Habari wanajamvi, kumekuwepo na video clip ikisambaa mtandaoni ndugu Tundu Lissu akiomba apigwe tafu, naamini tupo watanzania wengi ambao tupo tayari kuchangia chochote kadiri ya uwezo wetu. Tunaomba uongozi wa chama au familia utupe utaratibu wa kuchanga kwa kutupatia namba ya M-pesa, tigo pesa, airtel money au account namba ya bank tuweze kumchangia mtanzania mwenzetu aliyenusirika kifo kwa watawala wasiopenda ushindani. Cc Moderator Uongozi wa jamiiforum tunaomba mtusaidie kutupatia uthibitisho wa account na namba za simu tutakazopatiwa, shukrani