Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo Wapinga Matokeo, Wataka Uchaguzi Urudiwe, pia NEC na ZEC zivunjwe

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,467
UPDATES:

05:55 Asubuhi: Viongozi wa vyama vya ACT na CHADEMA wakiongozwa na Freeman Mbowe, Tundu Lissu na Zitto Kabwe wanaingia kwenye ukumbi ambapo watafanya mkutano na waandishi wa habari.

MNYIKA: Viongozi wakuu wa vyama vyetu tumekuwa kwenye vikao vya mashauriano na vimeendelea leo asubuhi kwa hiyo yapo mambo ambayo tulikuwa tunakamilisha na sasa tuko tayari kwa viongozi wakuu kuzungumza na Taifa kupitia kwenu(Waandishi). Naomba kumleta kwenu mwenyekiti wa chama mwenyeji, mheshimiwa Freeman Mbowe.

MBOWE: Kwa niaba ya viongozi wenzangu, wagombea Urais Muungano na Zanzibar, niwasilishe tamko la pamoja la vyama vya CHADEMA na ACT kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 27 & 28 2020. Kwa uzito wa Tamko lenyewe nitasoma kama lilivyoandikwa kisha katika hatua zinazofuata nitaruhusu maswali.

=======

TAMKO
Sisi viongozi wa CHADEMA na ACT pamoja na wagombea wa Urais Muungano na Zanzibar na kwa niaba ya wagombea wetu katika nafasi ya udiwani, uwakilishi na ubunge, wanachama na wafuasi wetu tunatoa tamko hili kuweka msimamo wetu ya kutoyakubali matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 yaliyotangazwa na ZEC na NEC.

Kwa umoja wetu tunaamini kilichofanyika Oktoba 28, 2020 hakina sifa wala uhalali wa kuitwa uchaguzi mkuu bali ni unyang'anyi na uporaji wa kutumia nguvu wa haki ya watanzania wa kuchagua viongozi inayowataka kwa njia ya demokrasia uliofanywa kwa makusudi na tume zote mbili za uchaguzi yaani ZEC na NEC

==========

Maswali na Majibu
Watasemaje kama waangalizi wa uchaguzi wakikubali kama ambavyo baadhi yao wameshakubali
Mbowe alijibu kuwa hawana shaka na waangalizi wanaokubali uchaguzi huu kwa kuwa waangalizi walioletwa katika uchaguzi huu sio waaangalizi wenye weledi wa uangalizi bali ni watu ambao wanaweza kuwa wana malengo yao

Wanataka Uchaguzi urudiwe lini
Mbowe alijibu kuwa inategemea na namna ambavyo serikali italipa uzito suala hili

Mbowe aliulizwa kuhusu kushindwa kwake katika Jimbo la Hai
Amejibu maandamano haya sio kwa ajili ya Jimbo la Hai, wala matokeo ya Hai sio taswira ya maandamano ila Hai ni sehemu ya Jamhuri ambayo matokeo yake yote wanayapinga

MBOWE amesema kuwa hawatambui matokeo yote hata ya wale wabunge na madiwani wa vyama vyao ambao wameshinda

MANENO YA ZITTO
Amesema katika jimbo lake walitenga zaidi ya kura elfu 15 ziliandaliwa kuingizwa katika kila kituo, katika jimbo lake walifanikiwa kuzikamata kura 3000 kwa hivyo zaidi ya elf 12 ziliingia kwenye vituo

Amesema hiyo ndio taswira ya jinsi mfumo wa uchaguzi Ulivyokuwa katika Taifa zima

Amesisitiza hakukuwa na uchaguzi Oktoba 28, pia wanataka uchaguzi mpya utakaoongozwa na tume huru ya Uchaguzi kwa Tanzania Nzima

Aidha madhara ya yatakayotokea hawatayabeba bali waliofanya udanganyifu

Zitto: Tunafungua Ukurasa mpya wa mapambano ya demokrasia

MAJIBU KUTOKA KWA LISSU
Aliulizwa kama atakuwa mstari wa mbele maandamano
Amesema wamewataka wananchi waandamane, na wao ni wananchi kwa hiyo na wao watashiriki maandamano, hawezi kukwepa wajibu wake

Amesema Magufuli hajashinda Uchaguzi Mkuu huu, kwa kuwa wamekamata kura zilizopigwa kabla ya Uchaguzi,

Amesema alivyokuwa Kawe alisema kuwa Tume ilikuwa na kura Milioni 12 za Magufuli na hata Ushindi uliotangazwa ulitajwa ni kuwa Magufuli alishinda kwa kura Milioni 12

Swali > Itawezekanaje kuwa na Tume mpya ya uchaguzi, huku vyombo vya ulinzi na usalama vikibaki vilevile
Lissu amejibu ni lazima kuwe na reforms katika majeshi ya ulinzi na usalama

Sababu ya Maandamano
Tundu Lissu amesema kwa kuwa matokeo ya Urais hayawezi kupingwa mahakamani kwa sheria za Tanzania, hivyo mahakama itakuwa ni wananchi ili kupinga matokeo ya Uchaguzi yaliyopo



EDE5E3B8-FDAD-42BC-9F7F-86D72E278525.jpeg

52B0FD55-F842-4C83-84C4-2D71807B9012.jpeg
 
Niaje niaje?

Moja Kwa moja kwenye mada kuu, napenda kuwapongeza WATANZANIA wenzangu Kwa kuwa wazalendo kabisa. Bila shaka ninyi ni mashujaa na wa kweli kabisa katika maisha ya kawaida ndio, lazima tuseme ukweli panapohitajika uwezi kupata ubunge ukalipwa posho zako ukasahau walio kupigania uupate, hii ni dharau. Kira siku ni kujipost tu uko mtandaoni mkijidai na kujitapa kama ninyi ni matajiri wakubwa mnashinda kuvaa gold kwenda kwenye mahotel makubwa na familia mkijiona Bora kabisa ndio.

Una magari sita sijui matano yote umeweka majina yako kwenye kwenye plate number ambayo unalipia Kira moja karibu milioni kumi Kwa mwaka wakati aliye kupambania ubaki kwenye madaraka bima ya afya ya elfu arobaini tu hana, na uko comfortable kabisa kujimwambafai kwa visuti vyako vya sinza kijiweni na vimoka vyako vya kariakoo sokoni.

ASANTE WAJUMBE KWA KUTOWAPIGIA HAWA MABAZAZI WAKUBWA, unajifanya unatupigania huku watoto wako wanasoma international schools Sisi wetu wanasoma changanyikeni haafu unasema tuko sawa wewe ni TAAHAHIRA MKUBWA.

SASA KWA TAARIFA YAKO HATUANDAMANI TUNAUNGA JUHUDI LIWALO NA LIWE. WEWE UKIONA HAPA PAGUMU HAMA NCHI MWANASESERE WEWE.

Nawasilisha
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom