CHADEMA MUST now Reform and Restructure!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Ili Chadema kiweze kuwa Chama mbadala, kinahitaji major overhaul ya kiuongozi na utendaji. Matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010, yamoenyesha wazi kuwa safari ya Chadema kuinga Ikulu na kushika hatamu ya kuongoza Tanzania ama ni ya kufikirika sana au ni mdadi ambao umejaa kwenye mioyo ya watu na wapenzi wa Chadema lakini hawaelewi kwa undani ni namna gani ya kujikit ndani ya mfumo wa siasa.

Sitarudia sana nilichosema kenye zile mada nilizoichambua Chadema kabla ya uchaguzi, lakini kama wana masikio safari hii na ni wasikivu mpaka ndani ya mioyo yao, basi wafanyie kazi sasa hivi mapendekezo ya Mchungaji.

La Kwanza, Mwenyekiti wa Chadema na Uongozi wote wa Chadema unahitaji kubadilishwa. Freeman Mbowe ajiuzulu Uenyekiti na focus yake iwe Bungeni na si kwingine.

Pamoja na hili la Freeman kujiuzulu, aidha Wabunge wote wa Chadema wajivue majukumu ya kuongoza Chama kama Watendaji wa Chama na nafasi ndani ya Chama na wawekeze nguvu zao ndani ya Bunge na kuachia safu mpya ya Uongozi wa Chama.

Freeman, kama mwenyekiti, hakuweza kukijenga Chama kikawa imara ipaswavyo na hata kukiandaa kikamilifu kwa ajili ya Uchaguzi Mkuuu huu uliopita. Freeman bado hajawa Mwanasiasa mwenye mvuto na uwezo wa kufikisha ujumbe wa kuuza Itikadi na Sera za Chadema kikamilifu kwa Watanzania. Atafaa sana kwenye utendaji wa Kiserikali Bungeni na itambidi aachie Uenyekiti kama ana ndoto ya kuona Chadema inapewa dhamana ya kuongoza nchi.

Binafsi, ningependelea Dr. Slaa awe Mwenyekiti wa Chadema na asiwe mbunge au kuwa na kazi ingine yeyote bali kukijenga upya Chama. Tumeona ni jinsi gani alivyo na uwezo wa kuvuta watu na akipewa nafasi hii na nyenzo za kutosha, anaweza kukijenga Chama kikawa imara sana na hata kuongeza wigo wa kuuzika kwa Chadema mpaka kila kona ya Tanzania.

Sambamba na Dr. Slaa kama Mwenyekiti, Chadema na Dr. Slaa vinanahitaji mtu mwenye uwezo kama Willy Lwakatare kama Katibu Mkuu kuratibu shughuli za Chama na kusaidiana katika kukijenga na kukiongoza Chama.

Hawa wawili wakipata mtu mwenye ushawishi na nguvu kama Makamu kutoka Zanzibar, watakuwa na uwezo wa kuwekeza nguvu za kukijega upya Chadema mithili ya Mzee Malecela na Mangulla walivyofanya kazi pamoja ya kukiimarisha CCM na kuchukua TAMISEMI 2004 na kuleta Tsunami ya 2005.

Pamoja na kubadilisha safu ya uongozi na hata kuubadili mfumo wa kiuongozina kiutendaji, Chadema inapaswa kupitia upya Sera na Itikadi zake kwa kubainisha na kuyaelewa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Chadema ni lazima kiwe na taswira na mfumo mpya ambao haufanani na CCM, CUF, TLP au NCCR na uwe wenye kujenga demokrasia ya kweli kwa kutumia sauti za wanachama na kuwaelewa Watanzania na mahitaji yao. CCM wamejifunza makosa ya kutokusikiliza maamuzi ya wanachama wake katika ngazi za majimbo wakati wa kura za maoni na ndio maana KInana leo analalamika na anasahau ni wao katika ngazi ya Taifa waliamua kubadilisha zile sauti za wanachama wake.

Pili, katika kujijenga upya huku kwa Chadema, ni lazima kijijenge kikamilifu katika maeneo yote ya Tanzania na hasa Zanzibar. Sijali watakaodai kuwa mbona CUF kiko Zanzibar pekee, bali ni lazima Chadema kiwekeze nguvu kubwa sana kupata uhalali na kukubalika Zanzibar kama kinadiriki kuongoza Serikali ya Muungano na si Tanganyika pekee.

Aidha katika tathmini ya uchaguzi wa mwaka huu, Chadema kianze leo hii kujijengea mazingira mazuri ya kushinda tena majimbo yote waliyoshinda mwaka huu, waanze kujenga mazingira ya kujijenga kichama na wanachama wenye uwezo wa kuweza kusimama na kugombea katika chaguzi wa TAMISEMI 2014 kwa kuhakikisha wanakuwa na watu wenye uwezo wa kushinda Udiwani na kuwa na uwakilishi wa kutosha katika Serikali za mitaa na mikoa.

Chadema ni lazima kifanye tathmini ya udhaifu wa kiutendaji na kiuongozi ambao kulikifikisha Chama ama kukosa wagombea au watendaji na pia kukosa kuungwa mkono kwa kutosha na Wananchi hasa vijijini.

Hii ina maana kuwa Chadema ni lazima ijisuke upya katika kila kata, tarafa, wilaya na hata mkoa na kuhakikisha kuwa kina jenga ushawishi wa kukubalika leo na si kungojea kesho kutwa!

Pamoja na jitihada za kujikita Zanzibar, Chadema inahitaji kuwekeza nguvu kubwa kwenye maeneo mengine ya Tanzana bara ambayo kura zao zilikuwa dhaifu mno. Mikoa kama Mtwara, Lindi, Ruvuma, Dodoma, Singida, Morogoro, Tabora, Shinyanga, Kigoma, Rukwa, Mbeya, Tanga na Pwani, iwe ni mijini au vijijini, ni lazima kijijenge upya na kwa haraka sana na si kusubiri 2015 na kuuza hoja ambazo hazieleweki sawasawa kwa Watanzania. Pia itakuwa muhimu kwa Chadema kuwekeza katika ujenzi wa ofisi kuu katika kila Wilaya na Mkoa.

Tatu, ujumbe wa Chadema uwe ni kuleta mabadiliko kwa Tanzania. Kipaumbele kiwe kwenye kuondoa Umasikini, Ujinga, Maradhi nakupunguza deni la Taifa. Bungeni, kina Mbowe, Mnyika, Zitto, Shibuda waungane na wenzao wa CUF, NCCR na TLP kujenga vyema upinzani wa kuiratibu Serikali hata kama idadi yao ya kura ni ndogo. Wote wawe na ushirikiano kwa ajili yamanufaa ya Watanzania na si kujitenga kwa manufaa ya kichama kama CCM.

Dr. Slaa, Lwakatare na wengine kwenye safu ya uongozi wa kichama, kazi yao iwe kunadi Itikadi na Sera za Chadema, kuelimisha Wananchi kwa nini Chadema ni chama bora na kitafanya nini kwa Watanzania. Pamoja na kujiuza kisera na kiitikadi, Uongozi mpya uwe mstari wa mbele kwenye suala la kudai Katiba mpya na Tume mpya ya uchaguzi. Hili liwe ni shinikizo la kuanza siku Kikwete anaapishwa kuwa Rais na si kusubiri 2014.

Nne, umoja ni nguvu, utengano ni dhaifu, sasa ni wakati muafaka wa Chadema kukaa chini tena na Vyama vingine vya upinzani na kuanza kujisuka ama viungane au viwe na makubaliano ya kweli ya kuwawezesha kuiangusha CCM ambayo itarudi kwa nia ya kujisahihisha katika kipindi cha miaka hii mitano inayokuja, pamoja na kuwa na mvutano wa ndani kwa ndani wa madaraka na uongozi.

Ukifanya tathmini ya matokeo ya uchaguzi wa 2010, kwa haraka haraka kuna majimbo karibu 15 ambayo yangeweza kwenda kwenye upande wa upinzani kama kungekuwa na ushirikiano na muafaka wa kugawanyana na kuachiana majimbo ili kupunguza nguvu za CCM Bungeni kwanza. Lakini kutokana na kila Chama kutaka kushika hatamu na kufanya mambo dakika za mwisho, CCM imepata ushindi wa kubahatisha kutokana na kura kugawanyika.

Tano, Dr. Slaa pamoja na kazi yake hii mpya ninayoshauri, yeye na timu yake itabidi waanze kazi ya kujisuka kwa ajili ya Chaguzi zinazokuja kwa kuhamasisha kupata wanachama zaidi, kuhakikisha wanachama wao wanajiandikisha kupiga kura na kutoa elimu ya Uraia kwa Wanachama wake ili uchaguzi mkuu utakapofika, wanachama na wapenzi wa Chadema wawe tayari.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na kile kitabu cha CIA, takriban asilimia 43 ya Watanzania ni chini ya miaka 14. Kati yao kundi hili, 30% watakuwa ni wapiga kura wapya 2015, hivyo Chadema ilenge kujijenga kwa Chipukizi na vijana ambao leo hii wana umri kati ya miaka 13 hadi 17 kwa kuwahamasisha kupitia elimu ya Uraia na kuwafundisha Sera na Itikadi za Chadema.

Aidha kwa kuwa kuna muelekeo wa Chadema kuwa na ufuasi mkubwa wa walioko vyuoni, basi hawa walio wasomi watumike ipaswavyo kukijenga Chadema katika majimbo yao, mitaa yao na mpaka kwenye kata kwa kuwafikia Watanzania naa kusaidiana na Dr. Slaa kukijenga Chadema na kunadi Sera an Ilani zake.

Kama Chadema watakuwa wasikivu na kufanyia kazi mapendekezo ya waliokishauri awali na hata sasa, watakuwa na nafasi nzuri ya kuongeza nguvu zao Bungeni hata kupita lengo lao la viti 70 bungeni ambalo hawakulifikia mwaka huu.

Uamuzi ni wao kujiimarisha na kujijenga upya, lakini wakae macho wakitambua kuwa CUF kinashika moto na matokeo ya muafaka Zanzibar, yataleta ushindani mkubwa kwenye Muungano na kuwa CCM sasa inajipanga kwa haraka mno kuhakikisha kuwa kinajisafisha na ikiwezekana kushinda kwa 90% hapo 2015.
 
Mchungaji;


CHADEMA kilizaliwa, wakati huo kwa msukumo wa mwanzilishi au waanzilishi wachache waliojaliwa busara na hekima tele! Mungu awabariki!

Hakuna aliyekijua CHADEMA kama kinavyojulikana sasa, Kimekuwa na kutawanyika .. kikondani ya fikra na mioyo ya mamilioni ya Watanzania na si ndani ya fikra na mioyo ya kundi la waasisi wake! Sio cha kundi dogo la uasisi wake ni ... CHAMA CHA WATANZANIA WOTE! NI CHAMA CHA WATU! Karibu kila Mtanzania mwema anajisikia ni chake na anajisikia hivyo kwa moyo wa ukweli kabisa.!

Kwa hiyo lazima kiwashirikishe na kuwajumuisha watanzania wote tofauti na kilipoanzishwa kwa maana kiukweli ni chao! Mahitaji na muundo wakati wa uchanga wake na sasa wakati kinaedelea kukomaa ni tofauti. Kwa sasa kitakuwa na MAHITAJI NA MUUNDO tofauti na ule wa enzi za uasisi!

Kipepeo anayeruka angani kwanza alikuwa yai akapitia ngazi ya lava akawa buu na hatimaye buu kuanguliwa na kuwa kipepeo...! Hatua zote hizo ni tofauti sana na zina mahitaji na muundo tofauti kabisa..lakini yote hayo ni Kipepeo tu!! Yaani NI CHADEMA YETU!!

CHADEMA imekomaa katika ngazi fulani sasa LAZIMA IZALIWE UPYA kuhimili mahitaji ya mamilioni ya Watanzania. Kwa hali ilivyo Sina shaka hata CCM ...hawatabakia kama walivyo!!
 
REv.Kishoka,
Tumejifunza nini kutokana na uchaguzi huu uliopita?..
Tatizo la siasa za Tanzania sio Upinzani bali ni chama tawala. Chadema wajipange vyovyote vile hawataweza kuleta mageuzi ya kweli ikiwa system inakitambua chama kimoja tu nacho ni CCM.
 
REv.Kishoka,
Tumejifunza nini kutokana na uchaguzi huu uliopita?..
Tatizo la siasa za Tanzania sio Upinzani bali ni chama tawala. Chadema wajipange vyovyote vile hawataweza kuleta mageuzi ya kweli ikiwa system inakitambua chama kimoja tu nacho ni CCM.

...Chama kimoja cha upinzani kitakapokuwa na wabunge kama 100 wa kuchaguliwa, system zote zitakitambua.
...It's about representing a larger part of Tanzania.
 
...Chama kimoja cha upinzani kitakapokuwa na wabunge kama 100 wa kuchaguliwa, system zote zitakitambua.
...It's about representing a larger part of Tanzania.
Utawapata vipi hao wabunge ikiwa uchakachuaji upo? hivi husomi yaliyotokea Zanzibar miaka yote iliyopita? Amini maneno yangu kwa mfumo huu uliopo Chadema or any opposition party will never gain 100 seat bungeni - NEVER!
 
Utawapata vipi hao wabunge ikiwa uchakachuaji upo? hivi husomi yaliyotokea Zanzibar miaka yote iliyopita? Amini maneno yangu kwa mfumo huu uliopo Chadema or any opposition party will never gain 100 seat bungeni - NEVER!

...Omba uzima, uje shuhudia siku moja.

...Nadhani ulikuwa makini kwenye somo la history darasani, hasa juu ya empires na kingdoms.
 
Chadema tunajipanga upya.. Ni wazi tunahitaji mageuzi ila siyo makubwa sana.

ila Tujipange kuanzaia matawi hadi taifa..
 
Bila katiba mpya na watu kubadili fikra zao hatuwezi kuwa na serikali ya chama zaidi ya CCM.

...Makosa makubwa ya msingi ndio yanahitajika kufanywa.

...Unakumbuka kifo cha KANU kilivyotokea?

...Kura ya maoni ilivyofanywa CCM, ni moja ya kosa la msingi.
 
...Makosa makubwa ya msingi ndio yanahitajika kufanywa.

...Unakumbuka kifo cha KANU kilivyotokea?

...Kura ya maoni ilivyofanywa CCM, ni moja ya kosa la msingi.
Mkuu wangu CCM haikushindwa kwa sababu ya kura za maoni isipokuwa wameshindwa kwa sababu Dr.Slaa na Chadema wameweza kuuza sera zao. Kama sikosei wengi walioshindwa majimbo yao walipita kura za maoni pia ktk kura za maoni na wapo wabunge wapya wameingia kutokana na kuchakachua.

Kifupi ni kwamba Chadema pamoja na nguvu yote waliyoifanya wamekuja pigwa na Vyombo vya haki... maadam sheria haifuatwi hata tukifanya nini, tubadilishe katiba na kadhalika hilo halkiwezi kuwa dawa til sisi wenyewe tumebalika. Ule utamaduni wa Fisadi kuitwa shujaa, kingozi anayeiba na kujienge mazingira na maisha mazuri ndiye mjanja na mwenye kuthaminiwa unategema haki itoke wapi?. Nambie mkuu wangu tumejionea kina Malecela, Sitta wakitupwa na wananchi wote wamefurahia lakini tumeshindwa kuuliza ujio wa kina Chenge na Lowassa, unategemea mabadiliko yapi kama hawa watu ndio wanaheshimiwa zaidi..
 
NATEGEMEA CDM IFANYE YA FUATAYO
1.katiba kuandikwa upya
2.UWT kuundwa upya
3.TAKUKURU KUVUNJWA NA KUUNDWA CHOMBO KINGINE
4.TUME YAUCHAGUZI ITAVUNJWA NA KUUNDA NYINGINE
5.TUME HURU ITAUNDWA KUCHNGUZA MWENENDO WA UCHAGUZI IKIBAINIKA KUCHEZEWA UCHAGUZI MWINGINE UTAITISHWA
 
Mkuu wangu CCM haikushindwa kwa sababu ya kura za maoni isipokuwa wameshindwa kwa sababu Dr.Slaa na Chadema wameweza kuuza sera zao. Kama sikosei wengi walioshindwa majimbo yao walipita kura za maoni pia ktk kura za maoni na wapo wabunge wapya wameingia kutokana na kuchakachua.

Kifupi ni kwamba Chadema pamoja na nguvu yote waliyoifanya wamekuja pigwa na Vyombo vya haki... maadam sheria haifuatwi hata tukifanya nini, tubadilishe katiba na kadhalika hilo halkiwezi kuwa dawa til sisi wenyewe tumebalika. Ule utamaduni wa Fisadi kuitwa shujaa, kingozi anayeiba na kujienge mazingira na maisha mazuri ndiye mjanja na mwenye kuthaminiwa unategema haki itoke wapi?. Nambie mkuu wangu tumejionea kina Malecela, Sitta wakitupwa na wananchi wote wamefurahia lakini tumeshindwa kuuliza ujio wa kina Chenge na Lowassa, unategemea mabadiliko yapi kama hawa watu ndio wanaheshimiwa zaidi..

...Kosa jingine la msingi ni ufisadi/mafisadi kusifiwa, kutetewa na kulegezewa kamba.

...And believe me, sera pekee hazitoshi kuwabadilisha mawazo na kuwafumbua macho watanzania, and that was the case.

...Kama nilivyokwishasema awali, we have a lot to learn, from history.
 
...Kosa jingine la msingi ni ufisadi/mafisadi kusifiwa, kutetewa na kulegezewa kamba.

...And believe me, sera pekee hazitoshi kuwabadilisha mawazo na kuwafumbua macho watanzania, and that was the case.

...Kama nilivyokwishasema awali, we have a lot to learn, from history.
Habari ndio hiyo, kujifunza kutorudia makosa kutokana na what U have learned ndio kuelimika, lakini sisi bado kabisa hatuelimiki kwa sababu hatuamini what we have learned -sijui kama umenipata!
 
naunga mkono hoja!!!!!!!!!
Dr. Slaa anamvuto sana kwa wananchi, achukue uenyekiti sasa. na safu ya uongozi ibadilishwe, ili wawepo viongozi wasio gombea majimboni
Mbowe apambane bungeni akisaidiana na wabunge wengine
 
Habari ndio hiyo, kujifunza kutorudia makosa kutokana na what U have learned ndio kuelimika, lakini sisi bado kabisa hatuelimiki kwa sababu hatuamini what we have learned -sijui kama umenipata!

...Kabisaaa!

...Ndio maana mbunge hafanyi lolote kwa maendeleo ya wananchi jimboni, lakini anachaguliwa kwa kishindo kila msimu.

...But this is changing, slowly.
 
Nadhani chini ya uongozi wa sasa wa chadema ndio tumepata haya mafanikio tunayofurahia. wananchi walifurahishwa sa sera za chadema. Nilidhani tungejenga kuboresha na kuendeleza haya. Ni vizuri pia ukajaribu kutafakari impact ya hiyo overhaul. Isijekuwa Nia yako ni kuimaliza chadema
 
Freeman, kama mwenyekiti, hakuweza kukijenga Chama kikawa imara ipaswavyo na hata kukiandaa kikamilifu kwa ajili ya Uchaguzi Mkuuu huu uliopita. Freeman bado hajawa Mwanasiasa mwenye mvuto na uwezo wa kufikisha ujumbe wa kuuza Itikadi na Sera za Chadema kikamilifu kwa Watanzania. Atafaa sana kwenye utendaji wa Kiserikali Bungeni na itambidi aachie Uenyekiti kama ana ndoto ya kuona Chadema inapewa dhamana ya kuongoza nchi.
La muhimu ni kuwa Chadema wawe ni mfano kwa matendo yao................ni rahisi kuongelea kuibadilisha katiba ya Tanzania ukiwa bado upo nje ya madaraka lakini ni suala jingine kuibadilisha ukiwa ndani ...............................

Ili watanzania wawaelewe Chadema yabidi waanzie kurekebisha katiba ya chama chao iachane kuwa kile ambacho JK amekuwa akiwabughudhi nachoo kuwa ni "fotokopi" ya CCM..................

watenganishe kofia za kazi za chama na za serikali ndani ya Chadema..............................Let us preach water and drink water but not wine......................
 
Mchungaji ana ushauri mzuri lakini kuna vitu anavisema kama ni uamuzi na siyo ushauri. Mfano anaposema Mbowe ajitoe kwa sababu hana mvuto naona anapotoka. Kila kitu kinapoanza kina ugumu wake maana hata aliyegundua ndege aliteseka sana alipoanza kuirusha na hasa wakati wa kutua. Kiushauri yapo mambo mengi ya kufanya lakini badala ya kuongelea mvuto wa mtu ni vizuri kushauri kurekebisha katiba ya Chama ili kuwe na democracia ya uchaguzi kwa ngazi zote. Chadema ni kama familia inayokuwa na hivyo mahitaji nayo yanaongezeka hivyo mipango yake ili ifanikiwe inahitaji umakini zaidi. Napenda kuona kila mtu anathaminiwa kutokana na mchango wake kuanzia viongozi,waasisi na hata wanachama na wasio wanachama walioshiriki kwa namna tofauti na si vinginevyo
 
Rev. Kishoka ume andika mambo mengi ya ushauri kwa CDM kutokana na mtazamo wako lakini sio utafiti/research na omba ni toe angalizo chama hiki kime pitia uongozi wa Mzee Mtei, Mzee Bob Makani na sasa Mbowe unaweza uka angalia ni wkatigani chama hiki kimeonekana na mtazamo wakitaifa zaidi na kuku balika kwa watu wengi zaidi.Hivyo kusema mbowe hafai kuwa mwenyekiti wa chama hiki eti hana mvuto nisigefurahi kabisa kuona zina rudiwa rudiwa na wana jamvi.Tatizo sio mbowe na wala sio chadema na wala sio upinzani tujaribu kuwa scientific na realistic ni kitu gani ambacho mbowe kafanya hadi umeona anakiangusha chama,hakika huna jambo lolote la msingi juu ya hilo na unatoa ushauri kabisa kwamba aondoke madarakani ampishe Dr. Slaa kwa uchaguzi upi? Kumbuka hiki nichama cha demokrasia kama kinavyo jipambanua.Acheni kabisa kutoa ushauri usio nautafiti kabisa kwani huu ni upotoshaji.

Unasema CDM iungane na vyama vingine kama CUF hivi nikweli unashauri kwania njema au una mpango gani Mchungaji,hawa CUF mkono wakulia ni CCM mkono wa kushoto ni wapinzani labda Mchungaji ndoa ya CCM na CUF huitambui, vyama vya namna hii huwezi kushirikiana kwasababu hawa eleweki na mtazamo wao hautabiliki.

Hawa wengine kama TLP unajua kabisa ni matawi ya CCM, mwenyekiti wake msimamo wake umesha onekana kweli CDM tunahitaji kufanya kazi na vyama vya namana hii,NCCR mageuzi nao ni wale wale kutwa wako mahakamani na vitisho kwa CDM hivi tuungane tunavyo taka kufanya nini hapo sija kuelewa.au mchungaji unataka vyama viungane halafu viitwe vimeungana kwa hiyo vina umoja, huo umoja kwa ajili ya kufanya nini? mara ngapi CDM haijaweka mgombe uraisi na kime waunga mkono hao unaotaka leo wa ungane nao nini kimetokea baada ya hapo? majibu utakuwa nayo mchungaji

Mchungaji una shauri chama kiwe na mshina toka kijijini hadi mkoani hivyo umeona kama hiyo ndio njia pekee yakuondoa ufisadi katika nchi hii? umefanya utafiti liability ya kumaintain huo mfumo?au una shauri bila kuwa na scietific research! Unafikiri kuondoa ufisadi nchi hii ina hitaji chama chenye wanachama wangapi? jaribuni kuwa logical jamani CCM ina wanachama wangapi naime pata kura ngapi pamoja na uporaji wa waziwazi ulio fanyika na tume au huelewi kilicho tokea?

Angalieni mnapo toa ushauri base yenu nini hasa!acheni kupotosha uma Please! huna utafiti unatoa ushauri wakubadirisha uongozi wa CDM baada yakuona nini eti kiongozi hana mvuto samahani mchungaji naomba nikukosoe mvuto hapo hapo anatafutwa mchumba hapo? tunahitaji uwezo wakuleta mabadiliko maisha yetu yawe safi.Nyie hamueleweki kwakuangalia sura ndio mnasema kiongozi mzuri mwaka 2005 wengine walisema eti mgombea wa chama fulani nichaguo la mungu leo wako wapi uliza kama wanajibu au watarudia tena kauli zile.

Nakataa kabisa ushauri wako
 
Back
Top Bottom