Uchaguzi 2020 CHADEMA na CHAUMA, Hashimu Rungwe ni kiongozi mwenye maono na hekima atawavusha

OTTER

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
476
331
Katika watia nia wa kugombea urais na walioteuliwana kwa ajili ya kupeperusha bendera za vyama vyao, kwa vyama vilivyo vya dhati vya kuwa na upinzani mkuu katika uchaguzi wa mwaka huu, Chama cha CHAUMA, kupitia mgombea wake Mhe. H. Rungwe, ukimsikiliza vizuri anapopita huku mikoani kwetu kutafuta wadhamini anaongea kwa unyenyekevu wa hali ya juu kiasi kwamba kila mtanzania anayepata fursa ya kumsikiliza anahamasika kumdhamini.

Ni kiongozi mwenye maono makubwa, mnyenyekevu na ana ahidi kusimamia na kuendeleza yale yote yanalifanywa na watangulizi wake na kuongezea maendeleo zaidi ya haya waliofanya wenzake, anadai hii ni awamu ya tatu anaomba nafasi hii ya pekee ya urais na wananchi kwa pamoja wamechukua sera zake wameahidi kuzifanyia kazi

Mhe. Mwenyekiti, kama ilivyodesturi ya Chama na miiko yake, tafadhali angalia upepo unasomaje, badili gia angani muunge mkono Mh. Rungwe wa CHAUMA, kwani huyu ni YEYE atakaye weza kukinusulu chama chenu iwapo mkimtumia vizuri kuuza sera zake na za CHADEMA, maana wananchi wanamuelewa.

Muondoeni huyu aliyepo kwa sasa kabla ya DEGE halijatua kwenye uwanja wa mapambano na kusababisha msambaratishwe msije mkakosa wawakili wa kurudi mjengoni. Sera zake ni kutuna watu na kuwadhalilisha hovyo huku mikoani, hana jipya. Atachuja hata kabla ya kampeni. Mumtue mzee Rungwe atawanusuru kwenye hiyo SUMANI ya kusomba majimbo yote, angalu munusuru hata majimbo mawili tu ili mkasimuliane. Mjumbe hauawi.
 
Sawa Mwana CCM mwenye mapenzi mema na CHADEMA,ila sidhani kama ni sahihi kuwauzia mbinu wapinzani wako juu ya kuchukua majimbo,ni busara kama ungenyamaza tu ili CHADEMA isipate hata hayo majimbo mawili uliyoainisha.
 
Kinachounganisha vyama ni Sera na Itikadi.
Pia gain/ loose analysis...inatumika.

Kuungana huwa ni sayansi...hata kwa individuals kuungana kushafelisha wengi.

Hadi ikapelekea watu wengi sasa kuamua kuungana na wake zao tu sababu wanaruka na mbawa moja.

Kwenye biashara unaweza kuita T/ L analysis!! ( Traiding and loss analysis) kwenye sayansi ama economics wanaita Risk analysis kwenye major ya Risk Management.

Kwa mfano yeye Mzee Hashimu na chama chake na Sera ya ubwabwa kwa madenti wrote nchini...Je CDM wanayo sera hii? Kama hawana wakiungana basi ni lazima sera hii iwemo kwenye ilani ya pamoja wakati wa kuomba ridhaa kwa wananchi kuliongoza taifa...
Na kama Hashim akukubali isiwepo basi ndiyo loss yenyewe hiyo!!

Umeona ugumu ulipo.
 
Back
Top Bottom