Uchaguzi 2020 CHADEMA na Mgombea Urais wa Tanzania Tundu Lissu, wahakikishieni watumishi wa Umma usalama wa ajira zao

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Wana JF;


1. Jana nilitupia uzi humu nikichambua mikakati ya CCM ya kujipatia ushindi haramu ktk uchaguzi mkuu huu nje ya ballot box kwa kuwatumia watumishi wa umma; walimu, manesi, madaktari wetu, polisi, TISS, DEDs, DCs na maRCs.

2. Mpaka sasa mgombea wa CCM, John Pombe Magufuli anaamini kuwa ataendelea kuwa Rais hata baada ya 28th Okt, 2020.

3. Watumishi wa umma hawa, nao kwa bahati mbaya sana wengi wanaamini kuwa John Pombe Magufuli ataendelea kuwa Rais wao na wako tayari kuisadia CCM ishinde sawasawa na maelekezo wanayopewa. Ni kwa sababu hawa ndiyo watakaokuwa wasimamizi katika vituo vya kupigia kura vyote.

4. Ambacho kimeshafanyika ni watumishi hawa wa umma kuanzia maRC, maDCs, DEDs, TISS, Polisi, walimu, manesi, madaktari, watendaji vijiji/mitaa wote nk nk wameshaambiwa WATAFUKUZWA KAZI kama watarimuhusu diwani ama mbunge wa uoinzani kutangazwa katika kata ama majimbo yao wanayosimamia.

Wameambiwa watumie kila njia "KUPINDUA MEZA" yaani kupindua matokeo ya kituo chochote cha kupigia kura, kata yoyote ama jimbo lolote aliloshinda mpinzani.

KWANINI HILI?
Ni kwa sababu, JOHN POMBE MAGUFULI anaamini ataendelea kuwa Rais wa nchi hii na hivyo kuendeleza udikteta wake, kukandamiza uhuru na haki za watu

NINI KIFANYIKE KUWEKA SAWA NA KUZUIA HILI?
Rais ajaye Mh. Tundu Antipas Lissu ahutubie taifa haraka na mapema iwezekanavyo kulieleza hili kwa ufasaha ili;

1. Awakikishie watumishi wa umma yeye ndiye Rais ajaye na kila mtu UHURU na HAKI yake italindwa

2. Awatoe wasiwasi watumishi wa umma na awahakikishie USALAMA WA AJIRA ZAO.

3. Wasikubali kushiriki UOVU wa CCM na MAGUFULI kwa kushiriki WIZI WA KURA ili kumsaidia mnyanyasaji na dikteta huyu kuendelea kubaki madarakani kwa sababu wataendelea kujifungia wenyewe katika gereza la mateso na utumwa.
 
Hao watumishi wa umma wote uliowataja hapo watampigia kura Lissu, hakuna hata mmoja mwenye hamu na Magufuli, nasisitiza wote kuanzia walimu, manesi, na wengine wote kura zao ni kwa Lissu.
 
Back
Top Bottom