KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 696
Muundo wa CCM ni matokeo ya legacy ya utawala wa chama kimoja na mfumo wa kikomunisti wa chama kushika hatamu, ambapo chama kinakuwa juu ya serikali. Kwa hiyo chama, ili kudhibiti mwenendo wa serikali yake, kinajitanua na kuwa virtual state ambayo inafika kila mahali serikali inapofikia. Katika mazingira ya sasa hakuna chama chochote kitakachoweza kuiga hali hiyo. Hata CCM huo mnaouita mtandao uta-collapse siku watakapoondoka madarakani. Mtandao uta-collapse immediately. Hilo ndo limetokea kwa nchi zote za kiafrika zilizokuwa na mfumo wa chama kimoja.
Kuishauri Chadema kujenga mtandao wa kiCCM hadi vijijini, ni kuishauri Chadema ijiue kabla ya kufika popote. Mfumo huo wa mtandao mpana hauigiki na hautekelezeki. Mojawapo ya nightmare kubwa ya CCM leo, ni huo mtandao. Kusema ukweli huo mtandao ndo unaoiua CCM kwani kutokana na ugumu wa kuuunganisha na kuratibu shughuli zake, mapambano ya ndani kwa ndani ya mtandao ndo chanzo kikubwa cha kufa kwa vyama vya aina ya CCM. Vyama ndani ya chama vinakuwa vingi mno. Unahitaji viongozi wa aina ya Mwalimu kuiweka CCM hai kwa muda mrefu. In absence of that, Nikuhakikishie, CCM haiwezi kuendelea na muundo huo katika next 15 years na ikaendelea kutwaa madaraka.
Back to Chadema. Huwezi kutenganisha mafanikio ya Chadema ya sasa na uongozi uliopo madarakani. Halafu haya mawazo kuwa kiongozi akishaonekana star basi apewe uenyekiti siamini kama ni mawazo ya kimageuzi badala ya mawazo ya kimgando mgando, au ki CCM CCM. Jamani, Chama kinahitaji viongozi mahiri at all levels. Kila kiongozi ana karama na vipaji tofauti tofauti. Kiongozi kung'ara mahali au kwenye post fulani, ina maana kiongozi huyo anaimudu nafasi yake na yuko mahali sahihi. Sasa kumuona kiongozi kang'ara kwenye urais, unataka umpe uenyekiti wa chama. Hii ni harufu ya Chama kushika hatamu, kwamba kiongozi akishakuwa kwenye position ya kuchukua madaraka ya nchi, basi huyo huyo akabidhiwe na uenyekiti wa chama. Sikubaliani na hili. Slaa amekuwa mzuri sana kama katibu mkuu na naamini anafanya kazi nzuri sana kama katibu mkuu. Katibu mkuu ndo mtendaji, kwa hiyo ni nafasi inayohitaji mtu ambaye ni technocrat. Slaa ame-prove kuwa anaimudu hiyo nafasi, tena akipewa urais, atakuwa rais bora, rais mtendaji si rais wa kuagiza na kuomba mambo yafanyike!
Huwa najitahidi sana kukwepa kujadili majina ya watu, but katika mada hii mchungaji kanikoroga zaidi kwa kujadili watu. Chadema under Mbowe imekuwa fluid na very focused vile vile kimekuwa more strategic kiasi cha kushinda majimbo ambayo tunaweza kuyaita uti wa mgongo. Kwa nini tunarudha lawama zisizokuwa na msingi kwa Mbowe? 2005 Mbowe alisimama kama mgombea urais, kwa mara ya kwanza Chadema kilionekana katika stage ile na kupata kura kama alizopata Lipumba mwaka huu. Alichofanya mbowe ilikuwa ni u-pioneer, alisafisha njia. Tuliona creativity ya helkopta ilivyo-shake-up siasa za Tanzania. Pamoja na nguvu ya matumaini makubwa waliyokuwa nayo watanzania juu ya Kikwete kutokana na utawala uliopita wa Mkapa kuanza kuboa, bado Mbowe alifanya monumental task. Ni kazi hiyo iliyoanzisha hiki tunachokishuhudia leo kuwa wote tunakubali kuwa Slaa aliibiwa kura (ingawa bado hatujapata ushahidi kamili kutoka Chadema). Hatuwezi kuyatenganisha mafanikio hayo na Mbowe kama mwenyekiti wa Chama na Kama mgombea wa urais wa mwaka 2005. Momentum yake ndo tunayoiona leo.
Kwa ujumla, kuishauri timu inayoonesha mafanikio makubwa, ingawa ni gradual, eti ifanye major overhaul ni kutoelewa. Chadema ifanye major overhaul ili ipate nini? Tunataka waendelee kuwa focused. Leadership iliyopo ni competent engough. Mawakala wa mabadiliko wayapeleke mawazo yao kwa CCM. Mawakala wa mageuzi, tunataka Chadema hii hii iendelee na mbinu na mikakati hiyo hiyo. Wabunge 23, mwaka 2015, wakifika zaidi ya mia, CCM imekwisha!