'CHADEMA Mwanza' watoa Tamko kuyapinga maamuzi ya Kamati Kuu dhidi ya kina Zitto


D

Democrat7

Member
Joined
Nov 26, 2013
Messages
33
Likes
1
Points
15
D

Democrat7

Member
Joined Nov 26, 2013
33 1 15
TAMKO LA UMOJA WA MATAWI YA WANACHADEMA MKOA WA MWANZA DHIDI YA UAMUZI HARAMU

WA KAMATI KUU YA CHADEMA.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTANGULIZI

Ndugu wanahabari, mbele yenu ni muunganiko wa wawakilishi wa matawi 189 ya chama cha demokrasia na maendeleo mkoa wa mwanza. Umoja huu wa matawi unawajumuisha wajumbe kutoka majimbo yote ya mkoa wa mwanza.

Hivyo katika kikao chetu tulichoketi tarehe 30.nov 2013 kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa tisa kasorobo, pamoja na mambo mengine tumeazimia kuanzisha umoja huu wa wanachama.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba viongozi wetu wanaotuwakilisha kwenye vikao vya maamuzi kama vile wilaya, mkoa na


taifa wamekuwa waoga na wameshindwa kuwakilisha mawazo yetu tuliyowatuma badala yake wengi wao wamekubali kuwa vibaraka wa kile kinachoitwa CHADEMA KASKAZ

Kutokana na ukweli kwamba msingi wa chama chetu na chama kingine chochote kile cha siasa, uimara na uhai wake unatokana na uwepo wa misingi na matawi ya chama, hivyo sisi wanachama wa matawi haya 189 tumeamua kuunganisha nguvu zetu kutetea chama chetu na kuhakikisha haki, heshima, katiba na maadili ya chama vinafuatwa bila ya kuogopana wala kuoneana haya.

Umoja huu umeonelea ni vema kuutaarifu umma wa watanzania na wapenzi na wanachama wa chadema mambo kadhaa yafuatayo

Kwamba:-

Chadema ni chama cha siasa kinachopaswa kuendeshwa kwa misingi ya kufuata taratibu, kanuni na katiba yake na si vinginevyo. Lakini badala yake kwasasa kumeibuka ombwe kubwa kwa viongozi wetu wa juu kujitwalia mamlaka ya chama kinyume na matakwa ya katiba ya chama chetu hususan katika kutoa haki sawa kwa viongozi na wanachama wa chama chetu. Kumekuwepo na upendeleo wa hali ya juu sana kwa wale wanao amini kuwa ndani ya chama hawawaungi mkono hivyo kupelekea kuwaadhibu kama ndio kinga yao ya kuendelea kuongoza bila kuhojiwa au kukosolewa.

Sababu zilizotolewa na kamati kuu hazikubaliki

Maamuzi ya kamati kuu ya tarehe 20-21 /11/2013 ya kuwavua uongozi Mh: Zitto Zuberi Kabwe,Dr. Kitila Mkumbo na Ndg Samson Mwigamba, kumeonyesha dhahiri si woga tu wa Demokrasia bali ni unafki na Uzandiki wa hali ya juu sana kwa viongozi wetu kuikwepa Demokrasia kwa kisingizio cha kusaliti na uhaini ndani ya chama. Katiba yetu imeweka wazi Ibara ya 6 Kifungu cha 3 kipengele cha 6. (a – f) Mamlaka za nidhamu na uwajibishaji ndani ya chama. Kulikuwa na haraka gani ya kufanya maamuzi bila kufuata taratibu hizi kwa viongozi hawa, tuonavyo sisi baadhi ya wanachama huo ni umangi meza na udhalilishaji wa kibaguzi ndani ya chama kwa viongozi wetu waliotumia nguvu zao na akili nyingi sana kukijenga chama.

Sababu kubwa ya kuandamwa kwa viongozi hawa ni


  1. Kutaka kujua mapato na matumizi ya fedha za chama zinazotokana na Ruzuku ya fedha za serikali.
  2. Michango ya wanachama na wapenzi kwenye mikutano ya wazi.
  3. Harambee za M4C Mwanza, Arusha na Dar es saalam.
  4. Kutaka kujua taratibu za manunuzi ya rasilimali ya chama namna walivyopatikana wadhabuni wa kusambaza bendera na kadi za chama, magari na pikipiki ambapo ununuzi wake ni wa mashaka makubwa.
  5. Kutaka kuona usawa wa kimadaraka kwa viongozi wote bila ubaguzi wa aina yoyote kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa kinyume na ilivyo sasa hasa makao makuu ya chama ambapo ukanda na ubaguzi wa hali ya juu umetawala.

Kushamiri kwa migogoro

Mwenyekiti na katibu mkuu wameshindwa kutatua migogoro ya viongozi na wanachama kutoka mikoani kwa njia sahihi za vikao na kwa wakati hivyo kutoa mwanya kwa viongozi na wanachama kutumia njia ya mitandao ya kijamii tukiongozwa na katibu mkuu mwenyewe, kujitokeza mara kwa mara kwenye mitandao hiyo hiyo kwa madai ya kutolea ufafanuzi ya mambo mbalimbali ya husuyo maswala ya chama ilihali akijua kufanya hivyo ni usaliti mkubwa kwa chama chake, njia hiyo ya nje ya vikao ilipelekea migogoro mikubwa sana hususan mkoa wetu wa Mwanza na kupelekea kupoteza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutokana na kufukuzwa kwa baadhi ya madiwani, kuvunjwa uongozi wa mkoa na wabunge kuwa juu ya chama na kutumia nafasi zao kuopanga safu za uongozi wanao uwona watawatumikia wao na si chama, hivyo kusababisha mifarakano mikubwa ndani ya chama na kupelekea kuvuliwa uongozi kwa viongozi mbalimbali katika mkoa wetu kwa maamuzi yasiyo zingatia utafiti na uhalisia wa kweli ndani ya chama.

Mwenyekiti na katibu mkuu wamekuwa vinara wa kuvunja katiba Mfano:


  • Kitendo cha kutoa muongozo nje na matakwa ya katiba juu ya kuwapata wawakilishi kwenye vyombo vya maamuzi kama wabunge kwamba wanaohitaji kugombea 2015 waandike barua makao makuu na wao ndio watatoa wagombea kinyume na katiba ya chama Ibara 7.2.13 inayotoa taratibu ya kuwapata wagombea, huwo ni uvunjaji wa katiba na ubakaji wa demekrasia ndani ya chama, sizani kama kuna uhaini zaidi ya huu swali la kujiuliza hapa, Je, kama leo sisi Chadema hatuheshimu katiba yetu tuliyoitunga sisi wenyewe itakuwaje siku tukikabidhiwa nchi yenye watu wenye mawazo na mtizamo tofauti na sisi?. Hatutaki kuamini kama nchi hii inaweza kugeuka uwanja wa maopambano ya kivita.

Tunataka kujua hatua gani zilizochukualiwa dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini Mh: Godbless Lema kumkashfu kiongozi wa chama Mh: Zitto Zuberi Kabwe kuwa ni mnafki na Mzandiki kwendye mitandao ya kijamii pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa na chama dhidi ya Bw Henry Kilewo kwa kuweka waraka unaoitwa ripoti ya siri inayomhusu Zitto mbao chama makao makuu kupitia kwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama kukana mbele ya vyombo vya habari kuwa waraka huo chama hakiusiki nao na hakiujui kabisa lakini chakushangaza Bw Kilewo ambaye pia ni kiongozi wa chama ngazi ya mkoa wa Kinondoni kichama, waraka huo ambao chama kiliukana yeye aliweka kwenye Blog yake ilihali akijua kufanya hivyo ni kinyume na kanuni za viongozi wa chama kuhusu maadili ya viongozi kanuni ya 10.

Pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa kwa waandaaji wa tamthilia hii ijulikanayo kama Ripoti ya siri kuhusu Zitto kwasababu tayari makada na viongozi wetu wamelidhihiri kuwa wao ndo miongoni mwa waandaaji wa tamthilia hii.

Lakini cha ajabu viongozi wetu wamelifumbia macho na kupelekea kwetu baadhi ya wanachama kuamini zengwe hili la kumchafua Zitto Lina Baraka zote za viongozi wa chama ngazi ya juu.

Tunataka kuona nguvu iliyotumika kuwaadhibu Mh: Zitto na wenzake kwa kuandaa waraka ujulikanao kama mkakati wa mabadiliko 2013 nguvu hiyo hiyo itumike kwa hawa waliotumia njia chafu ya kuandaa waraka wa kumchafua zitto ambao chama kinawajua na baadhi yao tumewaweka humu kwenye tamko letu.

Kingine tunataka kwa mara nyingine kwa viongozi wa chama makao makuu kuwaambia umma wa watanzania ni kwanini waraka huo huo uinaoitwa warajka wa siri kuhusu Zitto leo viongozi na wanachama mikoani na kwenye majimbo waraka huo uangawiwa kwa wanachama na wananchi kwa agizo la makao makuu kama si ubaguzi ni nini?.

Tunaonya na kulaani kitendo cha viongozi wetu kuendeleza utawala wa kibabe na kupelekea kuhatarisha maisha ya baadhi ya wanachama na viongozi wanaotofautiana nao kimtizamo mfano: kumezuka tabia ya baadhi ya viongozi na makada wa chama chetu wasiokuwa na uwezo wa kujenga hoja jukwaani hivyo kujikuta muda mwingi wa kutumia maneno ya uchochezi dhidi ya wanachama na viongozi wanaokinzana nao kifikra na kimtizamo na kuhamasisha wanachama wasiojua itikadi vizuri ya chama kuwa wawashughulikie na maneno haya yamekuwa yakisemwa hadharani kwenye mikutano mbalimbali hivyo wananchi wapenda Demokrasia ya kweli kubaki na maswali magumu kuliko majibu juu ya ukimya wa serikali kuhusiana na jambo hili.

Hitimisho

Mwekiti na katibu mkuu wajiudhuru mara moja ili kupisha uchunguzi wa mapato na matumizi ya fedha za chama ambazo zinatokana na kodi za wavuja jasho wan chi hii, M/kiti na katibu mkuu watoe ufafanuzi juu ya kuvunja katiba kwa kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya chama kutangaza uchaguzi huku mkiwaondoa washindani wenu ni uwoga na ubakaji wa Demokrasia.

Mwisho tunataka maamuzi haya HARAMU kamati kuu yabatilishwe na mchakato wa kuwavua viongozi hawa nyazifa zao ufuate taratibu na kanuni kwa mujibu wa katiba tofauti na hapo tarehe 4/12/2013 tutaungana na wapigania Demokrasia kote nchini kufanya maandamano yasiyokuwa na ukomo mpaka uongozi uliopo utoke madarakani.

Vile vile baada ya tarehe hiyo muhakikishe mnawaamisha wabunge vibaraka wote wa chadema mkoa wa mwanza, wamchukue wenje wakamtafutie jimbo moshi na highness kiwia wamtafutie jimbo HAI na MACHAME hii ardhi ya kanda ya ziwa sio saizi yao na tunataka waondoke mara moja. Kinyume na hapo tutawaondoa huku wakishuhudia kwa macho yao.

Tunamuagiza mbowe na slaa wasithubutu kukanyaga ardhi hii ya kanda ya ziwa ikiwa bado hawajajiudhuru ama kubadili maamuzi yao HARAMU haraka iwezekanavyo

Hatuna sababu ya kuendelea kuwa wsatumwa wa fikra ndani ya chama chetu,

Tumekuwa wanyonge kwenye chama hiki vya kutosha, tumedharirishwa kwenye chama hiki vya kutosha, tumeburuzwa na kupuuza kwenye chama hiki vya kutosha,

Sasa sisi wanachadema wa matawi ya mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla, tunasema kwamba kanda ya ziwa na magharibi watupo chadema kwa bahati mbaya, tupo humu kama wapokezi na waasisi wakuu wa chama hiki, tunajivunia uasisi wa wazee wetu kina Marehemu Bob Nyanga Makani, Marehemu Balozi ngaiza Marehemu Chacha Zakayo Wangwe, kamanda Zitto Kabwe na sisi wengine wengi.

Vyovyote itakavyokuwa kamwe, hatutaweza kukubali aina yoyote ya upuuzi huu unaoeneawa na kusimamiwa na WAHUJUMU DEMOKRASIA NDANI YA CHADEMA.

Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Mapambano yanaendelea. CHADEMA VEMA

ROBERT E. GWANCHELE

Mwenyekiti wa umoja wa Matawi ya CHADEMA mkoa wa MWANZA

Mwenyekiti wa Vijana KANDA YA CHAMA ZIWA MAGHARIBI

Mjumbe kamati Tendaji wilaya ILEMELA

0757 084776Source: Tamko la Umoja wa Matawi ya WanaCHADEMA Mwanza juu ya uamuzi wa Kamati Kuu - wavuti.com
 
Crashwise

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Messages
22,181
Likes
894
Points
280
Crashwise

Crashwise

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2007
22,181 894 280
jana nilisema bado 44.. bilashaka baada ya huyu watakuwa wamebaki 43..timua vishetani vyote
 
H

Haki sawa

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2007
Messages
4,701
Likes
569
Points
280
H

Haki sawa

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2007
4,701 569 280
Hivyo vyeo ni feki hazipo kwenye mfumo wa Chadema , ni tamko feki na huyu ni mwana CCM kama mtakumbuka alifukuzwa mwaka 2011 , leo anajipa vyeo ,a
 
B

bujash

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2013
Messages
3,471
Likes
2
Points
0
B

bujash

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2013
3,471 2 0
Upumbafu mtupu! hakuna kitu kama hicho mwanza,asikimbie awaambie huo mkutano ulifanyika katika ukumbi upi? GAMBA @WORK
 
Bramo

Bramo

JF Bronze Member
Joined
Oct 21, 2009
Messages
10,053
Likes
3,246
Points
280
Bramo

Bramo

JF Bronze Member
Joined Oct 21, 2009
10,053 3,246 280
Mtandao wa MM unazidi kupukutika Maskini ya Mungu
 
Njilembera

Njilembera

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2008
Messages
1,448
Likes
183
Points
160
Njilembera

Njilembera

JF-Expert Member
Joined May 10, 2008
1,448 183 160
Makubwa! Imekuwaje tena! Who is financing all these? Am sure it can be prohibitively expensive to organise 189 branches to a meeting to agree on such an item. And I can imagine each branch will have rallied and chosen at least two representatives to get into the 'regional or zonal' meeting.

Lakini je mbona sababu zinazotolewa ni tofauti na zile Zito walizokubali kwenye KK, kwa nini wana-matawi hawa wasingezingatia zile taarifa rasmi zilizotolewa na KK, au wanaamini KK wanafanya kazi kwa kificho. Kuna shughulinzito hapa.
 
samirnasri

samirnasri

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
1,387
Likes
9
Points
135
samirnasri

samirnasri

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
1,387 9 135
ni mwendelezo ule ule wa ccm kutumia pesa nyingi kutengeneza propaganda maana wanaona hii ndiyo nafasi pekee ya kuimaliza chadema ila wanapaswa kjua kwamba wanatwanga maji kwenye kinu. Chademahaitakufa
 
KakaJambazi

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2009
Messages
16,216
Likes
4,560
Points
280
KakaJambazi

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2009
16,216 4,560 280
Kipindi cha kutoa matamko na kuonekana kwenye tv hichi.
 
king kan

king kan

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Messages
1,380
Likes
945
Points
280
king kan

king kan

JF-Expert Member
Joined May 6, 2011
1,380 945 280
jana nilisema bado 44.. bilashaka baada ya huyu watakuwa wamebaki 43..timua vishetani vyote
Kaka inaonekana unaunderestimate ukweli, Wanachama wengi kutoka pande mbalimbali za nchi tunaamini Mh. Zitto kaonewa kwa sababu mpaka sasa hoja mahsusi hazijawahi kujibiwa kilichopo ni character assassination na kwa hili lazima haki itendeke. Hatuwezi kukubali mumchafue Zitto kwa mambo ya kipuuzi. Na kwa hili hata tuitwe wasaliti haturudi nyuma mpaka haki itakapotendeka.
 
Last edited by a moderator:
Ruttashobolwa

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Messages
45,873
Likes
16,331
Points
280
Ruttashobolwa

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Joined Feb 22, 2012
45,873 16,331 280
KUMEKUCHA
NILISEMA TOKA MWANZO ALICHO KIANZISHA Godbless J Lema KITAIZIKA CHADEMA.

SASA CHADEMA NI VIPANDE VIPANDE. KUNAENDELEA KUKUCHA KABISA NA BADO.

NI KWELI WAWAKILISHI WENU HASA WAKINA WENJE NA MWENZIE WAMEKUWA VIBARAKA WA KUNDI LA MBOWE NA SLAA.

NI WAZI HAKUNA MWENYE UTIMAMU WA AKILI ATA SHANGILIA MAAMUZI YA KIJUHA YA KAMATI KUU YA CHADEMA.

HONGERENI SANA KWA KUFUNGUKA NA BILA SHA CHADEMA KESHO WATAITISHA PRESS CONFERENCE KUWAJIBU.

SASA HIVI NI ZAMU YA DR SLAA KUTOA PRESS CONFERENCE
MWAKA HUU MTAJUTA.
UKWELI TUMEUPATA.

CC Kurugenzi ya Habari Dr.W.Slaa, Henry Kilewo, sixgates Mungi Ritz, CHAMVIGA.
 
Last edited by a moderator:
H

Haki sawa

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2007
Messages
4,701
Likes
569
Points
280
H

Haki sawa

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2007
4,701 569 280
Utashangaa kesho story hii I kapewa uzito na magazeti na hasa Mwananchi kuwa front page wakati wanajua kabisa hawa ni magamba at work
 
AdvocateFi

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Messages
11,185
Likes
1,232
Points
280
AdvocateFi

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2012
11,185 1,232 280
Huu ni mchezo mchafu wa akina Adamu Chagulani na Henri, huu ni ushetani na uharamia wa kujivika uchadema na kufanya uibilisi na uharamu kama huu! Hakuna umoja wa wanamatawi hata siku moja bali huu ni muendelezo wa magenge ya CCM kwa kupitia wachumia tumbo kama chagulani...

Ujinga huu haukubaliki.
 
Ulukolokwitanga

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2010
Messages
8,418
Likes
3,933
Points
280
Ulukolokwitanga

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2010
8,418 3,933 280
Hii move ya kumvua uanachama Muua Panya itasaidia sana kujua nani wako kwenye mapambano na nani ni wasindikizaji na Baraka wa Magamba. Pepeta pepeta hii itaicha CHADEMA ikiwa safi kabisa na wapambanaji walio tayari kuitoa CCM 2015 huku makapi yote nje
 
Taswira

Taswira

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2012
Messages
1,198
Likes
12
Points
0
Age
28
Taswira

Taswira

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2012
1,198 12 0
TAMKO LA UMOJA WA MATAWI YA WANACHADEMA MKOA WA MWANZA DHIDI YA UAMUZI HARAMU WA KAMATI KUU YA CHADEMA.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTANGULIZI

Ndugu wanahabari, mbele yenu ni muunganiko wa wawakilishi wa matawi 189 ya chama cha demokrasia na maendeleo mkoa wa mwanza. Umoja huu wa matawi unawajumuisha wajumbe kutoka majimbo yote ya mkoa wa mwanza.
 
New Force 2015

New Force 2015

Member
Joined
Oct 25, 2013
Messages
63
Likes
2
Points
15
New Force 2015

New Force 2015

Member
Joined Oct 25, 2013
63 2 15
Unajisikiaje kutuletea tamko la Mchange, Chagulani, na kundi la kina Mwampamba? mbinu zote zimeshavuja, we hamia CCM ukawe kibaraka kunyonya watu kizazi hata kizazi. Wenzako walipewa kazi tangu wakiwa Dar wakaingia Serena na sasa wanakula bata kumsaidia Zitto kutoa matamko na kuongea na Waandishi kabla hajapeleka lead stori kwenye Mwananchi. Wewe unapata nini huko Mwanza. Tamko unatoa peke yako, aibu tupu tumikia Ma CCM upate chakula cha jioni
View attachment 124224
 
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Messages
18,936
Likes
1,600
Points
280
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2013
18,936 1,600 280
Hiki chama kinamapepo sasa lazima watagawana mbao si mda mrefu.
 

Forum statistics

Threads 1,252,121
Members 481,988
Posts 29,796,704