CHADEMA na CCM, Watu wangapi wamekufa katika harakati zenu za siasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA na CCM, Watu wangapi wamekufa katika harakati zenu za siasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alexism, Aug 28, 2012.

 1. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Kama mtanzania mwenye upendo na mzalendo wa nchi na watu wake ningependa kujua idadi ya wananchi ambao wamekufa kwa kuuwawa na polisi wakati harakati za kisiasa baina ya CHADEMA na CCM.

  Swala ili ni muhimu tukalijua ili tuweza kufaham nani wakulaumiwa na nani anabidi awajibishwe katika mauaji ya watanzania wasio na hatia. Kama utakuwepo uwezekano kabisa na ninao uhakika upo wakuwajibisha watu waliousika moja kwamoja.

  Naomba wahusika kama polisi au vyama tajwa watoe taarifa kwa umma hasa kwakutumia mtandao huu ili umma uweze kujua na kufanya mahamzi dhidi ya vitendo hivi vinavyo endelea kila kukicha.
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Unachanganya mambo, Muuaji anajulikana, Bwana mipango wa mauaji anajulikana. Tuna TISS na Polisi hao ndi wa kuwauliza kama kazi yao wanaifahamu sawasawa.
   
 3. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  Heading yako umekosea andika CCM kwa kushirikiana na Polisi Mmeua wana CDM wangapi katika harakati zao za kisiasa?
  Kwani katika matukio yote ya mauaji na ukandamizaji juu ya Demokrasia hakuna sehemu ambayo wana CCM walivamiwa na polisi isipokuwa ni kwa CDM tu.
   
 4. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  Hili swali ungeuliza Polisi,kuna kila dalili za Polisi kuvuruga utulivu wetu kwa mabavu yasiyo na msingi.Kuna uelekeo wa kuishiwa uvumilivu nchi ilipuke.fanyeni mizaha na hali halisi ukiwaka umewaka kweli kweli,waoneni Wananchi ni wajinga tu!
   
 5. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Cha msingi si kutafuta wa kulaumiwa, bali Tutafute jinsi ya kuzuia mauaji zaidi yasitokee. Mimi naamini 100%, chama changu hakiwezi kutuma chombo chochote cha dola kuua. Mauaji hutokea pasipo dhamira ya chama chochote, isipokuwa tuombe vyombo vya dola, visiingilie uhuru na haki za vyama kufanya kazi zao za kuhamasisha jamii. Naamini mauaji ni mbinu chafu za baadhi ya watendaji wanao simamia vyombo vya dola, katika kumharibia Mkuu wangu wa kaya asipate nishani ya Mo Ibrahimu, ambayo kiukweli alistahili.
   
 6. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa ana list yote na malengo yake mpaka jinsi nchi itakavoingia katika machafuko.
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Waulize CDM kwa uchu wao wa madaraka wamepanga kuua watu wangapi mpaka kufanikiwa watakacho? kwenye bendera wameweka hata rangi yao nyekundu kuwa sera yao ni kumwaga damu na kutofuata utawala wa sheria. CDM ni janga la kitaifa na dunia

   
 8. a

  adolay JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280

  Unarukaruka kila hoja, jibu hoza unazoziacha nyuma kwa kila hoja unayoitibulia na kuichafua na kurukia nyingine.


  Kuwa mungwana.
   
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Haya ww ni kada kufa wa cdm, rangi nyekundu ina maana gani ? tujuze hapa jamvini

   
 10. a

  adolay JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280

  Mimi nitaanza kukuuliza maswali uliyotakiwa utupatie majibu kwenye hoja ulizorukaruka, nitakuuliza hapa kwa sababu amejitokeza hapa, japo haiendani na hoja tuliyonayo. Nakuomba tu tuendeleze huu mdahalo kwa maana ya uelewa, weka papara pembeni na chambua haya mambo kama great thinker no magumashi tunapodebeti.


  1. Kunahoja ulisema kifo cha kujitakia, hebu tueleze ulikuwa unamanisha nini, na nani alijitakia kifo hadi akajiuwa?


  2. Kwenye hoja ilele ukasema, alie uwa anapaswa kuuwawa kwa majibu wako na kwamba ndivyo mungu anavotaka. nikasema kwa mujibu wa sheria za mwanadamu za kimahakama mtu anahukumiwa kunyongwa ikithibitika pasipo kuacha shaka.

  Maswali yangu yalikuwa hivi.

  i) Mungu anaruhusu mwanadamu kuhukumu kwaniaba yake? kivipi na kwa nini?

  ii) Kama ndivyo i) hapo juu, je mungu hanauwezo hata mwanadamu amsaidie kuhukumu? na kama ndivyo elezea udhaifu wa mungu kukosa uwezo uko wapi hata asaidiwe kuhukumu?

  iii) Siku ya kiama ipo? na jehanamu ipo?
  -kama jibu ni ndio, je hukumu atakayotoa mungu (Allah) siku hiyo inauhusiano wowote na hukum ulioisema kwamba alieua kwa makusudi yampasa kuuwawa kwa amri ya mwanadamu?  RANGI NYEKUNDU.

  Mara nyingi rangi nyekundu huchukuliwa kama inshara ya hari ya hatari, lakini pia wapendanao huitumia rangi hiyo kwa maana ya upendo na haishii hapo itategemeana piwa na maamuzi ya mtumiaji. (mimi naelewa hivyo sijuwi wewe unaelewaje?)

  Matumizi ya rangi hii ni lazima yawe sahihi, kwa maana ya haki na kukubaliwa na wahusika wa pande mbili (kama ni kwa maana ya hatari, au upendo au maana nyingine yeyote)

  Tofauti na matumizi ya haki, hata mbwa unaemfuga na kumlisha kila siku usipomtendea haki na kumkandamiza ukamuumiza atakung'ata na anaweza kukuuwa. Hivyo, heshima ya utu na thamani kwa maana ya sheria kutoka katiba mama lazima kuzingatiwa ilikupata matokeo sahihi kwa watawala.

  Usitegemee kupanda umaskini, chuki na udharirishaji miongoni mwa raia wako ukitegemea kuvuna, utulivu, amani na upendo.
   
 11. N

  Ngoshanzagamba Member

  #11
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilitaka nikukumbushe pia mauaji ya CCM na CUF kule Zenji 95/96 had watu wakaenda uhamishoni SHIMONI na wamerudi juzi tu...na baaada ya hapo sasa tuongee ili uone nani muuaji wa wananchi....

   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,699
  Likes Received: 12,750
  Trophy Points: 280
  Nenda RITA
   
 13. E

  EMMANUEL NSAMBI JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hata Red Cross kazi yao ni kumwaga damu?
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Kama Wewe Sio Mnafiki unge-kuwa based kwa CHADEMA tu; kama kweli Unapenda haki na ni free haupendelei Upande wowote

  Ungebadilisha Tittle na kuuliza CHADEMA wamepoteza watu wangapi kwa NGUVU za CCM? CCM inatumia NGUVU za POLISI na

  SHERIA kukandamiza USAWA na haki za kisheria...

  Sasa, Umeona Mkutano wowote wa Nnape Nnauye Umeingiliwa na FFU? hata siku Moja? Wewe hata Mkutano wa USA - DMV

  Bado CCM wanasema CHADEMA wanahonga wana CCM; Unaona hakuna HAKI na USAWA.... PLEASE BE FAIR...

  "
  Emancipate yourselves from mental slavery, none but ourselves can free our minds!"

   
 15. K

  Kigano JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 349
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh, UMEPAONA VIZURI SANA ndugu yangu ! nilitaka kuuliza hivyo hivyo, maana nao wana alama nyekundu !
   
 16. a

  adolay JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280

  Mkuu Emmanuel

  Ndo hapa napata tabu kwa huyu mwenzentu geniusbrain, uwezo wa uelewa na kutafakali tunatofautiana sana.


  Bahati mbaya zaid hajibu hoja isipokuwa anarukaruka tu.
   
 17. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkuu, hapo kwenye red mwanzoni ni mwendelezo wa propaganda chafu na za kijinga za kujaribu kumtenganisha Mkulu na maovu, uchafu na udhaifu wa watendaji wake zinazoenezwa na ccm wakidhani wanamsaidia kumbe ndio wanadhihirisha udhaifu wake kiutendaji. Na bahati mbaya ni kwamba zimegeuka kuwa wimbo usiotamanisha kuusikia tena!

  Red ya chini ni upuuzi kabisa kufikiria hilo maana wanaotoa zawadi hawaangalii rais aliyefanya safari nyingi za nje bali yule aliye mbunifu na kwa ubunifu wake ameliletea taifa lake demokrasia ya kweli na maendeleo katika nyanja za kielimu, kisiasa, kiuchumi, kiuongozi, kiufundi na kijamii. Mambo ambayo jamaa'ako ameshindwa kabisa!
   
 18. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red, Mkulu amepungukiwa lipi????? Tuache siasa, tuhukumu watu kwa haki. najua yapo ambayo yamekuwa kasoro kwake. mfano swala la mabwepande limemchafua sana, swala la kufungia gazeti la mwana halisi ni kasolo kubwa, mauaji ya Arusha, mauaji ya jana, morogoro - hayo ni baadhi ya mambo ambayo yamemchafua, ingawa naamini ni upotofu wa vyombo vilivyo chini yake, na vimetenda bila kumhusisha. Toa maoni kiukomavu, na sio kwa wingi wa matusi na kashfa, haisaidii.
   
Loading...