CHADEMA na ACT kama wajenzi wa Mnara wa Babeli, Zitto asema Magufuli si Dikteta 'Uchwara'

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau, amani iwe kwenu.

Ni dhahiri sasa wapinzani wamechanganyikiwa. Wanaweweseka na hawana msimamo wa pamoja. Kwata za Rais Magufuli zimetifua bongo zao na sasa hawajui nini wanakisimamia.

Msimamo wa CHADEMA ni kwamba Rais Magufuli si Dikteta bali ni Dikteta Uchwara. Tena wameenda mbali na kuanzisha harakati za kupambana na Udikteta wa Rais Magufuli kwa kaulimbiu ya UKUTA.

Zitto Kabwe leo anaibuka na kumpinga mwasisi wa Udikteta Uchwara, Tundu Antipas Lissu. Zitto anasema kuwa Rais Magufuli si Dikteta na wala si Dikteta Uchwara bali anasema ni Dikteta Mamboleo. Anamlinganisha Rais Magufuli na Vladmir Puttin wa Russia.

Sasa hawa wapinzani vepeeeeeee! Mbona wamekuwa kama wajenzi wa mnara wa Babeli? Soon utasikia wanakuja na swaga mpya. Yetu macho.

Hapa Kazi Tu imewatifulia vumbi na matope

Msome hapa Zitto Kabwe kama alivyoandika kwenye ukurasa wake wa Twitter
image.jpg
 
Hiyo kauli inapply more kwa serikali/chama tawala kuliko upinzani.Nyie ndo mnajenga babel tower.
Mara ngapi tumesikia viongozi mbali mbali wakisema kitu halafu baadae wakaja kukanusha au kusema vingine.Mara ngapi tumuona Rais akisema kitu halafu waziri au kiongozi mwingine anakuja kukikanusha au kurekebisha alichosema Rais.
Yaani serikali iko out of sync na taasisi, idara na wizara zake.Wote hawana sauti moja, kila mtu anakuja kusema au kuelezea kitu anavyojua yeye.
 
downloadfile-2.jpeg

usicheze na hii kitu hapo juu tayari baada
ya prof kutimuliwa na mkakati umebaki huko dikotide.


swissme
 
hahahaha ili ni pigo kwa mifugo ya TANAPA na mgonjwa Tundu lissu
 
Sioni kama kuna mahali Zito amepingana na kauli ya CDM/UKAWA.

CDM - JPM ni DIKTETA UCHWARA
ZITO - JPM ni DIKTETA MAMBOLEO

Sioni tofauti ni kubadili jina tu.

Nguruwe - Kitimoto
 
Sioni kama kuna mahali Zito amepingana na kauli ya CDM/UKAWA.

CDM - JPM ni DIKTETA UCHWARA
ZITO - JPM ni DIKTETA MAMBOLEO

Sioni tofauti ni kubadili jina tu.

Nguruwe - Kitimoto
Hahahahahaaaaaaa! Mmevurugwa ninyi. Kwani huwa hamshauriani kabla ya kutoa matamko? Yupi yupo sahihi baina ya Zitto na Lissu?
 
Huyu Lizzy Hajasikia Jinsi Mitandao Ya Kijamii Inavyompelekesha Mtumishi?
Hahahahahaaaaa! Mitandao ipi inampelekesha Rais? Kama mnaendelea kuandika uzushi na uongo je sasa kuna faida gani ya kuwa na mitandao ya kijamii?
 
Hiyo ni Facebook... Twitter Maneno mengi hivo?

Anewei naona umepumua

Interesting!
 
Back
Top Bottom