CHADEMA na CCM wana madiwani wangapi Arusha?

mhalisi

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
1,181
320
wadau wa JF, naomba kuuliza Chadema na CCM kila kimoja kina idadi ya madiwani wangapi ktk halmashauri ya jiji la Arusha? nauliza hivi pia kwasababu inasemekana CCM inahofu Chadema ikishinda viti vinne vya udiwani ktk uchaguzi wa jumapili watapoteza kiti cha umeya wa halmashauri ya jiji la Arusha.
 
Habari ndiyo hiyo wakipigwa chini viti vinne meya wa kuchonga hana kitu
 
Kama sikosei Chadema ilikuwa na madiwani 10 na CCM 15 hivi. TLP ilikuwa na Diwani mmoja au wawili sina hakika vizuri Sasa baada ya Baadhi ya madiwani wa Chadema Kusimamishwa wakabaki wana 6 kwa hiyo kama Chadema Ikishinda viti vyote vya udiwani itakuwa na Madiwani 10 + Viti maalumu watakuwa 11 wakati CCM wana 15 + Maalumu 16 tofauti ya madiwani 5- 1 TLP = madiwani 4. Ili kuweza kumpata meya theluthi mbili ya madiwani lazima impigie kura.....au ili kuchagua meya lazima kikao cha madiwani kiwe na theluthi mbili ya madiwani wote sasa pamoja na wingi wa madiwani wa ccm. Ni kwamba ili kumchagua meya lazima theluthi mbili ipige kura kumkubali ndio maana MEYA aliyepo alichaguliwa baada ya zengwe kufanyika kwa kuwahadaa chadema kiasi cha chadema kuchelewa kwenye kikao cha uchaguzi nao wakampitisha haraka haraka......( Meya wa Kichina!)
 
Sasa hivi Ccm ina madiwani 11, Chadema ina madiwani 7, Chadema wakipata madiwani wote 4 itakuwa na madiwani 11 sawa na ccm halafu watapata diwani mmoja wa viti maalum, pia kwa mujibu wa sheria wabunge wa jimbo ni madiwani kwa mujibu ya nafasi zao, Chadema ina madiwani 3 jimbo la Arusha mjini, mahesabu yanakupa madiwani 15. Hata wasipofanya uchaguzi wa Meya ni budget gani ya ndioooo itapita? Je huyo meya atamuongoza nani? Kuna kupata ushirikiano hapo kweli?
 
hali hii inaonyesha CCM wapo ktk wakati mgumu.
 
Kama sikosei Chadema ilikuwa na madiwani 10 na CCM 15 hivi. TLP ilikuwa na Diwani mmoja au wawili sina hakika vizuri Sasa baada ya Baadhi ya madiwani wa Chadema Kusimamishwa wakabaki wana 6 kwa hiyo kama Chadema Ikishinda viti vyote vya udiwani itakuwa na Madiwani 10 + Viti maalumu watakuwa 11 wakati CCM wana 15 + Maalumu 16 tofauti ya madiwani 5- 1 TLP = madiwani 4. Ili kuweza kumpata meya theluthi mbili ya madiwani lazima impigie kura.....au ili kuchagua meya lazima kikao cha madiwani kiwe na theluthi mbili ya madiwani wote sasa pamoja na wingi wa madiwani wa ccm. Ni kwamba ili kumchagua meya lazima theluthi mbili ipige kura kumkubali ndio maana MEYA aliyepo alichaguliwa baada ya zengwe kufanyika kwa kuwahadaa chadema kiasi cha chadema kuchelewa kwenye kikao cha uchaguzi nao wakampitisha haraka haraka......( Meya wa Kichina!)

Katika 11 toa mmoja Alphonse Mawazo diwan wa Sombetini aliyehamia CDM
 
Madiwani wa ccm wapo 11 chadema wapo 7.
Ila chadema wakichukua kata zote wanarudishiwa diwani moja wa viti maalum jumla wanakuwa 12.
 
mkuu, kwa hali iliyopo CCM inaweza kushinda ata kata moja?
 
Back
Top Bottom