CHADEMA na ACT Wazalendo acheni utoto

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
CHADEMA NA ACT WAZALENDO ACHENI UTOTO

Kuna kamchezo kakipuuzi sana wanasiasa wa upinzani Tanzania wanakafanya kila uchaguzi mkuu unapokaribia. Jamaa hawajali madhara wanayotusababishia sisi wanachama wa vyama vya upinzani tunaoamini ipo siku tutaitoa CCM madarakani na kufanya mageuzi ya kiuchumi na kijamii ndani ya nchi yetu.

Taarifa za uhakika ni kwamba kinachofanywa hivi sasa ndani ya CHADEMA na ACT WAZALENDO ni kutengeneza njia ili wamsimamishe Bernard Membe kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya vyama vya CHADEMA, ACT WAZALENDO na washirika wao.

Kwamba kumbe Zitto Kabwe kumtangaza Membe kuwa Mshauri Mkuu wa ACT WAZALENDO na kutaka agombee Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa CHADEMA kujifanya wameendesha mchakato wa kidemokrasia wa kumchagua Tundu Lissu kupeperusha bendera ya CHADEMA ni danganya toto tu.

Hawa wote wanatufanya mabwege lakini ukweli ni kuwa Bernard Camilius Membe alishamaliza biashara na Freeman Mbowe zamani na alishamalizana na Tundu Lissu tangu akiwa Ulaya na akamalizia na Zitto ambaye hata hivyo ni mtu wake aliyemuandaa tangu wanaanzisha chama cha ACT WAZALENDO.

Yaani jamaa ameshatoa pesa ya kutosha na amewahakikishia kuwa wakimsimamisha yeye gharama zote za kampeni anazibeba mwenyewe na atachangia mzigo wa kutosha kwenye chama.

Kwa hiyo hii maana yake upinzani unakwenda kumsimamisha mwana CCM majeruhi ili agombee kiti cha Urais kama walivyofanya 2015 kumweka Edward Ngoyai Lowassa ambaye baadaye amerejea chamani kwake.

Ndio maana nasema huu ni utoto wa hali ya juu na ni muendelezo wa viongozi wa vyama vya upinzani Tanzania kujali matumbo yao badala ya kusimamia yale wanayoyaongea kila siku.

Yaani wanataka kumsimamisha Bernard Membe huyuhuyu ambaye walimchafua kwa kupiga mabilioni yaliyotoka kwa Muammar al-Ghaddafi wa Libya kwa ajili ya uwekezaji ambao ungewanufaisha Watanzania wanyonge, huyu huyu Membe anayehusishwa na ufisadi mkubwa akiwa Waziri wa Mambo ya nje.

Wanamtaka Bernard Membe huyu aliyefukuzwa uanachama na CCM juzi tu. Kweli domo la mshenzi likikosa nyama hula nyamafu.

Yaani leo Membe ndio akapambane na Magufuli? Daaaa nimeamini kuiangusha CCM nchi hii ni ndoto za mchana. Nakubaliana na Joshua Nassari kuwa CCM ni li mbuyu likubwa sana kuliko tunavyodhani upinzani.

Sasa masikini Lazaro Nyalandu sijui nae anaujua mchezo huu ama kapigwa daflao bila kujua. Mbowe, Mbowe, Mbowe Mungu anakuona.

Taarifa za uhakika ni kuwa Bernard Membe, Mbowe, Maalim Seif na Zitto Kabwe wamekuwa na vikao vya mara kwa mara kujadili mkakati huu.

Na hivi sasa baada ya kudukuliwa simu, Membe hataki tena mazungumzo ya simu, anakutana na watu uso kwa uso bila kujua kumbe hii imekuwa rahisi zaidi kupata taarifa zake za kila anapokwenda na kila anayekutana nae.

Sema jamaa anaonekana mtu hatari sana, maana bado anakutana na wana CCM tena viongozi ambao bila shaka anapanga nao mikakati hii ya Urais. Kwa sababu wanakutana usiku kwa kificho na anawapa pesa nyingi.

Mimi kinachoniuma ni huu upuuzi ambao vyama vya upinzani vinataka kuurudia tena. Wawaache wenzao ambao wamepambana nao wakati wote wakamchukue majeruhi wa CCM?

Yaani wafanye kama walivyofanya 2015 kumuacha Wilbrod Slaa aliyekuwa na mvuto mkubwa kwa Watanzania na kubadili gia angani kwa kumchukua Edward Lowassa.

Haya wacha tuone, ikiwa tofauti na hivi mtaniambia lakini upuuzi huu umevuja sana na ni aibu kubwa kwa siasa za upinzani Tanzania.

Mzee Kizito

Mkazi wa Mbeya
 
We will keep this thread for future reference maana October sio mbali. Na hapo ndio tutajua nani ni zombie anayefanya utoto.
 
Mkuu mleta uzi vipi hapo Iringa? Usingepigwa mkwara wa kugombea sasa hivi ungekuwa kwenu Tabora unalima tumbaku..
 
Wao wahangaike tu ila Chadema hatujasahau walivyotubadilishia gia angani 2015

Pole kwa Lissu namkubali sana ila bahati mbaya yuko kwa wasaka ruzuku wazee wa kaskazini
 
Naona unawaza kutolewa kuutawala huo mkoa wa Iringa baada ya kamanda Lissu kuwa rais, tutafuta vyeo vya ukuu wa mkoa, halafu niko namdogo wako Amina hapa, nayule mdogo wako anaeishi Tanga anasema kuwa,ulishindwa mpa mtaji akapewa mtaji wa duka languo na hawa wasanii wa bongo fleva.
 
*CHADEMA NA ACT WAZALENDO ACHENI UTOTO.*

Kuna kamchezo kakipuuzi sana wanasiasa wa upinzani Tanzania wanakafanya kila uchaguzi mkuu unapokaribia. Jamaa hawajali madhara wanayotusababishia sisi wanachama wa vyama vya upinzani tunaoamini ipo siku tutaitoa CCM madarakani na kufanya mageuzi ya kiuchumi na kijamii ndani ya nchi yetu.

Taarifa za uhakika ni kwamba kinachofanywa hivi sasa ndani ya CHADEMA na ACT WAZALENDO ni kutengeneza njia ili wamsimamishe Bernard Membe kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya vyama vya CHADEMA, ACT WAZALENDO na washirika wao.

Kwamba kumbe Zitto Kabwe kumtangaza Membe kuwa Mshauri Mkuu wa ACT WAZALENDO na kutaka agombee Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa CHADEMA kujifanya wameendesha mchakato wa kidemokrasia wa kumchagua Tundu Lissu kupeperusha bendera ya CHADEMA ni danganya toto tu.

Hawa wote wanatufanya mabwege lakini ukweli ni kuwa Bernard Camilius Membe alishamaliza biashara na Freeman Mbowe zamani na alishamalizana na Tundu Lissu tangu akiwa Ulaya na akamalizia na Zitto ambaye hata hivyo ni mtu wake aliyemuandaa tangu wanaanzisha chama cha ACT WAZALENDO.

Yaani jamaa ameshatoa pesa ya kutosha na amewahakikishia kuwa wakimsimamisha yeye gharama zote za kampeni anazibeba mwenyewe na atachangia mzigo wa kutosha kwenye chama.

Kwa hiyo hii maana yake upinzani unakwenda kumsimamisha mwana CCM majeruhi ili agombee kiti cha Urais kama walivyofanya 2015 kumweka Edward Ngoyai Lowassa ambaye baadaye amerejea chamani kwake.

Ndio maana nasema huu ni utoto wa hali ya juu na ni muendelezo wa viongozi wa vyama vya upinzani Tanzania kujali matumbo yao badala ya kusimamia yale wanayoyaongea kila siku.

Yaani wanataka kumsimamisha Bernard Membe huyuhuyu ambaye walimchafua kwa kupiga mabilioni yaliyotoka kwa Muammar al-Ghaddafi wa Libya kwa ajili ya uwekezaji ambao ungewanufaisha Watanzania wanyonge, huyu huyu Membe anayehusishwa na ufisadi mkubwa akiwa Waziri wa Mambo ya nje.

Wanamtaka Bernard Membe huyu aliyefukuzwa uanachama na CCM juzi tu. Kweli domo la mshenzi likikosa nyama hula nyamafu.

Yaani leo Membe ndio akapambane na Magufuli? Daaaa nimeamini kuiangusha CCM nchi hii ni ndoto za mchana. Nakubaliana na Joshua Nassari kuwa CCM ni li mbuyu likubwa sana kuliko tunavyodhani upinzani.

Sasa masikini Lazaro Nyalandu sijui nae anaujua mchezo huu ama kapigwa daflao bila kujua. Mbowe, Mbowe, Mbowe Mungu anakuona.

Taarifa za uhakika ni kuwa Bernard Membe, Mbowe, Maalim Seif na Zitto Kabwe wamekuwa na vikao vya mara kwa mara kujadili mkakati huu.

Na hivi sasa baada ya kudukuliwa simu, Membe hataki tena mazungumzo ya simu, anakutana na watu uso kwa uso bila kujua kumbe hii imekuwa rahisi zaidi kupata taarifa zake za kila anapokwenda na kila anayekutana nae.

Sema jamaa anaonekana mtu hatari sana, maana bado anakutana na wana CCM tena viongozi ambao bila shaka anapanga nao mikakati hii ya Urais. Kwa sababu wanakutana usiku kwa kificho na anawapa pesa nyingi.

Mimi kinachoniuma ni huu upuuzi ambao vyama vya upinzani vinataka kuurudia tena. Wawaache wenzao ambao wamepambana nao wakati wote wakamchukue majeruhi wa CCM?

Yaani wafanye kama walivyofanya 2015 kumuacha Wilbrod Slaa aliyekuwa na mvuto mkubwa kwa Watanzania na kubadili gia angani kwa kumchukua Edward Lowassa.

Haya wacha tuone, ikiwa tofauti na hivi mtaniambia lakini upuuzi huu umevuja sana na ni aibu kubwa kwa siasa za upinzani Tanzania.

Mzee Kizito

Mkazi wa Mbeya
Mkuu hayo ni majungu unaleta hapa wakati unajua kuwa sio kweli mbona ccm mmekuwa waoga sana kwa Lissu na CDM?
 
Back
Top Bottom