Chadema na cuf nunueni majeneza na sanda...hamtufai Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema na cuf nunueni majeneza na sanda...hamtufai Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waberoya, Mar 24, 2011.

 1. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,590
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Sikio la Kufa!

  Mara mbili nimeonya kwa capacity yangu ya kuwa great thinker kuwa siasa ni mchezo mchafu , mara tatu nimesema siasa is a game and only brilliant players can do something.

  CUF japokuwa walikuwa na nguvu sana visiwani na kufanikiwa kupata walichopata lakini bado wanaDOA kubwa ambalo haliwezi kufutika kirahisi katikatia ya umma wa watanzania hasa sisi tulio na dini zote mbili na wazazi wa dini zote mbili na tuliooa na kuona katika dini hizi mbili! CCM they said CUF ni chama cha magaidi na ni chama cha kiislamu, CUF hawakujitahidi kulirekebisha hilo. Umati wao, makusanyiko yao, wingi wao na salaam zao zilidhihirisha ule usemi wa kuwa ni chama cha kidini na kinapata misaada kutoka uarabuni. Bila kufanya jitihada za kujiondoa kwenye hili zigo la kinyessi CUF waliwathibitishia watanzania kwa vitendo, mikoa waliopita kufanya kampeni na mikoa wanayokubalika ni ile ambayo imetokea kijiografia kuwa na waislamu wengi kutokana na waarabu kufikia maeneo hayo. CUF leo hii imekufa huku bara, haihitaji kipimo cha daktari kujua hilo!

  Mahasimu wangu wakubwa wa kisiasa na ambao huwa najaribu kuwafinya kisiasa CHADEMA nao wameingia kwenye mkumbo huu bila kujua au kwa kujua na kama kuzinduka hawajazinduka bado labda watafanya hivyo ikiishakuwa completely declared dead kama CUF.

  Chadema kwa uelewa wangu na ufahamu wangu wa kutoegemea pande zozote IPO kwa AJILI ya maslahi ya taifa! hakina udini wala ukabila..LAKINI kwenye siasa sivyo inavyoonekana!

  Goli ni goli hata kama ni la mkono, kwenye siasa unaweza ukashutumiwa au kuzushiwa kitu cha uongo na jamii ikakubaliana na uongo ule, hata kama utasema na kujitetea vipi, ukiisha sambaa NA KUSEMA SANA unaonekana ni ukweli!

  Tangu Slaa alipoteuliwa na chama (au Mtei) kuwa mgombea urais..INTELIJINSIA au political expert wa chadema walitakiwa wawe aware na consequences za kumteua Slaa kuwa mgombea urais, si kuwa hafai JE MAKOMBORA YA UZUSHI YANAYOTUPWA, YALIYOTUPWA NA YATAKAYOTUPWA kwake je timu ya chadema iko tayari kiasi gani kuyazima??

  Tuhuma za udini si siri zimeishaiua chadema. Nikisema hivi najua mwenye hasira wewe na yule mtahamaki.Kumbuka sentensi yangu ya kwanza, SIKO HAPA KUKUFURAHISHA WEWE MCHADEMA AU MCUF, rather nimekojua kuwaokoa na kama mkinshindwa kuyanunua manukato yangu basi hata matanga yenu hayatahudhuriwa na watu.

  Chadema iko kwenye serious undisputable allegations that;

  1. Msimamo wenu juu ya Zanzibar
  2.Mikoa ile ambayo CUF imejikita kwa sababu 'zao' nyie huko hamko kwa sababu 'zenu'
  4. Unnecessary majibizano na CUF ( refer mdahalo wa CUF na CDM kuhusu upinzani bungeni na post nyingi humu)

  All those acts made PEOPLE TO CONFIRM THAT YOU ARE CATHOLICS!!


  Huwa nasema kumpinga Waberoya humu kwa ushauri ambao naamini kabisa unatoka moyoni kwa malengo mazuri huwa HAIMFANYI MPIGA KURA KUBADILI MAWAZO..sio mimi ninae piga kura, msiwaze kwenye keyboard wazeni uko URAIANI!!

  Kumbuka:

  Wapiga kura huwa wanapiga kura na majibu ya kura ndiyo yanatangazwa ( assuming uchakachuaji haupo) Hivyo basi ni wajibu wa Chadema;

  1. Kuuaminisha umma kuwa hauko affiliated na ukatoliki au ukristo kwa ujumla
  2. Kuwa mko karibu sana na jamii ya kiislamu( hasa wale wafuata mkumbo) kwani wako waislamu smart kama walivyo wakristo smart na vice versa holds.
  3. Kuwa SWALA LA IMANI na siasa ni very worst allegations that serious techniques should be engaged to deal with
  4. Kutembelea mikoa yote ile ambayo CUF imejikita ili kuwa na sura ya kitaifa zaidi
  5. Kuwa na sura ya usawa. HILI SI KWA SABABU HAMNA USAWA BALI KUUAMINISHA UMMA AMBAO UNAPIGA KURA na ambao hawana muda hata hawaijui JF!! kuchuja pumba na mchele!
  6.Acheni majibizano ya kijinga na yasiyo na msingi na CUF, this is being taken as a confirmation that CDM ni wakristo na CUF ni waislamu


  CUF walishaambiwa sana na sikio la kufa! CUF -bara imeishakufa na CCM waliishaiua vizuri tu. CCM pia wameiua chadema kwa silaha ile ile bila huruma! na Chadema kwa matendo yao WAKIFIRIA KUWA KILA MMOJA ANA PHD ya kupambanua! This assumption is deadly!!


  Cuf and Cdm ikiwa mnalala na MNAAKA MKIWAZA JINSI GANI YA KURUSHIANA MAKOMBORA then HAMTUFAI ( CUF nimeisha-confirm siku nyingi na CDM I am confirming now)
  If CDM will not take this seriously please buy sanda and coffin, will help you to buy manukato

  KUNA WAKATI KWENYE SIASA MTALAZIMIKA KUFANYA TOFAUTI NA INAVYOTAKIWA KUFANYWA ILI TU KUWAFURAHISHA AU KUWATEKA WATU WA MAKUNDI FULANI ILI MUWAPATE, MIGAWANYIKO KAMWE HAILETI TIJA
  ISSUE YA Zanzibar CDM tuliwaambia kuwa mkiingia kama nyie mtawateka wengi sana na mnaweza kabisa kuua CUF na CCM kwa sababu mtakuwa NYIE ( mwenye akili alipambanue hili), ni sawa na vibao vya muziki! Kila mmoja anatoka kivyake na mziki unauzika!

  If at this very time some people will think this is an insult and not great thinker inputs(I am not boasting), I am sorry I was just remind you all that, when we need changes we also need challenges! If we are serious then you will easily notice that CUF and CDM are fooling us-Kutokufanya kampeni na kujitikita baadahi ya mikoa is a wasting our HOPES!

  Finally kumbukeni, kuwabadilisha malimbukeni ni kazi, wanaowazushia tuhuma za udini ni malimbukeni then please, msiwajibu kama na nyie ni malimbukeni, SIASA seems hard in chadema. Should you need any advice on what to do kindly ask so.

  Why I writing this? Tuhuma za Mufti dhidi ya chadema zimenishtua sana. They are not true at all, but what do we need to do? Refer this post!
   
 2. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Waboreyo, Nakupongeza kwa maoni yako na naamini kuwa si kama ulivyosema kuwa umeandika kwa sababu wewe huegemei upande mmoja bali ni kuwa wewe ni mmoja wa wale walioko CHADEMA ambao wameshituka kutokana na kuuona ukweli wa namna vyama vyetu vya upinzani vinavyokuwa na ubinafsi. Unasema umeshituka eti kwa kauli ya Mufti, siamini kuwa hilo limekuja kama suprise kwako lakini pengine uliunderestimate hali halisi juu ya suwala la udini kutiwa ndani ya siasa zetu. Indicators zote zilionyesha mgawanyiko na msimamo wa harakati za CHADEMA na nini tafsiri ya Waislamu.
  Waboreyo ulikuwa wapi au CHADEMA walikuwa wapi wakati CUF ilipobambikwa udini? Ni bahati mbaya sana kuwa Tanzania ukisikia udini ni Uislamu. Nashangaa kutokea mtu akasema kuwa eti CUF imekufa Bara, jee kulikuwepo hata siku moja CUF ilitiliwa maanani Bara mbali ya kuwa na nguvu sehemu nyingi zinazoishi Waislamu? Hata kule Bukoba basi ni sifa ya mtu binafsi na pale alipoamuwa kuenda kunakomstahiki basi aliwachukuwa wafuasi wake.
  Ubinafsi wa vyama vya upinzani nao haukusaidia bali ulitumika kupalilia ile mbegu ya Uislamu na pale CHAdema ilipojitafautisha na CUF tulitegemea nini iwe tafsiri yake kwa Wadini (Waislamu)? Na kwa bahati mbaya CHADEMA kwa kutaka umaarufu ukafanya yale yote yanayoonyesha utafauti na CUF, Makanisa yakajiegemeza nayo, nguvu zikawa kwenye wenye dini tofauti na Wadini, sasa mtu wa kawaida atasemaje?
  Hili la udini katika hali halisi yaani Uislamu na ukristo lipo na wala halitaondoka mpaka pale patakapokuwa na usawa na haki kwa dini zote. Si jambo la kificho kuwa kura zetu tulizopiga uchaguzi uliopita zilipigwa kwa misingi hiyo mpaka pale masilahi binafsi yalipoingilia kati. Miongoni mwa maslahi binafsi ni kuwa CCM kama chama tawala kilitowa matumaini makubwa kuliko upinzani na kwa upande mwengine Wadini waliopigia kura upande mwengine ni kuwa walikukuwa na malalamiko binafsi na CCM.
  Upigaji wetu wa kura ulifuata udini na ndio maana kura nyingi za CUF zilikwenda kwa CCM ili kunusuru Rais Muislamu dhidi ya mgomea wa Kikristo. Hili kama unaona kuwa ndio kufa kwa CUF basi natungoje. 2015 kura zetu zitabidi zijigawe kwa pande tatu CHADEMA (wakirsto) CCM (Wakirsto) na CUF (Waislamu). Pengine CCM wanaweza kutafuta mbinu mbadala lakini hili la dini halitowasaidia tena isipokuwa waende kinyume na matakwa ya Wakristo ya kuendelea kuwanyima haki Wadini.
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  daaah! Ukienda studio kuingza beat itauza! Ucwasahau hamad na lipmba waksaidie kfnya featuring. Chorus mwachie makamba aimbe. Mtauza sn!
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  CHADEMA (Wakristo) CCM (Wakristo) na CUF (Waislamu) mkuu hiyo ni 2015
  siji ndo udini kweli umefika au bado tusubili JK bwana. haya yoote madhara yako.
   
 5. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama unaitendea haki CUF kuwa wameshindwa kujitetea mbele ya umma kuwa wao si Mjahidina au wako upande wa dini fulani pale tu mikutano yao inapohudhuriwa na Umati wa Watu wanaodhaniwa kuwa ni Waislamu! au kwa sababu ya mavazi yao au lugha na salamu zinazoyumika ktk mikutano yao!

  Kama kweli wewe una share pande zote mbili za Kiislamu na Kikristo basi uwe mkweli hapa na fafanua basi ni ipi hiyo salamu ya CUF ktk mikutano yao, mavazi gani huwa wanavaa kuonyesha kuwa ni Waislamu,na kiliconishangaza ni kuwa hata kama Mikutano ya CUF inahudhuriwa na Waislamu wengi wewe ulitaka CUF wawe na utaratibu maalum wa kuchuja wote wanaohudhuria mikutano yao ili kuwa na usawa wa dini kwa Wahudhuriaji? au ulitaka wafuasi wa CUF wawe waangalifu kwa uvaaji wao wanapokuja ktk mikutano ya CUF wasiwe wanavaa vazi fulani hivi?

  Au nilini CUF waliwakataza WaTZ wengine wasihudhurie mikutano yao? au ni Mkristo gani aliyenyimwa Uanachama? Kumbukumbu zangu zinaonyesha kuwa Mwenyekiti wa kwanza na muasisi wa CUF alikuwa Mkristo Marehemu Museni Mugobi na naibu Katibu mkuu bara alikuwa Mkristo Lwakatare! achilia mbali akina Tambwe Hiza na maafisa wengine waandamizi wa ngazi za juu!

  CUF kutokubalika ktk baadhi ya mikoa ya bara sio ajabu kwa sababu hata TANU wakati ilipoanzishwa ilikubalika haraka zaidi ktk mikoa ya ukanda wa Pwani na maeneo walioishi Waislamu wengi huku bara kama Tabora, Ujiji na ktk mitaa ya mijini ktk maeneo wanaishi Waislamu wengi! mfano, hapa Moshi na Arusha Mjini, TANU ilikubalika haraka zaidi ktk Mitaa ya BONDENI wanapoishi Waislamu wengi!

  Ndio maana CUF wameona wasitumie rasilimali za Chama kuendelea kujitangaza maeneo ambayo wameona wenzao CHADEMA wamekubalika na hivyo kuamua hata kuwaachia peke yao wagombee huku wenzao Chadema wanapeleka mgombea wao maeneo kama Chake Chake!! hiki ni kichekesho! halafu wakikosa kura huko wanalalamika kuwa CUF ni chama cha kidini!

  Chadema wanasema CUF ni chama cha Waislamu kwa kutoa ushahidi wa mavazi ya Wahudhuriaji mikutano ya CUF huku wenzao CUF wakithibitisha CDM kuwa ni cha Wakristo kwa ushahidi ufuatao:
  1) Makanisa kutangaza waziwazi kuipigia kura CDM uchaguzi mkuu 2010 mfano: Kakobe
  2) Makanisa kufungwa siku ya uchaguzi! haijawahi kutokea ktk historia!
  3) Chadema kumpitisha Padri na mlei wa Kanisa kuwa mgombea Urais!
  4) Chadema kupinga waziwazi hoja ya Mahakama ya Kadhi!
  4) Inapinga TZ kujiunga na OIC!
  5) Sera yao ya kufanya maamuzi magumu kuhusu Shule za binafsi zimewashtua Waislamu!
  6) CDM inapinga bila hoja Serikali ya Umoja wa Wazanzibari na kuwatia hofu Wananchi wa visiwani ambao ni Waislamu!
  7) Ukiacha CUF vyama vyote vikuu vya upinzani vinaongozwa na Wakristo watupu na wote wanatoka mkoa mmoja wenye Wakristo wengi!Waheshimiwa MMM(Mbowe, Mbatia na Mrema)!!!!!

  Mwisho:
  Napendekeza kuwa kama CHADEMA wanataka kututhibitishia si chama cha kidini basi kiache kufanya kampeni Makanisani, kisiwapitishe Walei wa Kanisa kuwa wagombea wao, na mwisho kiache kauli za kebehi kwa Waislamu na kupinga kila chenye Maslahi na Waislamu!!!
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu kwenye hiyo nyekundu mkuu wanaosema wewe ni chama cha kiislam ni ccm na nilidhani waliyopika uliyosema hapo juu ni ccm pia kumbe ni CUF????
   
 7. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  sijamaliza kuisoma lakini nakubaliana nawe hasa kwenye sehemu za mikoa' ya pembezoni' bado nashangaa kwanini hawaendi huko kutoa uamsho hilo ni jambo jema sana kufanywa na chama 'tawala-chadema'
   
 8. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu Waberoya,

  Tofauti ya CUF na CDM ni kwamba CUF walikuwa wanashambuliwa na CCM pekee kuwa ni wadini na magaidi!!

  CHAEDEMA on the other hand wanashambuliwa na vyama vyote vingine vya upinzani pamoja na CCM (NCCR, TLP, CUF, UDP) kwa propaganda za ukabila, udini, uhaini n.k....na sasa ameongezeka Mufti!! Ni makosa makubwa kulinganisha tuhuma za udini za CHADEMA na CUF!!
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ta'adabu!
   
 10. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  -Ushindi wa kishindo wa JK 2005 uliletwa na waislamu peke yao?
  -Kwako wewe hilo neno in bold red sio kashfa??
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Samahani...........

  Wabe, una umri gani?

  Makombora wanayorushiana CUF na CDM ni yapi? ya JF au? maana ninavyofahamu mimi (sijui wengine), over my dead body, sikuwahi kumsikia kiongozi yeyote wa chadema akisema cuf ni cha kidini, wala kiongozi wa kikristo akisema cuf ni cha kidini. huu ni uwongo wa mchana ndiyo maana nimehoji umri wako.

  Wabe, nilishakueleza na nitakukumbusha tena. While you throw stones on our lovely Chadema, please provide us with an alternative party to go by. vinginevyo mawazo yako hayawezi kuungwa mkono na watanzania wanaotaka mabadiliko. kwa kuungana na ccm (tunayoipinga), cuf wamefeli. kwa uroho wa 'ulaji na ubinafsi' nccr, tlp, udp wamefeli. now where do you advice us to go? kwa kina beno malisa? ningefurahi sana kama ungekuja na ufafanuzi kwa nini umeme unawaka 24 hours tanzania wakati tunajua kulikuwa na tatizo, na hatukuambiwa limetatuliwaje. tatizo nchi hii siyo cuf wala chadema. tatizo ni ccm inayofanya mbinu za kuuwa chadema na cuf kwa kutumia mamluki kama Wabe. as for my understanding, chadema hakitakufa, rather it will stay strong, na mimi kama mwanachadema mpenda mabadiliko, huwa napatwa na hasira sana nikisoma pumba za watu kama Wabe.

  Kama msomi you should know why Tanzanians, especially illiterate Tanzanians like Mufti Simba think CCM is better. Tatizo watanzania tunakosa kitu kinachitwa deviation wakati wa kupiga kura. Am not a political scientist, lakini hii dhana imekuwa ikiwasaidia sana watu wa marekani na mataifa mengine yaliyoendelea. kwamna m-democrat anaweza kumpigia kura m-republican kwa kuwa tu m-republican anamuhakikishia mmarekani kuwa atakaposhika hatamu P.A.Y.E itapungua kulinganisha na kiwango cha wakati huo. M-democrat akiahidiwa nafuu ya maisha na M-republican, hata awe kada namna gani, hawezi kumpigia kura M-democrat eti kwa kuwa ni mtu wa chama chake. huu ndiyo ugonjwa unatutafuna watanzania, hasa wasio na elimu dunia kama mufti wenu. Kwa hisia Wabe, umekwenda shule, lakini namna unavyoleta hoja za mchiriku hapa jamvini nachelea kusema, kichwani kwako umejaa madesa. cuf na chadema na jamii za watu. usituletee mada za kichonganishi hapa. tumia elimu yako kuelimisha watanzania namna na kuchagua viongozi. usijisahau sana kuwa uko Dar unakula nchi, kuna mamilioni ya Watanzania kijijini wasiojua haki na wajibu wao kwa sababu ya CCM hii hii. natamani kulia, lakini...............
   
 12. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Waberoya, umesomeka mkuu. Mapendekezo yako tutayafanyia kazi.
   
 13. i

  itahwa Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  atakayepinga haya uliyoongea atakuwa na utindio wa ubongo
   
 14. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  another kashaga in the JF habari ndeeeeeeeeeefuuuu lakini aina mantiki yeyote kama udini ukabila kaubirie kwenu hapa tz akuna hivyo vitu ulishapita mtaani ukasikia story za udini au ukabila? kama ni propaganda mmeiandaa kuipromote basi mmefeli tafuteni nyingine.
   
 15. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Waberoya uliyosema yana ukweli mkubwa japo kuna wengi humu jamvini hawatataka kuyasikia. ila kwa ambao hawana vyama wala ushabiki wa upande fulani hili jambo linafikirika. kwa tulioichoka ccm si wanachama wa chama chochote kabla ya kura nitaangalia mbadala mwenye uelekeo ninaouota. sasa haya mambo ya udini yamezidi, mimi ni mkristo lakini 2005 niligonga glass baada ya JK kuwashinda wenzake ndani ya ccm nikamini ndie rais tayari. lakin 2010 nilikuwa nikimsikia malaria inapanda. sasa kama misingi ya kuchagua tunaangalia mlei au ustaadh sijui inakuwaje, tuko wakristo na waislam kwa wingi zaidi na uwezekano mkubwa lazima raisi awe mlei au ustaadh sioni shida ila mwelekeo ushapotea kimtizamo kwa wengi inavyoelekea.

  vyama viwe na sura na ku-act kitaifa zaidi na kuepukana na propaganda za ccm za udini kwa cdm na cuf. kama wakisema ila nyie kazi zenu na mwelekeo wenu ni wa kitaifa sisi si tuna ubongo wa kufikiri na macho ya kuona, ila mkikaa kitata lazima tujiulize. hatutaki ushabiki tunataka TZ au Tanganyika moja tu na yenye maisha bora ya ukweli sio ya .....
   
 16. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  hsayo majeneza na sanda jinunulie mwenyewe kwa sababu kazima uzikwe wewe kwanza kabla ya chadma
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  VYAMA VYA CUF NA CHADEMA VYOTE VINATUFAA WANANCHI TENA SANA KULIKO
  CCM ENDAPO VITAWEKA MASLAHI YA UMMA MBELE KWA PAMOJA


  Nasema ni mara mia CUF na CHADEMA kuliko CCM-Ufisadi kwetu nchini Tanzania.

  CUF na CHADEMA ni vyama vya siasa ambavyo VINATUFAA SANA nchini na Wa-Tanzania tunasema viendelee kwepo kwenye ramani yetu isipokua Prof Lipumba na Juliasi Mtatiro fanyeni hima kujiondoa katika ndoano ya Muafaka na CCM linaloendelea kukidhoofisha sana wengine tuonao mbali na siasa za nchi hii ambavyo tusivyopenda kuona ikiendelea.

  Naamini kama si Maalim Seif Sharif Hamad kukamatishwa hili Janga la Muafaka uliosadia tu kuleta UTULIVU huku HAKI na AMANI ya kudumu ukiwa unaendelea kudai zaidi Zanzibar, naamini tena sana tu kwamba KUNA VICHWA SANA TU NDANI YA CUF kama vile Prof Lipumba mwenyewe hakika wasingekubali njia hii yenye mafanikio ya muda mfupi nchini na madhara makubwa kuliko kwa CUF katika kipindi kirefu siku za sasa na za uso.

  Ndio, naongeza kwamba hata aliyekua mwanachama Prof Safari, Katibu Mkuu Msaidi Juliasi Mtatiro, Mwanasiasa Machachari nchini Duni Haji Duni na Umoja wa Vijana CUF, Baraza la akinamama CUF ambao kwa pamoja laiti wangeshirikishwa moja kwa moja tena kwa KILA HATUA YA MAZUNGUMZO YA MUAFAKA KATI YA WAHESHIMIWA Maalim Seif Shariff Hamad na Yusuff Makamba, na wakatafakari uzuri mchakato mzima basi napata jibu la wazi kwamba katu wasingelikubali hatua hii ya zimamoto isipokua wangeungana na Wa-Tanzania wenzao wengine kudai kwa nguvu zaidi kuundwa kwa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi Bara na Visiwani ikiwa ni suluhisho la kudumu sana tu nchini kwetu.

  Hata hivyo, kwangu mimi najua fika kwamba kule kupotea njia ndio kujua mji hivyo wala siwalaumu wenzetu CUF hadi hapo isipokua nawahimiza wafanye hima kuchagua kati ya kupanga mstaari wao nyoofu kisiasa kwa kushirikiana na CHADEMA katika safu ya ukweli na ukweli mtupu huku vyama vyote vikiweka Maslahi ya Taifa Mbeleele kama tai au waendelee kula Good Time na CCM ili wapate kuanguka wote tena kwa kishindo!!
   
 18. only83

  only83 JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Udini wa nini hapa? Tumesema kila kukicha tupeni evidence ya udini na ukabila na huyo mtu anayefanya hayo achukuliwe hatua stahiki....tutabwabwaja kila siku bila kuchukua hatua.................
   
 19. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hii ni habari ya kipuuzi zaidi sijawai kuona.

  Siku zote mtu anaandika kilicho mjaa kichwani mwake, ukiona mtu anaandika habari za Udini ujue yeye ndio mdini zaidi kuliko mtu yeyote yule.

  Kama CCM mnadhani sera ya Udini itawasaidia dhidi ya CDM basi mjue ndiyo itawamaliza barabara, maana hata hao CCM members mliobaki nao watajiuliza kwanini waendelee kubaki huko wakati kila siku kila kukicha mpo Misikitini.

  Moi alipojenga siasa za Ukabila Kenya, alijua itamsaidia kujiimarisha, lakini ndiyo iliyouwa KANU nakuizika kabisa, endeleni na hizo kampeni zenu zenu za kipuuzi ila mjue CCM haitapo katika kapu la Udini ndio itasaulika milele. Hii akili ya Kikwete kama ya Iddi Amini na za Qadhafi zinafanana na Waberoya umepotea kabisa.
   
 20. J

  Joblube JF-Expert Member

  #20
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sitajadili udini huu ni upuzi kabisa na ni dalili ya kufilisika kimamawazo.
   
Loading...