Chadema mtoto habembelezwi kwa nyimbo mbaya!!

Tunayoipenda nchi tumeshukuru yale yote mabaya mliosema yatatokea hayakutokea na Mungu atatuepushi leo na siku za usoni Amin.
We unaipinda nchi au anafurahia kula na kunywa vinono chini ya kivuli cha utawala wa ndugu zako mafisada aka magamba!!??? Lipi la maana uliloifanyia nchi hii hata useme unaipenda zaidi ya kushirikiana na magamba wenzio kuifisadi?? Kwa mawazo hayo akili yako kama jojo tu!!
 
Great Thinkers,

Habari zenu na ni matumaini mu wazima wa afya na wale wanaumwa ni mategemeo yangu watajaaliwa afya na siha njema na Mwenyezimungu.

Tangu kukamatwa kwa viongozi wa chama kikuu cha "upinzani" kumetolewa kauli nyingi sana hapa jamvini na wapenda "chama" na nyingi ya kauli hizo ni za kuvuruga amani na utulivu zenye lengo la kuchochea machafuko na umwagaji damu! Bila kujielewa au kwa kuelewa wengi wamediriki hata kusema "watapindua" nchi na ndio uhuru wa kweli utapatikana! Nimejiuliza watu wenye kuweza kupindua nchi lazima watakuwa na majeshi yao sitaki kuamini kuna jeshi zaidi ya jeshi la ulinzi na usalama la Tanzania. Tumekuwa tukisikia watu wakipewa vyeo vya "kamanda" na "mpiganaji" nadhani hatuhitaji kupigana tunataka maendeleo yatakayo leta tija kwetu na kwa vizazi vijavyo.

Ndugu yangu Waberoya ameelezea nini kile wananchi wanacho kitaka katikama thread yake https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-maslahi-ya-taifa-they-are-just-another-tool japo wengi wenu mmeona kama ni kejeli kwa sababu hoja zake ni za kujenga na nyie sera yenu ni ya kubomoa na kuleta chuki na mifarakano wengi wenu hamkuipokea wala kuitafakari. Sisi tunahitaji utaifa kwanza! tunataka Tanzania iwe nchi yenye kutawalika! tunataka watoto wetu waje kuiridhi nchi ikiwa kwenye hali ya kutawalika!

Imefikia wakati napata wakati mgumu sana kutofautisha wanachama wa cdm na waumini wasabato masalia. Kuna fikra zenu na mawazo mnayoyatoa humu jamvini ni ya kufikirika zaidi kama yale ya kusafiri bila ya passport wala visa!

Nafasi mnayo ya kujenga Tanzania msije mkaandika historia ambayo itakuja kuwa chungu kwetu na kwa vizazi vijavyo. Tujifunze ustaarabu kidogooooo tujaribu kuipenda nchi na si kuwapenda "wapiganani" na vyama. Hii nchi itaendelea kuwepo lakini hawa "wapiganaji na makamanda" pamoja na vyama vyao vitakufa!

Ushauri wangu mdogo sana kwenu mlio na upofu wa kutoona uzuri wa maelewano/mshikamano/uhuru wa kwenda popote ni kuwa kuna nchi zina zilianza chokochoko kama zetu lakini mpaka leo hazitawaliki moja wapo ni Somalia.

Nimesikitishwa na ndugu jangu mmoja ambae ni memba nguli hapa JF kwenye FB status yake amewataadharisha Polisi na wanasiasa "watawala" wawe na busara na kuepusha maafa kwa kinachoweza kutokea kwenye issue ya Mhe Mbowe. Huyu ni mwandishi anatumia fani yake kama mwandishi kujaribu kujenga mazingira kuwa mamlaka ni za kionevu na busara zifanyike. Pengine ataandika makala ya kuelezea uonevu wa mamlaka zilizokuwa zinashughulikia hii issue naamini haitajenga ila kuongeza chuki! Natamani tupate waandishi wenye kujali maslahi ya nchi zaidi kama kuwaonya wawaonye wahusika wote. Mfano amwonye mtu ambae ana kesi aweze kuhudhuria kesi yake yeye au wakili wake kwani kwa kutokufanya hivyo kunaweza kukafanya akamatwe na kuleta machafu anayotaka yazuiwe kwa kukwepa kufata misngi ya sheria.

Najua hampendi kuambiwa ukweli lakini sioni tofauti yenu kifikra na wasabato masalia mnatofautiana kuwa nyie ni wanachama wa chama cha siasa wao ni waumini wa dini.

Ukweli kwako ni kuwa ccm na serikali yake wanafanya vizuri? sijui unatoa wapi muda wakuandika pumba kama hizi... wee ndio mwenye mawazo yakufikirika kama jk wako.
 
Najua huna maana ya kunidhalilisha nadhani jina langu linasomeka vizuri tu unless uwe unasababu zako binafsi za kuandika unavyotaka wewe.

Well maneno yako ni kweli na ndio maana utaona G Lema na girlfired wa Slaa hawakukamatwa na kupelekwa mahakamani japo kuwa na wao hawakuhudhuria mahakani lakini walifuata taratibu za kuwasilisha sababu za kutofika mahakani nasisitiza kwa hili nadhani CDM wameteleza kidogo lakini kuteleza huko haina maana tuhubiri machafuko. Napenda mageuzi lakini sio kwa machafuko ya kijinga kama yanayohubiriwa hapa JF na wapenzi vindakindaki wa CDM. Naomba mnisameh kwa kutokuwa mnafiki kwenu.

Jina lako nimekosea ilikuwa ni typing error tu wala sikumaanisha kingine na nimerekebisha.

Bado haukujibu kwani nini mahakama zetu zinakuwa na double standard zinapokuwa zina-deal na watu wa upinzani tofauti na wanavyo-deal na watu wa pro-ccm wakati sheria ni zile zile!
 
kwa hiyo hao wengine huwa wanakaidi amri ya mahakama?


Hapana sijasema kuna wengine wanakaidi amri za mahakama. Nilichotaka kumaanisha ni kuwa kuna na unfair treatment kwa wabunge wa upinzani na wale wa ccm.
 
Na wewe unatumiwa na nani? Slaa au Mbowe? Rais anawatawala watu wa dini zote kwahiyo wala sioni ajabu kwa JK kuhudhuria uapishwaji wa maaskofu au kusaidia kujenga sekondari za makanisa kwani hata Mhe Mkapa aliwapa Waislam majengo ya chuo cha Tanesco na kuyafanya chuo kikuu cha kwanza cha kiislam Tanzania na akabakia na dini yake anayoiamini.

Turudi kwenye mada hapa tunazungumzia nyie mashabiki/wanachama wa cdm na kauli zenu za kichochezi je hii ndio taswira ya chama?

Mwandishi Nguli Ngugi wa Thiong'o amepata kusikiaka akisema pale Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kuwa, "Ukitaka kujua nchi itakuwaje kesho basi waangalie vijana wake wa leo" Vijana wa leo wa cdm ambayo kesho wanataka kuchukua nchi wanataka Arusha isikalike wanasema eti leo wataandamana na kuingia bungeni kuchukua viti! Kwahiyo mtaona kesho nchi yetu itakuwaje!
hapo kwenye red good quote but poor analysis

kama tunaamini JK alishinda na wapiga kura wengi ni vijana, basi tunaijua kesho ya tanzania.... corrupt, udini, urongo na unapelization, achilia mbali masharo-uharo!!

but kama unaamini JK hakushinda, then i will buy 50% of your idea

BTW, how much is arusha representing the whole nation?
 
Bwana Mohamed Shossi, huhitaji jeshi kupindua serikali dhalimu, ni nguvu ya umma tu kama Misri na Tunisia. Pili unazungumzia maendeleo, maendeleo yatakuja vipi na utawala huu? Unazungumzia nchi tutayowaachia watoto wetu, ulitaka tuwaachie nchi ambapo majizi machache na watetezi wao kama wewe ndio wananufaika, watoto wetu waendelee kuumia eti kwa kulinda amani na utulivu? Amani na utulivu havina maana kama havijengi mazingira ya kuleta maendeleo kwa watu wengi (si maendeleo kwa mafisadi wachache). Wewe na wenzako mnatumia amani na utulivu kunyamazisha kelele za wanyonge ambao miaka nenda rudi mmekuwa mnaishi kwa jasho lao!
 
Naona thread ndefu lakini sioni point hata moja ambayo ya kuchangia.....zaidi ni yale yale ya siku zote yanajirudia...
 
Jina lako nimekosea ilikuwa ni typing error tu wala sikumaanisha kingine na nimerekebisha.

Bado haukujibu kwani nini mahakama zetu zinakuwa na double standard zinapokuwa zina-deal na watu wa upinzani tofauti na wanavyo-deal na watu wa pro-ccm wakati sheria ni zile zile!

Mkuu sijapingana na hilo la double standard lakini watu makini lazima wacheze karata zao kwa uangalifu ili zisitafutwe sababu za kipuuzi! Leo tumebahatika kuandaa rasimu ya katiba mpya tunaona mambo kama haya kwanini tusiyachukue haya matukio kama reference kubadilisha hii hali? Nadhani wengine hamjui sana siasa za vyama jinsi zilivyo gharimu watu hapa nchi! Kwa taarifa yako tu na wengine Zanzibar ni wahanga wa siasa hizi zinazohubiriwa sasa na cdm. Wananchi walinyanyasika sana kwenye yale mauaji ya 2001 Jan 27 kuna wanaosemekana kubakwa tena mbele ya familia zao! Kuna waliomiminiwa rsasi za moto kama vile wanaopigwa ni swala! kuna waliokimbilia shimoni mombasa na kuomba uhifadhi kama wakimbizi.

Mwaka 1995 baada ya Dr Salmin Amour kushinda kwa hila aliwasweka ndani kina Juma Duni Haji na wenzake 17 kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu na kusema kuwa kesi yao inashughulikiwa walihoji mbona inachukua muda akawajibu kwani wale ni mapapai kusema yataoza? Hivi haya yakiwapata viongozi wa cdm itakuwaje? hivi tu kukamatwa kwa mhe mbowe kumetikisha jf na vijiwe vya umbea!
 
KWANZA NAOMBA NIKUPONGEZI MR SHOSS KWA MAKALA YAKO NZURI YA KUHAMASISHA WATU WIPENDE NCHI YAO. LAKINI Makala yako imekuwa ya upande mmoja zaidi, bila kuhusisha sababu zilizo kuwa zinamfanya mbowe asiende makamani, je? umezipitia sababu zile nakuzipima msingi wake, je kanuni za bunge unazijua zinazo toa maelezo jinsi ya kukamatwa kwa mbunge. unapo jadiri maada usiazie juu wala katikati azia chini from the source, shwala lakuhamasisha watu wandamane ni impact, ya kunyimwa haki kwa baadhi ya watu, na kutokufuta kanuni za bunge zinazo mlinda mbunge,

ASANTE, TUSHILIKIANE PAMOJA KATIKA KUJENGA UCHUMI WA NCHI YETU.
 
Naona thread ndefu lakini sioni point hata moja ambayo ya kuchangia.....zaidi ni yale yale ya siku zote yanajirudia...

Unge save muda wako kuchangia point za maana au na wewe huna point kama mimi?
 
Aisee, Shossi umenimaliza!

Kumbe kuna nyakati watu huwa wapole!

Ukweli daima unasimama!
 
KWANZA NAOMBA NIKUPONGEZI MR SHOSS KWA MAKALA YAKO NZURI YA KUHAMASISHA WATU WIPENDE NCHI YAO. LAKINI Makala yako imekuwa ya upande mmoja zaidi, bila kuhusisha sababu zilizo kuwa zinamfanya mbowe asiende makamani, je? umezipitia sababu zile nakuzipima msingi wake, je kanuni za bunge unazijua zinazo toa maelezo jinsi ya kukamatwa kwa mbunge. unapo jadiri maada usiazie juu wala katikati azia chini from the source, shwala lakuhamasisha watu wandamane ni impact, ya kunyimwa haki kwa baadhi ya watu, na kutokufuta kanuni za bunge zinazo mlinda mbunge,

ASANTE, TUSHILIKIANE PAMOJA KATIKA KUJENGA UCHUMI WA NCHI YETU.

Kama kuna sifa cdm wanastahili basi ni kuweza kufanikisha suala la katiba mpya kuweza kujadiliwa sijali sana kuona hoja yao imetekwa na serikali lakini moyoni najua wao ndio waliosimamia hili swala na sasa kuna mwangaza juu ya hili tusubiri tuone. Kwa kutumia fursa hii ni vizuri wananchi pamoja na vyama vya upinzani vikatumia fursa hii kuandaa rasimu itakayo weka uwazi wa sheria hizi ili kama kuna kinga iwe kwa wote na sio sheria za kibaguzi na upendeleo. Tunayo fursa ya kuandika historia nzuri ambayo itakuja kutufanya kuheshimka mbele ya safari NADHANI CDM WANATAKA WAHESHIMIKE KWENYE HISTORIA YA NCHI KUFANYA UKOMBOZI WA KWELI BILA KUWEKA REHANI AMANI YA NCHI.
 
Ni nani asave muda wake kuchangia this crap?

Ajabu na kweli hata kula chakula hakijakushuka kwa kusoma hii crap yangu kwani unalazimishwa kuchangia hii inaonyesha jinsi gani ukweli unavyokuchoma ila tatizo lako wewe ni sawa na wasabato masalia endelea kuwa na fikra za kufikirika its not bad to dream ila have my words kwa mtindo wenu sidhani kama mtafanikiwa kushika nchi time will tell labda mbadilike mfiche hizo true colors zenu.
 
Aisee, Shossi umenimaliza!

Kumbe kuna nyakati watu huwa wapole!

Ukweli daima unasimama!

Cha ajabu wanasema ni crap na kuchangia if its crap why wasting your time kucomment si uende kule kwenye thread za kuwasifu wapambanaji! sijui wanapambana kwa kutumia silaha gani?
 
Mkuu sijapingana na hilo la double standard lakini watu makini lazima wacheze karata zao kwa uangalifu ili zisitafutwe sababu za kipuuzi! Leo tumebahatika kuandaa rasimu ya katiba mpya tunaona mambo kama haya kwanini tusiyachukue haya matukio kama reference kubadilisha hii hali? Nadhani wengine hamjui sana siasa za vyama jinsi zilivyo gharimu watu hapa nchi! Kwa taarifa yako tu na wengine Zanzibar ni wahanga wa siasa hizi zinazohubiriwa sasa na cdm. Wananchi walinyanyasika sana kwenye yale mauaji ya 2001 Jan 27 kuna wanaosemekana kubakwa tena mbele ya familia zao! Kuna waliomiminiwa rsasi za moto kama vile wanaopigwa ni swala! kuna waliokimbilia shimoni mombasa na kuomba uhifadhi kama wakimbizi.

Mwaka 1995 baada ya Dr Salmin Amour kushinda kwa hila aliwasweka ndani kina Juma Duni Haji na wenzake 17 kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu na kusema kuwa kesi yao inashughulikiwa walihoji mbona inachukua muda akawajibu kwani wale ni mapapai kusema yataoza? Hivi haya yakiwapata viongozi wa cdm itakuwaje? hivi tu kukamatwa kwa mhe mbowe kumetikisha jf na vijiwe vya umbea!

Shossi ccm hawawezi kuacha demokrasia na haki kuwepo bila shinikizo ikibidi vita kabisa. Sioni tatizo kama vita itakuwa ndio njia pekee ya kuwalazimisha ccm wawahudumie wananchi na sio viongozi. Ni bora tupigane vita kabisa kuliko hali ilivyo sasa.
 
Mwanzisha thread anataka kutuletea text-book approach kwenye mambo ya ukombozi.
Hizi ni taarabu za miaka nenda rudi ambazo 5 decades post-independence bado tunapiga mark time!!

Sidhani kama anayatambua matatizo ya sisi wa-TZ kwa mapana (bigger picture view). Sidhani!
Inabidi watu tusome vizuri historia ya akina Mandela kwa ajili ya kupata darasa. Inabidi!

Inabidi tufike mahali ninyi manojiita "wasomi" muondoe huo ukungu wa vitabu machoni na kwenye bongo zenu ili muweze kuiona na kuijjua hali halisi. Inabidi!

"Msomi" akikaa kwenye kijiofisi chenye AC, akaendesha ki-prado chake na kujenga kijumba pale Segerea anajiona basi kafika - this is pathetically myopic!!

Cut that "tusubiri mchakato wa katiba" crap. Cut all that bullshit and be practical!!

At least for a change since the Patels, the Dewji's, the RACHEL's started ripping us off, we have people who are saying "enough is enough".

Mbowe & co are on the right track. They need support ya "great thinkers" na si vinginevyo.

Wake up "wasomi"!
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
NDG YANGU SHOSSI, SOMA ALAMA ZA WAKATI, PIA REJEA SIASA ZA NCHI YETU,HIVI VYUO VIKUU VYOTE HIVI WASOMI WAKE UTAWAPELEKA WAPI????? KAMA VIWANDA VYOTE MFILISI,MASHIRIKA YA UMMA YAMETOKOMEZWA, KODI INALIPWA NA WATU WACHACHE HIVI...... I THINK BELOW 20%, RASLIMALI INAKWENDA KWA MIKATABA MIBOVU NAMNA HII, UFISADI KILA MAHALI , NAFIKIRI SASA KUTOKA LEVEL YA KITAIFA KARIBU INAFIKA NGAZI YA FAMILIA, JE NI NINI KITOKEE ILI UPATE KUJUA SYSTEM YA SERKALI YETU IME FAIL??????????? PIA HUONI JINSI WATAWALA WANAVYOWAGAWA WATANZANIA KWA DINI, WENYE NACHO NA WASIOKUWA NACHO,WATAWALA NA WATAWALIWA,etc,etc. HISTORIA YA HAPA KARIBU TU - UNGUJA NAYO HUIJUI???! KURA ZILIPOSHINDWA KULETA MABADILIKO NINI KILITOKEA??????
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Chadema hawalet chuki bali ccm na mambo yao wanayoyafanya mf.mauaj nyamongo,ufisad,matabaka n.k iv we unadhan wananch wa sasa iv ndo wale wa miaka 50 iliyopita hawajui a wala che..yan 2kiandamana kukumbushia ahadi walizotoa eti 2naleta vurugu bwana ee kama mbwai mbwai acha tuuane..by the way kila siku wa2 wanakufa kama sio ajal,kauliwa na polisi malaria..na kila mtu atakufa siku moja acha 2badilishe mapish ili 2tasonga mbele..WE HATA USIOGOPE MUDA UTAFIKA KITAELEWEKA TU.
 
Nadhani unastahili kupongezwa kwa constructive idea ambayo hiki kizazi cha vodafasta hakiwezi kukuelewa.Kila dhama zinamchepuko wake hivyo hizi purukushani zilizopo ni njia tu.Siasa si kwa vijana tu bali ni kina mama,wazee,watu wazima(umri wa kati) pia.Wafuasi wengi wa CDM ata ukiwatizama katika picha ni watu waliokata tamaa kimavazi,kiafya na kifikra pia.Tazama picha ulizoletewa leo toka arusha hawa ndio vijana wa kutuletea ukombozi kama wanavyodai?.

Jiulize mtu aliyekatika shughuli yake hawezi kuacha ama kumuaga mwajiri wake kuwa anakwenda kupigania haki ya mkosefu mahakamani.Hili ni kundi linalodhani CDM ikiingia madarakani ajira nje,chakula bure na mshahara utalipwa hata pasipo kufanya kazi.Nasikitika kwa sababu wengi wao hawatapata hicho wanachokitarajia hata kama CDM itachukua nchi na badala yake kuamia chama kingine huku wakizua machafuko (kenya baada ya KANU).Tuwajenge vijana wetu jinsi ya kukabiliana na maisha pamoja na kushiriki katika shughuli za kiuchumi kwani kwa mihemuko hii bila shughuli yeyote ndani ya miaka mitano watakuwa wamezeeka kimaisha na wengine jela kwa kudokoa vya watu.




Haya Mbowe anaelekea kwake kura kuku na mazagazaga kibao kurudisha afya,wewe kwa kuwa huna chochote wala hukujishughulisha na chochote leo kisa ulikuwa mahakamani hata kipande cha mhogo pale kona huwezi kununua. Inasikitisha sana.

Ndio maana nikamnukuu Mwandishi Nguli Ngugi wa Thiong'o amepata kusikiaka akisema pale Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kuwa, "Ukitaka kujua nchi itakuwaje kesho basi waangalie vijana wake wa leo" Vijana wa leo wa cdm ambayo kesho wanataka kuchukua nchi wanataka Arusha isikalike wanasema eti leo wataandamana na kuingia bungeni kuchukua viti! Kwahiyo mtaona kesho nchi yetu itakuwaje!
 
Back
Top Bottom