Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT, mkishindwa kuwa kitu kimoja na kuachiana majimbo mtawafaidisha CCM

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Sijui nini kinaendelea kati ya CHADEMA na ACT juu ya kushirikiana katika uchaguzi mkuu wa baadae mwaka huu, ila napenda tu kuwatahadharisha kuwa wakishindwa kukaa pamoja na kuja na mpango mkakati wa pamoja juu ya namna bora ya kushirikiana katika uchaguzi huu,basi watakaofaidika na hali hii watakuwa ni CCM katika baadhi ya maeneo ambayo ACT watakuwa na nguvu na CHADEMA nao pia watakuwa na nguvu hata kama watakuwa wanazidiana kwa kiasi fulani.

Zanzibar
Huko ni bora CHADEMA wawaunge mkono ACT kwasababu ujio wa Maalim Seif umeipa nguvu ACT hivyo ni bora CHADEMA wawaunge mkono kuliko kugombea alafu wagawane kura ingawa hata pasipo kuungana, bado ACT itashinda kulinganisha na CHADEMA. Tutambue kuwa adui yetu mkubwa wa kisiasa ni CCM na si chama kingine chochote kile cha siasa.

1593976527170.png


1593973560248.png


kigoma
Katika mikoa ambayo ACT na CHADEMA wanaweza kugawana kura na matokeo yakawa ni wote kukosa kama siyo kupunguza majimbo ya kwenda upinzani,basi Kigoma inaweza kuwa ni mojawapo, hivyo ni vizuri washirikiane katika kusimamisha wagombea kwa maana ya kuachiana majimbo na kata za uchaguzi vinginevyo itakula kwao.

Mikoa ya kusini
Iwapo Membe atajiunga ACT bila kujali atagombea uraisi kupitia ACT au laa,kitendo tu cha Membe kujiunga ACT kitaipa nguvu ACT na kuongeza ushindani wa kisiasa baina ya vyama vitatu:CCM,ACT na CHADEMA.Kwa maana hiyo,wapinzani wakishindwa kuungana,CCM inaweza kufaidika ingawa ACT bado inaweza kushinda hata ikisimama peke yake ila hasara itakuja katika kura za mgombea uraisi iwapo hivi vyama kila kimoja kitasimamisha mgombea wake.

Ukiacha mikoa hiyo niliyoitaja pamoja na Zanzibar,athari za wapinzani kutoachiana majimbo na kata za uchaguzi zinaweza kuonekana pia katika maeneo mengine machache kama kwenye mikoa ya Tabora na Tanga, na lazima ieleweka athari za kugawana kura zitaweza hata kuathiri wagombea uraisi ikitokea kila chama kitasimamisha mgombea wake.

Tanzania kwa ujumla
Iwapo Membe kweli atajiunga ACT kama dalili zinavyoonyesha,basi ni dhahiri Membe atakuja na kundi kubwa la wana-CCM waliko nyuma yake nchi nzima;hivyo, iwapo wapinzani hawataungana na ACT wakamsimamisha Membe kama mgombea wao wa uraisi, hii maana yake ni kuwa wapinzani wanaenda kugawana kura za uraisi na hili litakuwa ni pigo kubwa sana kwa upinzani.

Jambo lingine:hata kama watakuwa wamechelewa kuungana kisheria,swala la wao kushirikiana kwa kuachiana majimbo na kuamua kuwapigia debe wagombea wao haliwezi kuwa ni kosa kisheria zaidi tu ya kuhitaji dhamira ya kisiasa kutoka wahusika.

Ukweli ni kwamba,hata pasipo vyama hivi kuungana,CCM na wagombea wake ndio inayostahili kushika mkia kwenye matokeo ya uchaguzi ila ndio hiyo tena bado kuna baadhi ya watanzania wenzetu hawajielewi.

Muda wa nusu karne na zaidi kama umewashinda kubadili maisha ya watanzania,sioni ni sababu gani ya kuendelea kuwapa nafasi ya kuendelea kubaki madarakani.

CHADEMA mkijiona mna nguvu na mnaweza kusimama kivyenu katika kila sehemu ya nchi hii,basi matokeo yake mtakuja kuyaona;halikadhalika kwa ACT-Wazalendo.

Nukuu muhimu za wanasiasa zinazoendana na mada hii:


Wananchi wa Tanzania wanaotaka mabadiliko hawatatusamehe viongozi wa vyama makini vya upinzani hapa nchini iwapo tutashindwa kuweka maslahi yetu binafsi pembeni na kuunda ushirikiano utakaowaongoza Watanzania kuiondoa CCM madarakani. Wakati ni Huu! Wakati ni Sasa-Ismail Jussa on twitter.

Ni wajibu wetu sote kuonyesha dhamira zenu za kweli kwamba tunahitaji coalition. Wananchi wanafahamu kwamba wapo ambao wqnafanyabiashara katika hizi siasa. Nakubaliana na wewe Kaka Ismail Jussa kwamba hili lazima tusimame na tuhesabiwe-Patrick Ole Sosopi on twitter.

Wananchi wa Tanzania wanaotaka mabadiliko hawatatusamehe viongozi wa vyama makini vya upinzani hapa nchini iwapo tutashindwa kuweka maslahi yetu binafsi pembeni na kuunda ushirikiano utakaowaongoza Watanzania kuiondoa CCM madarakani. Ninaamini TUNAWEZA na TUTAWEZA-Zitto Kabwe on twitter.
 
Huu muungano umeingia shubiri Mara baada ya zitto kumtamani mwanachama Wa ccm aje aokoe jahazi LA kugombea urais kupitia Act kisha muungano huo.Zitto kwa hili kapotoka sana, membe aweza karibishwa upinzani ila sio kwa kugombea urais.
 
Ushauri mzuri. Ngoja tuone sasa kama watakaza shingo zao au wataungana kwa pamoja ili kupigania mabadiliko ya kweli nchini.
Kuungana Ni ndoto, chadema walishaumizwa na lowasa Mwaka 2015, ACT wanatamani wajaribu kuonja sumu kupitia mgombea kutoka ccm aitwaye membe,Leo anaonekana masia.membe Leo anataka tume huru, alikuwa waziri mwandamizi kwa jk alishindwa hats mshawishi jk kupeleka mswada bungeni.duh huu unafiki huu sio sawa
 
Wanatakiwa wasivurugane tu

Ova
Hawatabiriki hawa jamaa,mfano huko Zanzibar Maalim Seif ana nguvu nilitegemea wangeungana huko kumuunga mkono Maalim badala yake kila chama kitasimamisha mgombea mwishowe watagawana kura na CUF (Ccm B) huku mgombea wa CCM akitumia huo mwanya kujinufaisha.
 
Huwa sisomi sana nyuzi zako lakini kwa hili nakuunga mkono. Kuna mijitu io CDM bado inaamini wao wanaimarika kuliko wakati wowote ilhali ni mbaya kupita maelezo. Mtu kama Yeriko Nyerere hataki muungano wa CDN na ACT kwa kuwa tu ana ugomvi na Zitto sasa watu kama hawa hawafai hata kuwasikiliza. Leo nakubaliana na wewe mkuu.
Kuhusu suala la Zitto kumchukua Membe, mimi nasema tatizo ni Lissu. Laiti kama Lissu angekuwa na uhakika wa kuja Tanzania na kugombea kwa tiketi ya CHADEMA nna uhakika Zitto ataachana na huo mpango wa kumchukua Membe.
Zitto yupo tayari kushirikiana na CHADEMA lakini wakati huo huo nae awe anajenga chama chake hivyo si kosa yeye kumchukua Membe ni kutaka kuongeza uungwaji mkono wa chama chake.
LISSU AWE NA UHAKIKA WA KUJA KUGOMBEA KWA TIKETI YA UPINZANI NNA UHAKIKA ZITTO ATAACHANA NA MEMBE.
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom