CHADEMA muacheni Lowassa apumzike, uchokonozi utawaponza

Naona umehama kumshabikia Dk Slaa umehamia kwa Lowasa,hivi Josephine kwanini huridhiki?
 
Wakuu,

Chadema kati ya mambo yanayosikitisha ni kutojifunza kupitia makosa wanayofanya. Wanapokosea zinatumika nguvu nyingi kuhalalisha makosa yao na kugeuza wakosoaji wao wenye nia njema maadui.

Mlipoingia kwenye mgogoro na Dr Slaa mwezi july 2015 mlianza kumchokonoa kwa kila namna kila mahali wakati Dr Slaa kwa heshima aliamua kukaa kimya. Baada ya miezi miwili ya propaganda ikalazimika Dr Slaa afunge mjadala kwa pigo la karne pale Serena.

Sasa mnaanza kufanya yale yale kwa Lowasa. Tunaona wanachama wenu maarufu na wabunge wanachofanya mitandaoni. Mnasahau mnadeal na mtu ambaye anakijua chama chenu kabla hata wengine hamjajua siasa ni mdudu gani.

Chadema narudia tena kuwaasa, wekeni utaratibu wa chama kutoa matamko na misimamo. Katibu mkuu Mashinji ameshaongea na kutoa msimamo tena kwa weledi mkubwa. Lakini akina Lema na wengine wameshaanza kuropoka na kukejeli kwa mtu ambaye hamjui anajua nini!

Msipojidhibiti mkaendelea na hizo kejeli mnataka kujikuta mnaingia kwenye vita na vijana wake ambao mnajua kazi yao kwenye propaganda. Mtajikuta badala ya kujenga chama kuelekea uchaguzi mkuu mnawekwa kwenye kona ya kujibu tuhuma muda wote.

Hili la EL mliingia cha kike kubalini makosa msonge mbele na msianze kazi ya kumchafua mtu ambaye mlimchafua wenyewe na kisha mkamsafisha! Hamuwezi tena kumchafua zaidi ya nyie kuabika zaidi.

Muacheni Lowasa apumzike na nyie jipangeni namna ya kukihuisha upya chama chenu ambacho kwasasa kimejaa ukakasi mbele ya wananchi ambao nyie ndio mlikuwa tumaini lao pekee.

Mkishupaza shingo muda utaongea!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wew endelea kusherehekea fisad papa limesema limerudi kwa mafisad wenzake ccm lijinga kwel limejichokea kama chama chakavu kilivyojichokea na kubak na usaidiz wa Police.
 
Kweli ni vizuri kumuacha apumzike kwa amani. Sio kuendelea kumsemasema.
 
Ushauri Mzuri Mkuu, ingawa hukuwahi kuwapa CCM wakati wanamkejeli..
Makonda, Polepole, Msukuma..nk Walivuka mipaka Walitukana kabisa..
Jiwe angepata heshima kubwa sana kama angetupilia mbali Maombi ya EL kurejea CCM ..
Chadema haijaathiriwa kuondoka kwa EL ila CCM ndiyo wanaaminisha hivyo..
Kuondoka kwa Dr. Slaa Kuliathiri CDM lakini si EL..
2020
Hivi ninyi wadudu mna matatizo gani? Hata mkishauriwa bado mnakuja na kejeli za kipuuzi
 
Wapi nimetoa Kejeli! Zaidi ya wewe kuniita Mdudu..
Jiwe alitakiwa aonyeshe kwa Vitendo anapambana na Ufisadi,
Angefyekelea mbali Ujio wa EL ningemuamini..
Mwenyekiti kashamkubali Kazi imebaki kwenu Kumtawaza
 
Hakuna mtu anaweza kutoa siri za baraza la mawaziri hata kama ni Mbowe. Ukishakuwa waziri mkuu unabanwa na kiapo hadi kifo. Hiyo ni tofauti na Chadema, anaweza kusema lolote na si lazima aseme yeye!

Mtatafutana, hamjui kwenye siasa partners hufanya nini! Umeshaona Mbowe na Dr Slaa wakishambuliana? Mashabiki tusiojua lolote ndio wanaumizana kwa matusi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unapoteza muda wako,hawa SACCOS hawasikia maoni ya wengine hawana tofauti na wafuasi wa Kibwetere
 
Wakuu,

Chadema kati ya mambo yanayosikitisha ni kutojifunza kupitia makosa wanayofanya. Wanapokosea zinatumika nguvu nyingi kuhalalisha makosa yao na kugeuza wakosoaji wao wenye nia njema maadui.

Mlipoingia kwenye mgogoro na Dr Slaa mwezi july 2015 mlianza kumchokonoa kwa kila namna kila mahali wakati Dr Slaa kwa heshima aliamua kukaa kimya. Baada ya miezi miwili ya propaganda ikalazimika Dr Slaa afunge mjadala kwa pigo la karne pale Serena.

Sasa mnaanza kufanya yale yale kwa Lowasa. Tunaona wanachama wenu maarufu na wabunge wanachofanya mitandaoni. Mnasahau mnadeal na mtu ambaye anakijua chama chenu kabla hata wengine hamjajua siasa ni mdudu gani.

Chadema narudia tena kuwaasa, wekeni utaratibu wa chama kutoa matamko na misimamo. Katibu mkuu Mashinji ameshaongea na kutoa msimamo tena kwa weledi mkubwa. Lakini akina Lema na wengine wameshaanza kuropoka na kukejeli kwa mtu ambaye hamjui anajua nini!

Msipojidhibiti mkaendelea na hizo kejeli mnataka kujikuta mnaingia kwenye vita na vijana wake ambao mnajua kazi yao kwenye propaganda. Mtajikuta badala ya kujenga chama kuelekea uchaguzi mkuu mnawekwa kwenye kona ya kujibu tuhuma muda wote.

Hili la EL mliingia cha kike kubalini makosa msonge mbele na msianze kazi ya kumchafua mtu ambaye mlimchafua wenyewe na kisha mkamsafisha! Hamuwezi tena kumchafua zaidi ya nyie kuabika zaidi.

Muacheni Lowasa apumzike na nyie jipangeni namna ya kukihuisha upya chama chenu ambacho kwasasa kimejaa ukakasi mbele ya wananchi ambao nyie ndio mlikuwa tumaini lao pekee.

Mkishupaza shingo muda utaongea!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa Fredoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri Mzuri Mkuu, ingawa hukuwahi kuwapa CCM wakati wanamkejeli..
Makonda, Polepole, Msukuma..nk Walivuka mipaka Walitukana kabisa..
Jiwe angepata heshima kubwa sana kama angetupilia mbali Maombi ya EL kurejea CCM ..
Chadema haijaathiriwa kuondoka kwa EL ila CCM ndiyo wanaaminisha hivyo..
Kuondoka kwa Dr. Slaa Kuliathiri CDM lakini si EL..
2020
Kwani Edo alituma maombia yakurejea Ccm?Hata kama angetuma kweli Jpm hana ubavu wakumbania Edo Kurudi Ccm.Anajua umuhimu wa Edo kurudi Ccm.In short Ccm ilimuhitaji zaidi Edo kuliko Edo kuhitaji Ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapotumia neno "Mlisema" unamaanisha nini!? Ni wapi niliposema hayo uliyoainisha hapo juu!? Hao waliosema ni kina nani?
Naona nafsi inakusuta kwa kumpokea EL. Endeleeni kutoa matamko ya kumpongeza ili wenye akili tuendelee kuwa-enjoy maccm
 
Nasikia Polepole kapata mgao toka kwa EL. Mbele ya shekeli Polepole mpole kabisa! Natamani kumsikia Polepole akiuhabarisha umma kumpokea 'fisadi' aliyekuwa anajengewa mahakama. Kwa hiyo ujenzi wa mahakama ya mafisadi umesitishwa?
 
Mbona haikua Demokrasia alipohamia CDM!!
Mkuu hakuna athari yoyote, Muda utasema 😂
Naona nafsi zao zinawasuta hasa wakikumbuka mitusi waliyomtukana alipohamia Chadema hadi wakaanza kumjengea mahakama ya mafisadi.
 
  • Thanks
Reactions: prs
Back
Top Bottom