CHADEMA na ACT Wazalendo ni wanafiki sana tunahitaji chama kipya cha siasa

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,661
15,026
Akiwa Mkuu wa Mkoa wa DSM, CHADEMA walimchafua sana Makonda na kumsingizia mambo mengi.

Ugaidi,Uuaji, utesaji n.k tena walienda mbali na kumhusisha na dhulma kubwa kubwa,rushwa na upigwaji risasi wa Tundu Lissu.

CHADEMA waliuaminisha Umma kuwa Makonda atakuja shtakiwa kwa makosa yake lukuki kwa namna ambavyo waliyatanabaisha. Nmesubiria kusikia hata kesi moja dhidi ya Makonda kuhusiana na Shutma hizo. Mpaka leo kimya.

Hii inaonesha Makonda alichukiwa na kuonewa sana na Chadema. Huyu jamaa ndo alikuwa punching bag ya Chadema. Baada ya kutokuwa Mkuu wa Mkoa imeonekana kumbe hakuwa a makosa yoyote yale. Issue ilikuwa ni Ukuu wa Mkoa.

Natoa wito Chadema kumwomba Radhi Makonda Paul na kuahidi kuwa hawatarudia tena tabia hizo za kuchafua watu.​

20211028_123608.jpg
 
Hivi Bashite anaweza kusafishika kiulahisi hivi ukilinganisha na matendo yake yale ??

Ninani asije jua maovu ya Makonda?
Wewe mwandishi unakumbuka akifanya Ile ya maziko ya mzee Mengi ?

Je! Shutuma zile mpaka katibu mkuu waccm wakati uleanalalama umesahau kilahisi hivyo ???

Duhh!
 
Wewe ngoja Makonda akifunguliwa mashtaka ndio akili zako zitakaa sawa
 
Wasingekuwa wanapigwa mabomu kwenye mikutano yao, viongozi wake kubambikiwa kesi na kuporwa kura.

Hata Lipumba alishawahi kupigwa mabomu sana na kwenda mahakamani mpaka kuvunjwa mkono na kuibiwa kura zake... Lipumba alishawahi kushinda Urais akaibiwa kura aka za kichina akiwa CUF....au umesahau..

TLP na NCCR mageuzi wakiwa na Lyatonga, Masumbuko lamwai, Mabere Marando nk walishawahi kuchezea mabomu na kukaa sana jela pia na kial aina ya usumbufu...
 
Yes, ni lazima CCM tutengeneze chama kikuu cha upinzani ambacho kitafanya kazi bega kwa bega na CCM yetu ili kuwaletea wananchi maendeleo. Badala ya hivi vyama kila kukicha ni chokochoko tu hakuna jema, mara katiba mpya, mara haki za binadamu, mara uchaguzi haukuwa huru na haki, mara tozo si sawa sasa tushike lipi? - hivi uchaguzi ukiwa huru ndiyo utaushiba? ndiyo utapeleka watoto wako shule zuri wakute walimu na madawati, ndiyo utapata maji na umeme vijijini?
 
Demokrasia haiwezi kustawi kwa nchi masikini. Nafikiri nimeeleweka. Bado watu wanatafuta uongozi ili wapate mlo na familia zao
 
Wanasiasa wote ni wanafiki iwe chama tawala au hao wapinzani......tena ni waongo sana
 
Back
Top Bottom