli Chadema inafanya vizuri! Hata kipofu anaona. Lakini kinachoniudhi ni hawa vibaka wa buku 7 kupinga kila kitu.
 
Dr.Mo

Dr.Mo

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2012
Messages
3,814
Likes
36
Points
145
Dr.Mo

Dr.Mo

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2012
3,814 36 145
CDM kimejipambanua kwa kufanya maamuzi thabit......yaani mtaani tunaita maamuzi ya KIUME.....hawacheki na kima....hongera sana
 

Forum statistics

Threads 1,250,617
Members 481,419
Posts 29,738,938