Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo wanadai uchaguzi wa haki wakati Wagombea Urais wao hawajawatendea haki

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,909
51,904
CHADEMA kupitia vikao halali kabisa vya kikatiba walimteua mgombea urais wao wa Zanzibar.

Lissu anahubiri haki lakini alipofika Zanzibar akaanza kumnadi Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo. Haki ya Mgombea wake akaitupa kwenye dustbin.

ACT-Wazalendo nayo inahubiri haki ikamteua Membe kuwa mgombea wao kupitia vikao halali kabisa ghafla haki wakaacha wanamuunga mkono Tundu Lissu.

Hawa matapeli wanahubiri uchaguzi wa haki wakati wenyewe wameanza kucheza rafu kwa kutowatendea haki wagombea wao poa tu tukutane October 28.

Michezo ya rafu za kutotenda haki mmeanzisha nyie halafu mnahubiri haki.

Charity begins at home
 
Bado sijaamini kama Magufuli amekwapua hekari elfu 25 huko Karagwe, nasubiri ajibu hili kama alivyojibu suala la ajira kwa kuajiri watu wachache saaana. Na namna alivyosema kitambulisho cha umachinga si lazima huku kunawatu aliwatumbua kwa kushindwa kufikia target ya makusanyo ya fedha za walalahoi,waliozulumiwa fedha zao kupitia vitambulisho fake visivyo na jina.

Je Magufuli amejimilikisha ekari elfu 25 huko karagwe?. Bado nasubiri hoja ya utetezi wake.
 
Muongeaji Lisu alionyesha hati ya ardhi kama ushahidi? Au alikuwa akitoa mimacho tu anapoongea? Yeye Lisu ndie atoe ushahidi
 
Muongeaji Lisu alionyesha hati ya ardhi kama ushahidi? Au alikuwa akitoa mimacho tu anapoongea? Yeye Lisu ndie atoe ushahidi
Mkuu tunahitaji JPM aseme neno juu yahiyo aridhi, mbona suala la majimbo kalisemea,suala la machinga, ndege ,uwanja wa chato, ajira akaamuru kabisa watu elfu 13 waajiriwe, tunasubiri nahio yakujimilikisha aridhi ya walalahoi.
 
Back
Top Bottom