CHADEMA na hasa timu ya Kampeni ya Tundu Lissu, pokeeni huu ushauri wangu kwenu kama mtaona unawafaa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,247
110,809
Niliamua Kiumakini kabisa kutenga muda wangu na kumuangalia kwa Jicho langu la Tatu Mgombea wenu wa Urais Mtani wangu kutoka Singida Mheshimiwa Tundu Antipasi Lissu na hatimaye nikajikuta 'nagundua' mambo kadhaa ambayo kwa nia njema tu kama Watani na Marafiki zangu nitawaomba muyasome, muyatafakari, muyafanyie Kazi na ikiwapenda anzeni 'Utekelezaji' wake

1. Mshaurini Tundu Lissu asitumie nguvu nyingi sana katika Kuongea kwani atachoka upesi mbele ya Safari Kampeni zikianza.

2. Mshaurini Tundu Lissu kuwa tunajua ya kwamba ana Hasira na 'Maadui' zake ila apunguze mno Kuhutubia kwa Kufoka atachoka.

3. Mshaurini Tundu Lissu kuwa akiwa anageuka wakati akihutubia asiwe anageuka 'Kishamba' kama Meli za Bandarini bali ageuke Kihotuba.

4. Mshaurini Tundu Lissu kuwa 99% ya Maongezi yake yawe ni kuhusu tu 'Issues' na siyo ajikite katika 'Personalities' kama sasa.

5. Mshaurini Tundu Lissu kuwa pamoja na kwamba anakuwa 'anahutubia' ila pia awe anawaangalia wana Usalama wake Kiumakini.

6. Mshaurini Tundu Lissu kuwa kutokana na sasa ameshapata 'Ulemavu' basi hata Kusimama Kwake Kuhutubia Jukwaani kuwe Kiasi.

7. Mshaurini Tundu Lissu kuwa ajitahidi sana maneno yake mengi yawe ni ya 'Kiushawishi' zaidi na siyo ya 'Kiuchochezi' itamponza.

Hakuna Simba bila Yanga na vile vile hakuna CCM yangu bila CHADEMA yenu, hivyo nimeyasema haya kama Upendo wangu Kwenu Watani zangu.
 
Kweli asitumie nguvu nyingi sana atachoka. Kampeni si lelemama ukizingatia ni nchi nzima. Asije akaanza kuumwa kwa uchovu.
 
Lissu anacheza na "SAIKOLOJIA" ya meku, anajua mzee baba hapendi kukosolewa wala kupingwa kwa maneno makali, anapenda kusifiwa tu. Hivyo anatumia juhudi kumsugua roho na dodoki la steel wire. Ukimsukuma kidogo tu meku, hua gari linawaka (anaanza mipasho ya kejeli).

Na meku kawaida yake akikosolewa kidogo tu anashindwa "KUJIZUIA" jazba. Lissu anafanya juhudi kumjaza "UPEPO" mzee baba ili aripuke, na mzee baba huko alipo anajaa upepo kisawasawa moyoni (hii itamletea madhara makubwa sana meku kwasababu ya ule ugonjwa wake alionao kiafya - mara pap tutasikia amepelekwa South Africa kwa matibabu).
 
Najiuliza mara kwa mara hasa namba 6, kama NECwatakuwa makini huenda wakatenda ya kwao.baadhi ya kada zinazingatia haya mambo madogo madogo!
1. Jeshi
2. Wachungaji hasa Mapadri
3........
 
Kweli asitumie ngugu nyingi sana atachoka. Kampeni si lelemama ukizingatia ni nchi nzima. Asije akaanza kuumwa kwa uchovu.

Na ndiyo maana kwa Mapenzi yangu mema Kwake Yeye na kama Mtani wangu wa Singida na Watani zangu CHADEMA nimewatahadharisha upesi.
 
Lissu anacheza na "SAIKOLOJIA" ya meku, anajua mzee baba hapendi kukosolewa wala kupingwa kwa maneno makali, anapenda kusifiwa tu. Ukimsukuma kidogo tu meku, hua gari linawaka (anaanza mipasho ya kejeli).

Na meku kawaida yake akikosolewa kidogo tu anashindwa "KUJIZUIA" jazba. Lissu anafanya juhudi kumjaza "UPEPO" mzee baba ili aripuke, na mzee baba huko alipo anajaa upepo kisawasawa moyoni.

Sawa ila mwambieni aende taratibu kwani kuna tofauti kubwa kati ya anayesubiria Ndege JNIA na anayesubiria Basi la Mikoani Ubungo Terminal.
 
Mshauri mgombea wenu aache ubabe akubali kukosolewa.
Mshaurini awaheshimu na kuwapa nafasi viongozi Wendie asipende wamtetemekee.
Mshaurini ajifunze kiingereza atahojiwa navyombo vya kimataifa Kwa kiinglish.
Mshaurini asitishie wananchi walioamua kuchagua kiongozi wachama pinzani.
Mshaurini asijenge chili na washindani wake na kutumia Dola kuwakandamiza.
Mshaurini asijione wapekee Kuwa hakuna mwingine anayeweza zaidiyake.
Mshaurini maisha yawatu yakizidi Kuwa magumu hata ajenge kitugani hatokubalika.
Mshaurini asikilize sera mbadala kwaumakini maana nchi niyetu sote.
Mshaurini haki huinua taifa hivyo aitende ikiwamo pia uchaguzi Kuwa huru na wazi.
Mwambieni push-up siohoja na kampeni so show za fiesta kujaza wasanii.
Mwambieni Elimu ndiyo ufunguo wa mafanikio, bora isiwe bure Bali iwe bora na watoto lazima wale shuleni
Mwambieni uhuru wetu nifahari yetu hatutaki kiongozi anayetu/wanyima wananchi haki
 
Mkuu agiza kitu cha pepsi walahi
 
Writing is the combination of art (creativity) and innovation. write sense or otherwise nobody will take you seriously. Go to school and get a descent job. Cretin!
 
Back
Top Bottom