Chadema na Bajeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema na Bajeti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by V.P, May 26, 2011.

 1. V

  V.P Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wengi wetu tumechoka kuburuzwa na CCM na kila siku hali ya maisha inazidi kuwa ngumu bila ya matumaini yoyote. Kwa bahati mbaya kura za 2010 hazikutosha kutuwezesha kuleta mabadiliko ya uongozi na kujenga mahusiano mapya kati ya Serikali na Wananchi.

  Sina imani kwamba hali ya maisha itabadilika chini ya chama cha magamba kwa sababu kufanya yaleyale na kutegemea matokeo tofauti ni uwendawazimu.Ni matumaini yangu kwamba Chadema itakabidhiwa dhamana ya kuongoza dola mwaka 2015 Inshallah ili tufungue kurasa mpya.

  Lakini hatutaki mabadiliko ya uongozi ili mradi tuwe na chama tofauti. Tunataka tuwe na chama ambacho kwa kweli kina uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli na kina wajibika kwa wananchi.

  Ni muhimu Chadema ikaimarisha utamaduni wa kuwajibika na kujiwajibisha kabla hata hakijaingia madarakani ili kikiingia madarakani tayari tuwe na utamaduni huo kwa maslahi ya wananchi.

  Kwa mantiki hiyo basi napenda kuhoji machache juu ya utendaji wa Chadema katika kulinda maslahi ya wananchi.

  Hivi karibuni tumesikia kwamba ofisi ya Waziri Mkuu ilinunua gari lenye thamani ya zaidi Tsh280m ambalo halikuhitajika kama Waziri Mkuu mwenyewe alivyokiri. Fedha hizo za walipa kodi zingeweza kusaidia matatizo yetu mengi.. Pia shirika la ndege la ATCL limepewa ruzuku na mabilioni ya fedha za walipa kodi bila ya matumaini yoyote ya kufufuka, uhalali wa zile fedha za ruzuku hatuufahamu. Leo shirika lina wafanyakazi 200 na hakuna hata ndege moja inayofanya kazi. Hii ni sawa na kudharau walipa kodi.

  Maswali kwa viongozi wa Chadema.

  1-Je, fedha zote hizi ziliidhinishwa ndani bajeti?

  2-Kama ni ndio kwa nini muliidhinisha matumizi ya gari lisilohitajiwa na uhalali wa ruzuku za mabilioni kwa shirika la ATCL ni upi wakati wengi wetu tunawaunga mkono kwa hoja ya vita dhidi ya ufisadi?

  3-Kama hamukubariki malipo hayo mumechukua hatua zipi dhidi ya malipo yasioidhinishwa na Bunge?

  4-Kuna udhaifu gani katika utaratibu wa kupitia na kupitisha bajeti ya taifa, Chadema imefanya nini kurekebisha udhaifu huo?

  5- Mkaguzi na Mhasibu Mkuu amekuwa kifanya kazi nzuri ya kuandaa ripoti za kitaalamu amabazo zinahusisha ubadhilifu wa fedha za umma, Chadema imechukua hatua gani kuhakikisha wahusika wanawajibishwa?
   
 2. Mbutunanga

  Mbutunanga Senior Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 183
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sijajua kwa nini umeyaelekeza haya maswali kwa chadema na wala si CCM, maana hata hao wabunge wa chadema wakikataa hizo bajeti na kuhoji bado huwa zinapitishwa na kuungwa mkono kwa asilimia mia moja na wabunge wa CCM ambao ndio majority. Kitu ambacho naona ungeuliza, je sie wananchi tufanyeje pale bunge litakapopitisha bajeti ambayo hatuikubali au hatuoni kama ina manufaa kwetu? na hapo tuwaombe hao chadema na vyama vingine vya upinzani vituongoze ili kama tuna njia ya kuikataa basi tuitumie.
   
Loading...