Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo Wapinga Matokeo, Wataka Uchaguzi Urudiwe, pia NEC na ZEC zivunjwe

Vijana jiulizeni Kwann uandamane?

Maandamano yenyewe ya amani kwa upande mmoja, upande wa pili(Jeshi) wamejiandaa kwa vita.

Yaaani maana yake maandamano ya kikondoo kwenu nyinyi waandamanaji.

Kwa lugha nyepesi ni kwenda kuomba kuvunjwa mataya na viuno kwa amani.

usifanye huo ujinga. Yaaani ujipeleke na bango zito, jua Kali au mvua ili ukavunjwe taya na kiuno?

Mfano tukiambiwa"Kila mtu abebe silaha aje vitani kupambana na jeshi" hapo ningepima kama Nina sababu ya msingi ya kupigana vita, na kama ipo ningeaga familia, ningeenda vitani.

Ila naambiwa"kila mtu abebe bango apeleke kiuno/taya likavunjwe kwa amani na jeshi" siwezi Fanya huo utoto. Bora nitumie hizo hasira kulima shamba hata ekari moja nipande michongoma.
 
Nakumbuka humu jamvini nilipendekeza vyama vya upiñzani vifanye coalition au kukubali uchaguzi Wa Rais upite bila kupingwa ili pesa isipotezwe bila sababu na pengine zisaidie kustawisha vyama vyao sasa wameona mwanguko Wa mende!

Hata wakienda mtaani wataandamana peke yao.

Poleni ndugu zetu.
 
Leo tarehe 31.10.2020 vyama viwili vya upinzani vya CHADEMA na ACT - wazalendo vimetoa tamko la kutotambua matokeo ya uchaguzi mkuu na kuitisha maandamano ya nchi nzima kuanzia jumatatu ya tarehe 02/11/2020.

My take
Vyama hivi havikupaswa kuvitenga vyama vingine vya upinzani kwenye hili. Kama malalamiko yao yana msingi basi ilipaswa vyama vingine vya upinzani viwaunge mkono. Kukosekana kwa vyama hivyo kunawakata mkia katika mpango huo wao.

Kitendo cha kutangaza maandamano ndio kimewamaliza. Jumatatu hawatapata watu na Kama watapata watakuwa ni watu wachache sana huko Arusha, Dar na Tarime. Hawatafika watu 200 na wakifanikiwa itakuwa ni hiyo siku ya kwanza tuu.

Kitendo cha watanzania kususia maandamano kitawanyima legitimacy na credibility ya madai yao. Hata huko wanakoshitaki wataona jinsi wananchi wa Tanzania wasivyotaka vurugu.

Tuombe uzima tuone hiyo j3 lakini uwezekano mkubwa ni kuwa hakuna mtanzania wa kuandamanishwa ili mtu flani aende ikulu. Vijana wengi sasa hivi wanaajira zao za bodaboda zinazowaingizia vipato. Wahitimu wa vyuo hawadanganyiki kirahisi kwani kuandamana hakutawapa ajira.

Ushauri
Mambo haya yanategemewa sana kufanywa na vijana hasa ambao hawana shughuli maalumu. Tuhakikishe tunafanya kila tuwezalo kuwashauri vijana wetu kuwa kamwe wasije wakashiriki maandamano hayo ambayo yanaweza kuleta tatizo kubwa nchini kwetu.

Nawasihi wapinzani watafute njia nyingine za kutafuta haki wanazoona wamepokwa. Haifai kwenda ikulu kwa damu za vijana wanyonge.

Amani
 
Kigogo na Amstadamu wamesema uchaguzi utarudiwa
Na makamanda utaona wana coment kwa furaha huku wakimshukuru kigogo!

Wamesahau kuwa aliwadanganya kwamba ana kituo chake cha kukusanyia matokeo hivyo nec watakiona

Aisee..... Aibu hii
 
Leo tarehe 31.10.2020 vyama viwili vya upinzani vya CHADEMA na ACT - wazalendo vimetoa tamko la kutotambua matokeo ya uchaguzi mkuu na kuitisha maandamano ya nchi nzima kuanzia jumatatu ya tarehe 02/11/2020...
Hivyo vyama vingine unaweza kuwasaidia kutoa tamko,ukiona vipi meza wembe
 
Kumekuwa na sintofahamu juu ya uchaguzi mkuu wa Tanzania.

Wapo wanaosema ushindi wa Magufuli ni wa halali na wale wanaosema ni wa kuiba. Kwa kuwa nina hakika kila mmoja anaujuwa ukweli juu ya hili jambo, ili kuondoa unafiki naomba kila mmoja aitikie dua hii ili tujue ukweli.

Hii kwa wale wanaosema kaiba kura.

Ewe Mungu wa mbingu na ardhi nina hakika Magufuli hakushinda kwa kura halali katika uchaguzi uliofanyika 28/10/2020. Kama naongea uongo basi nijaalie mimi na familia yangu iwe na mkosi na iwe dhalili duniani na akhera.

Hii kwa wale wanaosema kashinda kihalali bila kuiba kura.

Ewe Muumba wa mbingu na ardhi nina hakika Magufuli ameshinda kwa kura halali katika uchaguzi uliofanyika 28/10/2020. Kama naongea uongo basi nijaalie ugonjwa mbaya sana mimi na familia yangu na tuishi kwa maisha magumu mpaka tunaingia kaburini.

Cha kufanya quote sehemu ya dua yako halafu andika Ameen.
 
Mleta mada ulishawahi kuolewa?
Kama bado, basi tafuta sasa mume. Na kama umeshaolewa basi tulia kwa mumeo.
Acha mambo ya kindezi.
Nitapigania amani ya nchi hii mpaka tone la mwisho la damu yangu. Siwezi hata kidogo kuruhusu uvunjifu wa amani etinili mtu flani aende ikulu. Nasema hapana na nikiwa Kama raia ninayejitambua, nachukua fursa hii kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama vucbukue hatua stahiki haraka iwezekanavyo na vikizembea namuomba Rais aviwajibishe Mara moja.

Tanzania ndio inapokea wakimbizi na kamwe watanzania hawawezi kuwa wakimbizi.

I wish ningekuwa na mamlaka flani
 
Leo tarehe 31.10.2020 vyama viwili vya upinzani vya CHADEMA na ACT - wazalendo vimetoa tamko la kutotambua matokeo ya uchaguzi mkuu na kuitisha maandamano ya nchi nzima kuanzia jumatatu ya tarehe 02/11/2020...
Kwani hujaona kuwa navyo vimetoa tamko la kumuunga mkono mzee baba? Kwahiyo hapo nani kamtenga mwenzake? Na kwa tamko lao lilivyo nadhani Mbowe hakukosea!
 
Mwanamke alieachika kwa umalaya wake utamjua tu hata kwa maandishi yake. Shenzi kabisa
 
Mleta mada ni kenge tu.
Matusi sina shida nayo, we nitukane mpaka hasira zako ziishe zooote lakini maandamano tena yasiyo na kikomo eti kumpinga Rais ambaye amechaguliwa hairuhusiwi. Narudia tena kamwe hairuhusiwi. Nawataka polisi kuchukua hatua haraka sana vinginevyo nitaomba wawajibishwe kwa kushindwa kusimamia amani ya nchi hii.

Watu hawalali wanakesha kuhakikisha nchi hii inasonga mbele na watanzania wanajisikia furaha kwa kutatuliwa kero zao halafu watu wachache watake kuharibu mafanikio yaliyofikiwa. Hii haiwezekani hata kidogo. Hata kama nitabaki peke yangu, hili jambo la maandamano nitalipinga mpaka ninaenda kaburini.
 
Aman NI zao la HAKI.....
Tume imeshamtangaza Rais Magufuli. Magufuli halali usingizi kuipigania nchi hii na watanzania wameona halafu watu wachache wanaotumiwa kutaka kutifanya Kama Tunisia, Libya na Zimbabwe hawawezi kuvumiliwa.

Cc: IGP Simon Sirro
George Simbachawene
 
Back
Top Bottom