Chadema na CCM wachapana Rukwa!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema na CCM wachapana Rukwa!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by minda, Oct 8, 2010.

 1. minda

  minda JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Chadema na CCM wachapana Rukwa
  Na Muhibu Said

  8th October 2010  Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu zinazoendelea nchini kote, jana ziliingia katika sura mpya, baada ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Mpanda Mjini, mkoani Rukwa, kupambana.


  Jimbo hilo linawaniwa kuwakilishwa bungeni na Said Arfi (Chadema) na Sebastian Kapufi (CCM).
  Mapambano hayo ambayo yalizuka saa 8.30 mchana muda mfupi kabla ya mgombea urais kupitia Chadema, Dk. Willibrod Slaa, kuhutubia mkutano wa kampeni, yalisababisha mfuasi mmoja mwanamke wa CCM, ambaye jina lake halikufahamika mara moja, kuzirai.

  Mapambano hayo yalizuka baada ya wafuasi wa CCM waliovalia sare wakiwa kwenye maandamano ya magari zaidi ya 15 ya teksi, yakipeperusha bendera za chama hicho, kupita karibu na eneo ziliko ofisi za Chadema wilayani hapa na kuanza kuzomea, huku wakipiga honi za magari.

  Kitendo hicho kilifanywa na wanaCCM hao dakika chache baada ya wafuasi wa Chadema kusitisha maandamano yao kwa muda katika ofisi hizo zilizoko karibu na Mahakama ya Wilaya ya Mpanda.
  Maandamano ya wafuasi wa Chadema waliovalia mavazi rasmi ya chama, pamoja na kubeba bendera za chama na mabango yenye ujumbe tofauti, yalianza saa 4.00 asubuhi kwa kuzunguka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya mji wa Mpanda, huku yakitumia usafiri wa pikipiki na baiskeli.

  Mara baada ya kufika karibu na ofisi za Chadema, wafuasi wa chama hicho waliokuwa wamekusanyika nje ya ofisi hizo ‘walijibu mapigo’ na kuanza kuwazomea kwa nguvu wafuasi hao wa CCM.

  Mbali ya kuzomea, wafuasi hao wa Chadema, wengi wao wakiwa vijana walioonekana kuwa na hasira, waliyavamia magari hayo na kuyazuia kupita katika eneo hilo kwa madai kwamba yalilenga kuleta uchokozi dhidi yao ili kuvuruga amani.

  Hatua hiyo ilizua hofu kubwa kwa baadhi ya madereva wa magari hayo, ambao waliyaondoa haraka katika eneo hilo ili kuepusha kuharibiwa.

  Hata hivyo, baadhi ya wafuasi wa CCM waliokuwa kwenye magari yaliyokuwa yangali nyuma kwenye msururu wa maandamano hayo, walipoona wenzao mbele wamezuiwa kupita, walishuka na kuwafuata wafuasi wa Chadema na kisha kuanza kurushiana maneno makali.

  Wafuasi hao wa CCM walidai kuwa hawakupaswa kuzuiwa kupita eneo hilo, kwa madai kwamba wana haki ya kutumia barabara hiyo kwa vile nao ni sehemu ya walipakodi.

  Mzozo huo ulidumu kwa dakika kadhaa, huku wafuasi wa Chadema wakiwa wamefunga barabara hiyo wakizuia wafuasi wa CCM kupita eneo hilo.

  Baadaye mzozo huo ulitulia baada ya baadhi ya viongozi wa Chadema kuingilia kati na kuudhibiti na magari ya wafuasi hao wa CCM yaliendelea kupita eneo hilo.

  Baada ya gari la mwisho kupita, wafuasi wa Chadema waliweka ulinzi katika eneo hilo.
  Wakati wakiendelea na ulinzi, dakika chache baadaye, alipita katika eneo hilo mfuasi huyo mwanamke wa CCM akiwa kwenye baiskeli huku akiwa amevaa kofia ya chama hicho.
  Wafuasi wa Chadema waliokuwa katika eneo hilo, walimvamia na kumshusha kwenye baikeli aliyokuwa amepanda na kisha wakamvua kofia hiyo.

  Mfuasi huyo wa CCM hakukubaliana na kitendo hicho, alianza kujibu mapigo kwa kuanza kuwarushia ngumi vijana wa Chadema waliomshusha kwenye baiskeli na kumvua kofia aliyokuwa amevaa.
  Vijana hao wa Chadema, walijibu ngumi hizo na mwanaCCM huyo alizidiwa nguvu na kuanguka chini na kuzirai.

  Hali hiyo ilizua mtafaruku mkubwa na baadhi ya wafuasi wa Chadema walianza kumpepea mwanaCCM huyo wakati akiwa amelala chini na kisha kumbeba na kumuondoa katika eneo hilo.
  Wakati wakimbeba, mwanaCCM huyo alipata ahueni na kuanza kupaza sauti kwa kupiga kelele mithili ya mtu aliyeapandwa na mashetani.

  Askari polisi wakiwamo waliovalia sare, kiraia na wale wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa kwenye gari la polisi aina ya Toyota namba PT 18 37, waliobeba mabomu ya machozi na silaha za moto, walifika katika eneo hilo wakati huo hali ikiwa imetulia.

  Katibu wa Chadema Jimbo la Mpanda Mjini, Joseph Mona, alisema walijua mapema kwamba, vurugu hizo zingetokea na kwamba, walitoa taarifa hizo kwa Ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) ya Mpanda.
  “Nilimwambia OCD kuwa CCM wamepanga kuzuia tusitumie teksi na watakuwa na maandamano kwa lengo la kutuharibia mkutano wetu wa mgombea urais. OCD aliahidi atawaona viongozi wa CCM, lakini tunashangaa tumeona teksi zikiwa na bendera kwenye ofisi zetu, ambako ni jirani na uwanja wa mkutano wetu,” alisema Mona.

  NIPASHE iliwatafuta viongozi wa CCM Wilaya ya Mpanda kuelezea suala hilo, hawakuwepo ofisini na kuambiwa kuwa pamoja na Katibu wa Wilaya, Jacob Nkomola, walikuwa maeneo ya vijijini.
  Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Dk. Rajabu Lutengwa, alisema hawezi kulizungumzia hadi hapo atakapopata taarifa kutoka vyombo vya dola.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage, alisema hajapata taarifa za tukio hilo na kuahidi kwamba, atalifuatilia.

  Hata hivyo, alisema wamejipanga vyema kumpokea Dk. Willibrod Slaa na kuimarisha ulinzi.
  Akizungumzia tukio hilo, Dk. Slaa alisema kama amani itapotea Tanzania, polisi watakuwa washitakiwa namba mbili baada ya CCM na kwamba watastahili kufikisha katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

  chanzo: nipashe

  nb:
  sakata hili pia lilikaririwa na tbc1 kwenye kipindi cha habari cha saa 2 usiku

  naomba kuwasilisha!!!
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Shimbo anasemaje kuhusu jambo hili? Kwanza nasikia eti ndio kaanza mazoezi ya 31 Okt 2010, kama hajui siku hiyo misuli itakuwa inamuuma! Hawa wa CCM sio Green Guard?
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,254
  Trophy Points: 280
  Vurugu zote ni JK na CCM ndiyo wanasababisha na ICC wako macho kumtia mikononi JK mara uchaguzi ukiisha kwa vurugu za umwagaji damu.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  WanaCCM hao walikipata walichokuwa wanakitafuta!
  Huo ni uchokozi dhahiri...Ni kweli wanalipia kodi mabarabara, lakini isiwe sababu ya kuwafuata wenzenu hadi wanapofanyia mkutano na kuwavuruga!
   
 5. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tamaa ya madaraka hii bila kufanyia kazi wananchi watamaliza vibaya maisha yao.
   
 6. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  hhahaaah....!
  niliona kwenye tbccm wakati hako kabinti ka sisiem kakichakachuliwa kwa makonde..! kweli unapita kwa mkutano wa chadema na kofia ya thithiem unategemea nn...?
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu zinazoendelea nchini kote, jana ziliingia katika sura mpya, baada ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Mpanda Mjini, mkoani Rukwa, kupambana.

  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...