Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo kutangaza kujitoa kwenye nafasi za Ubunge na Udiwani walizoshinda

Mlikuwa mnatuaminisha kuwa upinzani ndio unaochelewesha maendeleo, hata mwenyekiti wenu alituasa tusichanganye betri na magunzi. Sasa mbona mnachachawa tena pale mnapotaka kuachiwa bunge wenyewe?
Hakuna anayechachawa. Ila kuwaamuru wawakilishi wa wanwnchi wajitoe hiyo ni dhulma kubwa wanafanua na wataadhibiwa tena 2025
 
Wadau, amani iwe kwenu.

CHADEMA na ACT Wazalendo sasa wamevurugwa. Wamechanganyikiwa na wamevurugikiwa na akili. Kuna msemo unaosema kuwa ukiwa na hasira au furaha iliyopitiliza usifanye maamuzi yoyote makubwa. Hilo CHADEMA hawajalizingatia.

Ni hivi, nimedokezwa na Wasiri wangu wa Kuaminika ndani ya CHADEMA na ACT Wazalendo kuwa pamoja na mambo mengine kwenye kikao chao cha leo pale Mtaa wa Ufipa kwenye kijibanda cha Makao Makuu ya CHADEMA wanatangaza kujiondoa kwenye nafasi zote za Udiwani na nafasi moja ya Ubunge waliyoshinda kwenye uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020. Tayari Mbunge wa Nkasi, KHENANI ameshawishiwa kujiondoa na amekubali na anachosubiri ni tamko la leo.

Hayo yatakuwa maamuzi mabaya sana kuweza kuchukuliwa na vyama vya upinzani. Kususa kwao uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopita ndio umeleta Anguko Kuu kwenye uchaguzu Mkuu wa mwaka huu. Ni dhahiri kwamba maamuzi hayo yanaenda kuvifuta kabisa vyama hivyo kwenye ulingo wa siasa hapa nchini.

Sisi tunawachora tu kwa pembeni na tunawacheka Kwi kwi kwi kwiiiiii
Kiumbe mweusi katika ubora wake!!! Halafu kwa akili kama hizi pale wazungu wanapohoji uwezo wetu wa akili tunakuwa wakali!!!!
 
Hakuna anayechachawa. Ila kuwaamuru wawakilishi wa wanwnchi wajitoe hiyo ni dhulma kubwa wanafanua na wataadhibiwa tena 2025
Kuna mbunge hata mmoja wa ccm anayewawakirisha wananchi??! Au ni matakwa ya bwana yule!! Ila history ni mwalimu mzuri sana!! Sasa ni zamu ya jini mliyemfuga kuanza kuwala wenyewe!!! Ni suala la muda tu!!
 
Duuh! Yaani siasa ni mbaya sana. Yaani baada ya matokeo yote kutoka nchi imetulia tuliiiii!

Hali ilishakuwa mbaya sana kabla ya uchaguzi hadi wengine tumetolewa katika makundi ya whatsaap zenye mrengo ya CHADEMA kisa tu tunasema mapungufu yao.
 
Wapinzani wamejiondoa wenyewe. Wamekataliwa na Wananchi
Aliyekataliwa na wananchi MNA sababu gani ya kumwibia kura? Hivi wewe mbona unakuwa mpumbaf wa kiwango hicho?
Kwa akili yako waona uchaguzi ulifanyika? Ukijibu ndio, basi jitambue kuwa huna tofauti na anaye okota makopo.
 
Itakuwa hivi: Wakijitoa hao walioshinda ubunge wataamia CCM na kupewa nafasi ya kugombea tena...the rest is history!!
 
Mwaka huu mtaimba sana wimbo kwa kupokezana, ila ni lazima chadema ifutwe iwe kwa busara au kutumia nguvu.
Nyie lazima dawa ieaingie tu, si mlijifanya mnajua sana kuongea na kutukana??
Sawasawa. Kama Mungu aishivyo nakuhakikishia huu ndo mwanzo wa mwisho wa Ccm na sio chadema. Maandamano ya amani yaanza nchi nzima jumatatu
 
Kwa hiyo hamuamini kama Aida kashinda?
Aida Ameshinda Kama walivyoshinda wagombea wengi wa Chadema akiwemo Tundu Lissu. Lililofanyika ni vyombo vya usalama kuiamrisha NEC kuwaachia Chadema jimbo aliloshinda Aida tu. Sasa kwa sababu hatuwezi kuhalalisha ujinga na upuuzi tunasema uchaguzi urudiwe upya na maamuzi ya wananchi yaheshimiwe
 
Kwangu mimi huu ndio uamuzi kwa sasa tena wa busara sana.... Kuna haja ya watanzania kuuhitaji upinzani sio wapinzani wachache kuwalilia watanzania wasiojielewa..... Tena ikibidi waache kujihusisha na siasa kabisaaa tuone hayo maendeleo CCM tuliyokua tunayaimba na yakakwamishwa.....

Ili CCM itoke inahiji maamuzi collective ya watanzania na si watu wacheche waliojitoa kupambania wengi.... CCM DAIMA
Na sasa ndiyo kifo cha CCM kinakuja, baada ya hilo bunge la chama kimoja. Watakosa wa kumrushia ngumi watarushiana wenyewe na mpasuko utatokea utakaokiua chama. Muda wa kifo kwa CCM umefika.
 
Hakuna anayechachawa. Ila kuwaamuru wawakilishi wa wanwnchi wajitoe hiyo ni dhulma kubwa wanafanua na wataadhibiwa tena 2025
Wakiadhibiwa tena 2025 ni vema kwa CCM iendelee kubaki yenyewe bila hawa wanaokwamisha maendeleo.
 
Kumbe hatavwewe haujui wabunge wa viti maalum wanapatikanaje? Hakuna uwezekanonwa chama chochote zaidi ya ccm kupata viti maalum
Sawa Sasa wanataka kujadili Nini tena? Kama wao wameshindwa wamwache huyo mama atekeleze wajibu wake maana aligombea hawakumzuia na Mbowe hakuzuiwa, ina maana Mbowe angeshinda angesusa?
 
Na sasa ndiyo kifo cha CCM kinakuja, baada ya hilo bunge la chama kimoja. Watakosa wa kumrushia ngumi watarushiana wenyewe na mpasuko utatokea utakaokiua chama. Muda wa kifo kwa CCM umefika.
Unaacha kuona kifo Cha chadema unaona kifo Cha CCM kweli mwaka huu mmevurugwa.
 
Itakuwa hivi: Wakijitoa hao walioshinda ubunge wataamia CCM na kupewa nafasi ya kugombea tena...the rest is history!!
Itapendeza zaidi ili bunge liwe la CCM 100% wajadili vizuri maendeleo ya wananchi. Nadhani hata bunge sasa litakua live kwa sababu waliokua wanawasumbua sasa hawapo.
 
Unaacha kuona kifo Cha chadema unaona kifo Cha CCM kweli mwaka huu mmevurugwa.
Chadema na vyama vingine vinakufa. Baada ya hapo CCM pia inameguka na kupatikana vyama viwili ndani ya kimoja. Hapo ndipo upinzani wenye nguvu utakapoanza na kuua kabisa jina la CCM. Angalia mfano wa KANU iko wapi?
 
Tatizo la wafuasi wa ccm walio wengi ni vilaza hawafikirii kabla ya kutenda..
Wanashangilia upinzani ukifa lakininwajue zikianza kupitishwa sheria mbovu wote tutaisoma namba...

1.Kikokotoo kikipita hakina ubaguzi...uwe chadema uwe ccm kitakuka uoande wako.

2.kuna mbunge mmojaalisema Magufuli aongezewe muda wa utawala kinyume na uke muda wa kikatiba....hili likipitushwa kama lina faida tutaila wote kama lina madhara tutayapata wote....Rejea Uganda

3.Ogopa sana serikali ambayo haina watu wa kuikosoa, watafanya wapendacho ili mradi kutetea maslahi yao...walala hoi mluopiga kura wote mtaisoma namba bila kujalusha ni ccm au chadema..

Bunge lijalo tutarajia maajabu ya karne..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa Sasa wanataka kujadili Nini tena? Kama wao wameshindwa wamwache huyo mama atekeleze wajibu wake maana aligombea hawakumzuia na Mbowe hakuzuiwa, ina maana Mbowe angeshinda angesusa?
Lakini mbona mnateseka sana na huyo dada? Huyo dada alikuwa mbunge wa cdm bunge lililopita haitaji kufundishwa na wanaccm wala chadema afanye maamuzi gani. We relaxy akifanya uamuzi taarifa utazipata.

Mara hii mmekuwa na upendo na mbunge wa chadema? 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ni aibu kubwa sana kwa Mbowe, Msigwa, Lema, Mdee, Sugu kuzidiwa mbinu za medani katika kulinda kura na mtoto mdogo tena mwanamke Aida!
Wewe uliambiwa huyo Aida ndiyo aliwazidi hao wapinzani mbinu..?
Mkakati kwa uchaguzi huu ulishaandaliwa mapema kwa sisiem kutangazwa iwe iwavyo..

Mmesahau ile kauli ya bwana mkubwa kwa wakurugenzi alipiwaambia haiwezekani awape nyumba, gari, mshahara halafu watangaze mpinzani kashinda...ike kauli we uliielewaje.?
 
mbunge wa Nkasi acha kupoteza wakati na watu wasiojielewa kapige kazi bungeni chukua mshahara wako hudumia familia yako. Usikubaliane na watu walioshindwa. Fanya kazi
Tuliyajua haya mapema. Hakuna wanachojadiliana tukashindwa kukifahamu
 
Lakini mbona mnateseka sana na huyo dada? Huyo dada alikuwa mbunge wa cdm bunge lililopita haitaji kufundishwa na wanaccm wala chadema afanye maamuzi gani. We relaxy akifanya uamuzi taarifa utazipata...
Tatizo Nini Hadi Mara hi mnakuwa na chuki na mbunge wenu? CCM hatuhitaki upendo na wabunge wa Chadema ndo maana tunashangilia mlivyotembezewa kichapo ila tunashangaa baada ya kipigo toka CCM Sasa mnaanza kutembezeana kichapo wenyewe kwa wenyewe.
 
Back
Top Bottom