MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Nataka kuwashauri viongozi wakuu wa vyama hivi vya upinzani ambavyo vinaonekana kukikosesha usingizi chama chetu cha CCM upande wa bara na Visiwani.Msikosee hapa kwa tamaa za muda mfupi, kuweni na long term plans.
URAIS
Urais kwa Upande wa bara mwachieni Tundu Lisu wa CHADEMA agombee na visiwani mwacheni Maalim Seif Agombee, najaribu kusema hivi ni kutokana na aina ya Wagombea wa CCM tulionao.Kwa bara Dr Magufuli kupambana na Lissu ni sahihi kabisa kulingana na siasa za hawa wawili za ukali na za kutoogopana. Ni wanasiasa wachache sana Tanzania wenye ujasiri wa kuikosoa serikali ya CCM hadharani bila kuogopa ukimtoa Tundu Lisu.
Upande wa Zanzibar hapa siwezi kuongea sana kwa sababu iko wazi kabisa kua Maalim Seif siasa za huko yeye anauzoefu nao na ndiyo nafasi yake.
Ningemuomba Mzee wangu Benard Membe atulie tu maana anayo nafasi kubwa sana ya kupata nafasi za juu serikalini upinazani ukishinda na hata kua PM, anayo nafasi hata ya Spika wa bunge la Jamhuri ikiwa mtakuwa na sayansi nzuri ya kugawana majimbo kiufundi kisha mkaachiana.
ACT bara msihangaike na Urais kwa sababu bado chama chenu hakijawa na ushawishi mkubwa sana kama ilivyo Zanzibar,bara Urais mking'ang'ania hamtashinda kuliko ambavyo mngetafuta wabunge wawasaidie kuongeza nguvu na nje ya bunge .Kwa bara CHADEMA ndio wenye Ushawishi mkubwa karibia 20 ya mikoa ya Tanzania bara ukiachia ile michache 5 ya Pwani ambayo ACT mtakua na nguvu kiasi.
UBUMGE
Msikomalie Urais mkaacha kukitwaa Chombo hiki muhimu cha kufanya maamuzi, Maana mkilitwaa bunge hata Rais akitoka CCM hatoweza kufanya chochote bila ya Spika kuamua, yaani sawa na Democratic na republican vya USA.
Pigeni na kisha zichangeni hesabu zenu vizuri kuachiana majimbo, sahihisheni mapema kwa kushirikiana wote mfute madhaifu ambayo CCM wamekua wakiyatumia kuwashinda.
Wekeni wagombea wenye ushawishi kwa umma, wapeni elimu za namna ya kumudu uchaguzi ikiwa bado ni mapema. Chukueni form mapema mzipitie na wanasheria wenu kifungu kwa kifungu kisha zirejesheni mapema msiwape nafasi wakurugenzi kuja kufanya yao.
wawikeeni mapingamizi mapema wagombea wa CCM wasio na sifa msisubiri ninyi kuja kuwekewa muenguliwe, waengueni wao wenyewe.
UDIWANI
Hizi nafasi ni muhimu sana, ndiyo zinakipa Chama kulitwaa Halmashauri za miji,Wilaya, manispaa na jiji. Mkipata madiwani wengi ndivyo mtakavyopatq halmashauri nyingi zikawa chini yangu. Hii itawarahisishia sana kuimarisha na kutekeleza sera zenu bila bughudha.
HESABU HII LAZIMA MUENDE NAYO.
Ikiwa Jimbo X lina wapiga kura 10, CCM inaweza kupata kura 4, CHADEMA kura 3 na ACT 2, Maana yake mkiungana mtapata kura 6 na mbunge mliyeemuunga mkono ninyi lazima ashinde.
Ni hivyo hivyo hesabu ni ile ile kwenye Urais na Udiwani.
SHTUKIENI NJAMA NA UJANJA HUU WA CCM MAPEMA.
Kuna tetesi kua kuna mbina ya siri sana imeanza kutumiwa na CCM kuwashawishi wagombea wenu kuwapa madau manono waachie majimbo waunge mkono juhudi wakati wa kampeni na ninyi mbaki bila wagombea wao wapite bila kupingwa.Tetesi hizi zipo na ni mkakati kwa kila jimbo na kila kata.Watu wenu wengi bado wana njaa na tamaa, mkifeli katika hili mmekwishaa.
wapimeni watu wenu mapema kabla hawajachukua forms za kugombea.Litaftieni mwarobaini wake haraka iwezekanavyo.Msiponielewa nawapa pole sana na shauri yenu.