Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo Wapinga Matokeo, Wataka Uchaguzi Urudiwe, pia NEC na ZEC zivunjwe

njeeseka

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
1,356
2,000
Hili tusi Mbowe Mungu anamuona...yaani sisi Watanzania 12M twende mirembe hii ni dharau kubwa dhidi yetu....
Mbowe sio kosa lake, kisu kimezama mfupani safari hii na yeye kakosa ulaji, madeni ya kampeni atalipaje, wa kwanza kuwa punguani ni mawakala wao waliotokeza hadharani kukubali matokeo.

Njaa ni mbaya sana inaweza kukutia upofu.... subiri tuone wakitangulia mbele ya maandamano. Hii ndio karata yao ya mwisho...
 

NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,208
2,000
Safi sana Chadema na ACT. Haya ndo maamuzi niliyokuwa nayatarajia. Tukikalia kimya udhalimu huu nawahakikishieni, watanzania kwenye hii miaka 5 tunaenda kuchinjwa kama kuku...
Nimekuwa nikijiuliza hapa hivi nikiandamana ni kwaajili ya Mbowe na Genge lake wapate Mihela na mikuku, mm nafaidikaje hapo baada maadamano?

Sasa mara pa mguu wangu au mkono he watakuja Mwimbili maana ugomvi na vyombo vya Dolla sio wa mchezo.
 

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,424
2,000
"Msemakweli ni mpenzi wa Mungu". Tuache kubwabwaja, tuseme ukweli. Na pinga ukweli kwa ukweli, na sio kwa kurudiarudia uongo. A lie cannot be transformed into truth by merely repeating it endlessly.

1. Kuna USHAHIDI kwamba kura zilijazwa isivyo halali kwenye masanduku ya kupigia kura.

2. Kuna USHAHIDI toka Kawe wa watu kukamatwa na mifuko yenye karatasi za kura za chama kimoja.

3. Hairuhusiwi kupeleka mahakamani malalamiko kuhusu kutotendewa haki katika uchaguzi wa Rais.

Sasa katika hali hiyo wananchi wakiamua kuandamana hutawaelewa?

Nadhani ni Rais Mstaafu Kikwete aliyeonya kuhusu chama kutegemea risasi za polisi ziwahifadhi madarakani.

Viongozi wa Kanisa Katoliki, na viongozi wengine wa dini, wameshuhudia wenyewe USHAHIDI kwamba uchaguzi huu haukuwa wa HAKI. Wanalazimika kutoa tamko uchaguzi urudiwe chini ya tume huru.

Power corrupts, and absolute power corrupts absolutely. Nawasikitikia sana viongozi wa ccm. Wako katika culture ambayo saa zote inawafanye wawe karibu sana na shetani, na mbali sana na Mungu. Woe to them.
 

Congressman

JF-Expert Member
Jun 2, 2020
310
1,000
Uhuni wa CCM jumatatu ndiyo mwisho, na wasifikiri haya yatakuwa kama maandamano ya Mange. This is really political revolution.
 

njeeseka

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
1,356
2,000
Uhuni wa CCM jumatatu ndiyo mwisho, na wasifikiri haya yatakuwa kama maandamano ya Mange. This is really political revolution.
Kama mnadhani wa TZ ni mapunguani kama mnavyodhani ingieni barabarani nyie mnaoshinda mitandaoni, mara vpn mara USA, UK hakuna kitu kama hicho
 

John7371

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
779
1,000
Mimi kama mwanamke ninayejielewa siwezi kuwa na mwanaume mwenye akili za kiboya na coward kama wewe.

Sifa ya mwanaume ni kupambana...tena akae mbele kabisa kutetea Nchi yake na kizazi chake..
Ni mwanaume wa jinsia tu au siyo? 😁 😁 😁
 

Shehullohi

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
940
1,000
Huyu Mbowe ni mpumbafu wa kwanza. Kipanga/ kichwa mpumbafu. Eti eti, eti, eti....
waangalizi walioletwa safari hii wana malengo yao. Tusemeje sasa juu ya malengo yenu cdm ya kurudisha ukoloni kwa 'mlango wa nyuma'

Mkoloni wa mwanzao angalau alikuja wakati ule wa mababu zetu akiwa mkono mmoja kashika misahafu. Biblia wazungu na Korani waarabu.

Mkoloni anaye letwa na Lissu na Mbowe na cdm yao safari hii mkono mmoja kashikilia ubeberu na mwengine ushoga. Lissu anataka awarudishe hawa kwa kupitia mlango wa nyuma. Zingatia maneno 'mlango wa nyuma.'

Ni Watanzania matahira tu watakao waunga mkono hawa kwenye huu ukawa mpya wa 2020. Ukawa wa maandamano haramu. Matahira hawakosekani. Kule Hai walikuwepo walilipwa buku tatutatu na wakaishia kugugumia maumivu katika vitanda vya sibitali. Hata hapo kwenye mkutano wa waandishi wa hanari tumewasikia wakipiga tumakofi twa hapa na pale.

Serikali isicheke na hawa viongozi na isikikubali wananchi wachache wakatumiwa kama kinga na nyenzo kwa hawa viongozi ili wafikie malengo yao haya ya kijingajinga. Serikali inaposhughulika na huu Ukawa wa maandanano ihakikishe inalenga hawa viongozi wenyewe. Ili mwisho wa siku they have to face and feel the consequences of their stupidity.

Kwenye maandamano hayo vyombo vya ulinzi na usalama vilenge kuyazima kwa kuhakikisha viongozi ndio wanalipia huu ujinga wao.
 

santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
1,253
2,000
Huyu Mbowe ni mpumbafu wa kwanza. Kipanga/ kichwa mpumbafu. Eti eti, eti, eti....
waangalizi walioletwa safari hii wana malengo yao. Tusemeje sasa juu ya malengo yenu cdm ya kurudisha ukoloni kwa 'mlango wa nyuma'

Mkoloni wa mwanzao angalau alikuja wakati ule wa mababu zetu akiwa mkono mmoja kashika misahafu. Biblia wazungu na Korani waarabu.
Mkoloni anaye letwa na wa Lissu na Mbowe wa cdm safari hii mkono mmoja kashikilia ubeberu na mwengine ushoga. Lissu anataka awarudishe hawa kwa kupitia mlango wa nyuma. Zingatia maneno 'mlango wa nyuma.'

Ni Watanzania matahira tu watakao waunga mkono hawa kwenye huu ukawa mpya wa 2020. Ukawa wa maandamano haramu. Matahira hawakosekani. Kule Hai walikuwepo walilipwa buku tatutatu na wakaishia kugugumia maumivu katika vitanda vya sibitali. Hata hapo kwenye mkutano wa waandishi wa hanari tumewasikia wakipiga tumakofi twa hapa na pale.

Serikali isicheke na hawa viongozi na isikikubali wananchi wachache wakatumiwa kama kinga na nyenzo kwa hawa viongozi ili wafikie malengo yao haya ya kijingajinga. Serikali inaposhughulika na huu Ukawa wa maandanano ihakikishe inalenga hawa viongozi wenyewe. Ili mwisho wa siku they have to face and feel the consequences of their stupidity. Kwenye maandamano hayo vyombo vya ulinzi na usalama vilenge kuyazima kwa kuhakikisha viongozi ndio wanalipia huu ujinga wao.
Unafokafoka nini sasa? Maandamano ni swala la halali na haki ya raia. Maandamamo ni kati njia za kuwasilisha ujumbe, na hufanyika duniani kote! Sema wengi wenu hapa nyumbani ni mateka wa fikra, Polepole akishakuambia kitu chochote unakimbilia kuhalalisha tu kwa ujinga! Watu wanahisi
Wamedhulumiwa, Kwanini wasioneshe hisia zao?!
 

Jimbi

JF-Expert Member
Aug 16, 2010
3,039
2,000
Sanaa mwanaumee we nendaa ....msijee mkaanza kutusumbua kuomba michango ya matibabu ...😎😎😎😎
Askari polisi atakaye tuletea fujo kwenye maandamano yetu ya AMANI tutachinja familia yake hadharani, wewe endelea na shughuli zako acha sisi tuka andamane.
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
9,899
2,000
Madai ya Tume huru za Uchaguzi ni madai sahihi kabisa na yalipaswa kuja tangu November 2015.

Wenzetu Kenya, Malawi na Ghana walipata Tume Huru baada ya jasho na damu kumwagika.

Lissu na Mbowe waongoze tu hayo maandamano hiyo Jumatatu. Polisi wanatarajiwa kufanya yao kwa nguvu kubwa lakini hizo ndizo gharama za demokrasia

Inabidi tuzoee kuishi bila internet kwa angalau mwezi mmoja
 

Mkandara

Verified Member
βœ…
Mar 3, 2006
15,486
2,000
NINAYO MSWALI MACHACHE..

Yahusu Uchaguzi Mkuu wa Taifa 2020.

1. Kwa nini Wananchi wengi hawakutumia UHURU na HAKI yao ya msingi kujitokeza kupiga kura? (Kati ya Wapiga kura mil. 29.1 Wamepiga Kura watu Mil.15.8) kuna ombwe la zaidi ya mil.13.

2. Inadaiwa Uchaguzi huu haukuwa wa Haki na Amani, Kwa nini vurugu zimetokea baada ya kutangazwa Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Taifa na sii kabla?

3. Mpaka wakati vituo vyote vya Kupiga kura vinafungwa, hakuna Mgombea au Kiongozi hata mmoja wa Upinzani alokamatwa, kupigwa ama alodai na kulalamikia kuwa Taratibu zote hazikufuatwa isipokuwa baadhi ya vituo visivyozidi 20 kati ya vituo Elfu 37 kwa Mawakala wao Kuzuiwa.

4. Baada ya Kiongozi wa CCM - Zanzibar kuvamiwa na kupigwa mapanga, Serikali iliweka Ulinzi mkubwa Zanzibar kwa Usalama wa raia wote lakini Upinzani wamelaani vikali kuwepo kwa Ulinzi huo Visiwani. Nini hasa ilikuwa dhamira yao ikiwa Ulinzi usingekuwepo.

5. Nasikia Viongozi wa Upinzani wanayakataa matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa visingizio vya NEC na ZEC kutokuwa vyombo huru. Kwa nini hawakuweka Madai haya kabla ya kutangazwa Matokeo ya Uchaguzi Mkuu?

6. La mwisho, nitarudia tena hoja yangu ya siku zote. Kwa nini Wananchi na Viongozi wa vyama vya Upinzani kwa.nchi za Kiafrika, huwa hawakubali Matokeo ya Uchaguzi hata kama wanajua Wameshindwa. Kwao Uchaguzi Halali ni ule tu unao kiondoa Chama Tawala madarakani?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom