Chadema na ccm wakatana mapanga mkoani iringa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,110
[h=3][/h]



MWENYEKITI wa Baraza la Wazee wilayani Kilolo, Lunyiliko Nyaulingo amelazwa katika Hospitali ya mkoa Iringa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mgololo amelazwa Hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wanaodaiwa ni wanachama wa CCM katika kampeni za mwisho za kuwania nafasi ya udiwani.


Sambamba na hiyo Katibu wa CCM kata ya Ng’ang’ange wilayani Kilolo, Wilhad Ngogo (40) na Yohana Mchafu anayedaiwa kuwa ni mwanachama wa CCM wanashikiliwa na Polisi kwa kuhusika na matukio hayo.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema watu hao walikamatwa jana kufuatia
vurugu zilizojitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya mwisho katika wilaya hizo mbili.


Alisema kufuatia mzozo huo wanachama wa CHADEMA walizuia barabara ya Iringa-Mbeya kwa kuweka magogo ili kuzuia magari kupita na kuwa Polisi wanamtafuta Rabart Sam maarufu kwa jina la Kideri kwa kuongoza vurugu hizo.


Kamanda Mungi alisema wanafanya uchunguzi wa kina juu ya matukio hayo na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.


Aidha alitoa wito kwa viongozi wote wa vyama vya siasa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ili kuepusha vurugu ambazo zinaweza kutokea.


Leo Uchaguzi wa udiwani katika kata ya Ng’ang’ange wilayani Kilolo na Mbalamaziwa wilayani Mufindi ulifanyika ambapo Zuberi Nyomolelo (CCM) na Ezekiel Mlyuka (CHADEME) walipambana kwa kata ya Mbalamaziwa na kwa upande wa Ng’ang’ange Kilolo Nafred Chahe (CHADEMA) na Namgalesi Msuva (CCM) walipambana



chanzo. CHADEMA NA CCM WAKATANA MAPANGA MKOANI IRINGA - MPEKUZI HURU
 
hv kwa nn ccm wanafanya haya mambo ya kijinga? Hv unajua chadema wakiwa wana jihami kwa kutembea na visu na bastola unajua itakuwa noma sana
 
CCM ni wauwaji tukubali tu kwani hata huruma hawana kabisa. Lile jeshi wanalandalia huko Mbeya si litamaliza watanzania wakati wa uchaguzi mkuu? Mungu tuondolee hawa wadhalimu.
 
Chinjanen, uwanen, mfe na mpotee kabisa katika uso wa dunia, kwan mna faida gan kwetu? haya mambo ya vyama ni mambo ya kijinga kabisa. Natamani jeshi lishike hatamu then lipige marufuku vyama vyote kuliko kuona ujinga unaendelea
 
Back
Top Bottom