KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
CCM wamejipanga vizuri kupata ushindi, hata kama ni ushindi kwa njia isiyokuwa halali.
Miaka yote hii mitano, na kabla ya hapo, tumesikia manung'uniko yenu kuhusu ubovu wa usimamizi wa uchaguzi wetu unaowapendelea CCM. Miaka yote hii mmekuwa mkilalamika kuhusu jambo hili, lakini hatukuona mikakati yoyote mliyokuwa mkiiandaa kuzuia uharamia huu. Mmekuwa tu mkilalamika bila ya kutafuta suluhisho lake.
Huu uchaguzi mwingine unaokuja Oktoba, nao inaelekea kwamba matokeo ni yale yale na ulalamishi utaendelea vilevile.
Sasa tunawapa angalao pendekezo, ili msiendelee kuwa walalamishi tu, ni bora kujitayarisha vyema ili mlalamike mkiwa na ushahidi usiofichika kuhusu malalamiko yenu.
Haitoshi kulalamika tu, bila ya kuonyesha ushahidi wowote unaoonyesha malalamiko yenu kuwa ya msingi.
Ni lazima muwe na njia za kuweka ushahidi kamilifu zaidi katika kila jambo mtakalokuwa mmefanyiwa rafu. Tknologia zipo sasa za kukusanyia ushahidi wa uhakika utakaoonyesha wazi mnayoyalalamikia. Isiwe ni kulalamika tu, kama kule kwa Lowassa kudai kura milioni kadhaa bila ya ushahidi wowote.
Leo wakati mnaambiwa kwamba hata nakala za matokeo huenda msipewe, kwa nini nyinyi mkubali tu kauli hiyo hata bila ya kufanya juhudi za kuwa na uhakika wa kura zilizopatikana kituoni? Yaani haiwezekani kamwe kujua ni kura ngapi mmepigiwa na watu wenu, na juhudi zao hizi hata hamuwezi angalao kuonyesha ni kura ngapi walizowapa? Kwa nini muwakatishe tamaa wapiga kura wenu kiasi hiki.
Kazi yenu ya kwanza, mliyopaswa kuifanya tokea 2015, ni kuwa na watu wenu mnaoamini ni wanachama wenu wasiotetereka wala kuuza juhudi za wanachama wenzao huko waliko. Hawa ndio wanapaswa kuwa wasimamizi wenu katika vituo vyenu vyote vya kupigia na kuhesabu kura.
Haiwezekani watu wanaosimamia kazi mhimu kiasi hiki wawe ni wa kuokoteza tu mitaani siku chache kabla ya uchaguzi. Hawa ndio wanaouza kura za wapiga kura wenu na kuharibu juhudi zenu zote.
Kama kazi ya kuwatambua na kuwaanda hawa watu bado hamjaifanya hadi sasa, huo ni uzembe na mtastahili mtakachokipata.