MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Wascotland wana methali inayosema"Give a Dog an ill Name, and he'll soon be hanged’’.
Hii methali imekuwa ikitumiwa sana wakati wa harakati za uchaguzi ndani ya CHADEMA kwa wagombea ambao malengo na mitazamo yao inapingana na uongozi wa juu wa chama.
Mwanachama ambaye anaonekana kuwa na malengo na mitazamo tofauti ndani ya CHADEMA amekuwa akipewa na viongozi wa juu majina ya PANDIKIZI au MSALITI huku wakishirikiana na kundi walilounda halafu baadaye wanachama wengine wanaaminishwa kama ni pandikizi au msaliti ili wamshughulikie.
Tuliona mwaka 2013/14 ilivyokuwa wakati wa harakati za uchaguzi ndani ya CHADEMA ambapo Zitto Kabwe alionyesha nia ya kutaka kugombea Uenyekiti wa CHADEMA Taifa ambapo alipewa jina la PANDIKIZI na MSALITI na akashughulikiwa kweli kweli mpaka akaamua kukimbia kabla hajafukuzwa rasmi.
Kwenye maandalizi ya uchaguzi ndani ya CHADEMA tuliambiwa CHADEMA inamuhitaji sana Mbowe wakati huo kwa sababu chama kiko kwenye mafanikio makubwa ambapo kinaenda kitachukua dola kwenye Uchaguzi Mkuu 2015. Tukaambiwa Zitto ni PANDIKIZI na MSALITI kwa sababu ametumwa na CCM ili kuhakikisha CHADEMA haishiki dola mwaka 2015.
Kama ilivyo methali, Zitto alinyongwa kisiasa mpaka kuimbia CHADEMA na mengine ni historia!
Kwa njia ileile iliyotumika kumnyonga Zitto kisiasa, ndivyo hivyo kwa sasa inatumika kumnyonga Cecil Mwambe na kundi lake baada ya kuonyesha nia ya kugombea nafasi ya juu ndani ya CHADEMA huku akionekana kuwa na malengo na mitazano tofauti na uongozi wa sasa wa juu wa CHADEMA.
Sumaye baada ya kuonja joto la Mbowe na kundi lake mapema ameamua kukimbia haraka kabala ya kuitwa MSALITI.
Tunaambiwa Mwambe ni PANDIKIZI kwa sababu ametumwa na CCM ili kuiua CHADEMA.Yaleyale kama methali ya Wascotland inavyosema, "Give a Dog an ill name, and he'll soon be hanged’’.
Baada ya kumnyonga kisiasa Mwambe, kundi la Mbowe linawaaminisha wanachama kuwa CHADEMA inamuhitaji sana Mbowe muda huu kuliko wakati wowote kwa sababu bila Mbowe basi CHADEMA itakufa. Kwa maana nyingine, kiboko cha CCM ya sasa ni Mbowe!
Mwaka 2014 wanachama waliambiwa wamchague Mbowe kwa sababu ‘’imemla ng’ombe mzima na amebakiza mkia’’. Kwamba wamchague Mbowe kwa sababu amekifikisha chama katika hatua ya mwisho ya kuchukua dola mwaka 2015.
Mwaka huu wanachama wanaambiwa wamchague Mbowe kwa sababu ni yeye pekee anaweza kupambana na kuishinda CCM ya awamu ya Tano! Kama watamchagua mwanachama mwingine basi CHADEMA itakufa!
Dhana ya USALITI na PANDIKIZI ni silaha ambayo imekuwa ikimpa ushindi Freeman Mbowe kila baada ya miaka mitano na mwaka huu inaelekea kutoa tena ushindi!
Mbowe and his stooge are giving Mwambe a bad name and hang him! He’s finished!