Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo Wapinga Matokeo, Wataka Uchaguzi Urudiwe, pia NEC na ZEC zivunjwe

Wanawaza ile mikopo.. ruzukuuuuuu ndio Mbowe analia kabisa. Pesa ya familia wanaikosa kivileeeeee

Watulie, ila duh Wananchi mumewatenda hawa...loooo.. tabu hawatabadilika.. wamuombe Sr. Slaa msamaha pia
 
Mbona unakwepa maswali jomba?

Hivi tulipowaambia acheni kuwekeza akili zenu kwa akina kigogo njooeni field mlituona hatuna akili ee?

Wezi, vibaka, wakora, Majambazi, wanyori, bandits, mijizi, matapeli, nk ni majina ya wale wale. Lugha tofauti, level tofauti na vifaa tofauti vya kazi.
 
Safi sana Chadema na ACT. Haya ndo maamuzi niliyokuwa nayatarajia. Tukikalia kimya udhalimu huu nawahakikishieni, watanzania kwenye hii miaka 5 tunaenda kuchinjwa kama kuku.

Ni uamuzi mzuri sana wa kufanya maandamano haya nchi nzima. Nasisitiza kusiwe na kurudi nyuma. Mikoa yote, Mbeya, Kagera, Songwe, Mara, Arusha , Kilimanjaro, Lindi , Mtwara, UNGUJA na Pemba, tuandameni kweli kuelekea ofisi za Tume ya Uchaguzi. Huu haukuwa ni uchaguzi bali uchafuzi na tukiukalia kimya tumeisha wote.
 
Wanaanza maandamano J3 tarehe 2, watu wapumbavu sio wa kuwafuatilia ujinga mtupu. Huwezi kuingia kwenye uchaguzi ukashindwa then unaandaa maandamano. Haya ngoja tuone hiyo tarehe mbili (02/11/2020) ya maandamano kama Lisu na Mbowe pamoja na familia zao wataongoza hayo maandamano.
 
Huna jipya, unakazania tu wagomee uchaguzi nothing else, ukiambiwa mbona walishagoma hakuna kilichobadilika huna majibu, akili imekuganda
Mgomo unapaswa kuwa endelevu.

Unagoma mpaka kinaeleweka.

Siyo unakuwa mtu wa matukio ya hapa na pale.

Goma 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, 2020, 2025 na kuendelea.

Kwani Makaburu walipogomewa na jumuiya ya kimataifa, waligomewa kwa siku moja tu?

Wewe unafikiria tukio moja moja tu.

Hata hivyo, sijali sana.

Endeleeni tu kushiriki na kama hamtoshinda chochote cha maana.
 
Watu wenyewe hawafiki hata milioni 3 halafu wanataka kutusumbua watu milioni 12.
 
Amani iwe nanyi.

Nyie ndio walinzi wa Watanzania, nyie ndio mnashika silaha kwa niaba ya watanzania. Nyie kama jamii ya watanzania na sehemu ya watanzania mmeona kilichotokea tarehe 28 ambapo kura zilipigwa ila watu wametangaza matokeo yao walioyandaa kabla hata ya uchaguzi. Nyie ni mashahidi na mmeona yote.

Nyie pia mnajua kuwa wapinzani ni watanzania, ni ndugu zenu na ni sehemu pia ya jamii yenu kama watanzania. Maisha ya kuwa magumu kwao ni yapo magumu na kwenu pia, bei ya sukari ikipanda kwao imepanda na kwenu pia na hata watoto wao wakikosa elimu bora na mikopo au ajira ni watoto wenu pia yamewapata haya.

Ombi langu kwenu.
Vyama vya upinzani vimetangaza kufanya maandamano ya amani kuanzia jumatatu, tarehe 2. Ni maandamano ya haki, kudai kurudiwa kwa uchaguzi na tume huru kufanya uchaguzi huo.

Naomba nyie kama sehemu ya watanzania hawa nanyi muwe sehemu ya kudai haya mabadiliko. Msitekeleze amri zisizo halali na kuwapiga na kuwaumiza watu au hata kuua watu kwa sababu mabadiliko wanayoyadai hayatawanufaisha wao tu bali sehemu nzima ya watanzania na nyie mkiwepo pamoja na vizazi vyenu.

Naomba msikubali amri mbovu na muwalinde watanzania kudai haya mabadiliko kwa amani.

Mungu awabariki.
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom