Chadema mtoto habembelezwi kwa nyimbo mbaya!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema mtoto habembelezwi kwa nyimbo mbaya!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mohammed Shossi, Jun 6, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Great Thinkers,

  Habari zenu na ni matumaini mu wazima wa afya na wale wanaumwa ni mategemeo yangu watajaaliwa afya na siha njema na Mwenyezimungu.

  Tangu kukamatwa kwa viongozi wa chama kikuu cha "upinzani" kumetolewa kauli nyingi sana hapa jamvini na wapenda "chama" na nyingi ya kauli hizo ni za kuvuruga amani na utulivu zenye lengo la kuchochea machafuko na umwagaji damu! Bila kujielewa au kwa kuelewa wengi wamediriki hata kusema "watapindua" nchi na ndio uhuru wa kweli utapatikana! Nimejiuliza watu wenye kuweza kupindua nchi lazima watakuwa na majeshi yao sitaki kuamini kuna jeshi zaidi ya jeshi la ulinzi na usalama la Tanzania. Tumekuwa tukisikia watu wakipewa vyeo vya "kamanda" na "mpiganaji" nadhani hatuhitaji kupigana tunataka maendeleo yatakayo leta tija kwetu na kwa vizazi vijavyo.

  Ndugu yangu Waberoya ameelezea nini kile wananchi wanacho kitaka katikama thread yake https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/107636-inflammatory-chadema-hawako-kwa-maslahi-ya-taifa-they-are-just-another-tool japo wengi wenu mmeona kama ni kejeli kwa sababu hoja zake ni za kujenga na nyie sera yenu ni ya kubomoa na kuleta chuki na mifarakano wengi wenu hamkuipokea wala kuitafakari. Sisi tunahitaji utaifa kwanza! tunataka Tanzania iwe nchi yenye kutawalika! tunataka watoto wetu waje kuiridhi nchi ikiwa kwenye hali ya kutawalika!

  Imefikia wakati napata wakati mgumu sana kutofautisha wanachama wa cdm na waumini wasabato masalia. Kuna fikra zenu na mawazo mnayoyatoa humu jamvini ni ya kufikirika zaidi kama yale ya kusafiri bila ya passport wala visa!

  Nafasi mnayo ya kujenga Tanzania msije mkaandika historia ambayo itakuja kuwa chungu kwetu na kwa vizazi vijavyo. Tujifunze ustaarabu kidogooooo tujaribu kuipenda nchi na si kuwapenda "wapiganani" na vyama. Hii nchi itaendelea kuwepo lakini hawa "wapiganaji na makamanda" pamoja na vyama vyao vitakufa!

  Ushauri wangu mdogo sana kwenu mlio na upofu wa kutoona uzuri wa maelewano/mshikamano/uhuru wa kwenda popote ni kuwa kuna nchi zina zilianza chokochoko kama zetu lakini mpaka leo hazitawaliki moja wapo ni Somalia.

  Nimesikitishwa na ndugu jangu mmoja ambae ni memba nguli hapa JF kwenye FB status yake amewataadharisha Polisi na wanasiasa "watawala" wawe na busara na kuepusha maafa kwa kinachoweza kutokea kwenye issue ya Mhe Mbowe. Huyu ni mwandishi anatumia fani yake kama mwandishi kujaribu kujenga mazingira kuwa mamlaka ni za kionevu na busara zifanyike. Pengine ataandika makala ya kuelezea uonevu wa mamlaka zilizokuwa zinashughulikia hii issue naamini haitajenga ila kuongeza chuki! Natamani tupate waandishi wenye kujali maslahi ya nchi zaidi kama kuwaonya wawaonye wahusika wote. Mfano amwonye mtu ambae ana kesi aweze kuhudhuria kesi yake yeye au wakili wake kwani kwa kutokufanya hivyo kunaweza kukafanya akamatwe na kuleta machafu anayotaka yazuiwe kwa kukwepa kufata misngi ya sheria.

  Mwandishi Nguli Ngugi wa Thiong'o amepata kusikiaka akisema pale Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kuwa, "Ukitaka kujua nchi itakuwaje kesho basi waangalie vijana wake wa leo" Vijana wa leo wa cdm ambayo kesho wanataka kuchukua nchi wanataka Arusha isikalike wanasema eti leo wataandamana na kuingia bungeni kuchukua viti! Kwahiyo mtaona kesho nchi yetu itakuwaje!


  Najua hampendi kuambiwa ukweli lakini sioni tofauti yenu kifikra na wasabato masalia mnatofautiana kuwa nyie ni wanachama wa chama cha siasa wao ni waumini wa dini.
   
 2. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Tunayoipenda nchi tumeshukuru yale yote mabaya mliosema yatatokea hayakutokea na Mungu atatuepushi leo na siku za usoni Amin.
   
 3. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We ni gamba lisilovulika wala kukwangulika huna la maana.
   
 4. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Mkuu nakupa hongera kwa makala yako. Safi sana. Siku zote tusiwe negative tu, wakati mwengine inatakiwa tuwe positive. Siasa za chuki na ugomvi zimepitwa na wakati. Mungu ibariki TANZANIA.
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  Naona jumatatu ya leo huna kazi ya kufanya, kuna kitabu kizuri hiki hapa jisomee utaelimika

  View attachment 31557
   
 6. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Unaturudisha nyuma magamba mkubwa wewe!!!!crap crap crap crap this!!!!
   
 7. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #7
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Unajua kebehi hata mie nazijua tena zinye kuumiza na kufurahisha kwa wakati huo huo hivi nikuulize wewe unashabikia chuki mwenyekiti wako anapeana mkono na Rais akienda jukwaani anakupika uwe na chuki na aliekuwa akisalimiana nae kwa bashasha unatakiwa hata kama una akili za kushikiza ujitambue. Nadhani kati yangu mimi na wewe ni wewe mwenye magamba tena unagamba ya Mamba!
   
 8. e

  ebrah JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kuongea umeongea lakini huna point, kumbuka historia tulipokuwa tunadai uhuru toka kwa wakoloni, kwanza walikuwapo wachache wenye kuwa na ujasiri wa kufuatilia, waliwashawishi wtz wengine, jaribu kuuliza ni magumu ganii walikutana nayo kabla hujaropoka non sense! na pia wakati huu kumbuka now tunafight against wale wanaotumia migongo ya wanyonge kunufaika, tunaposema nchi isitawalike haina maana vita, nah! we mean mbinu za unyonyaji wanazotumia tuzipinge! upo? fikiri kabla hujaongea!
   
 9. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #9
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Hiyo attachement yako inahusiana nini na mada? jaribu kuficha upumbavu wako uonyeshe busara japo kidogo au wewe ndio wale mnaoishi nje na hamjali hata kukitokea machafuko?
   
 10. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #10
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe ni kweli walipata misukosuko nakumbuka hata Bibi Titi Mohamed alipata msukomsuko wa maana baada ya uhuru! Lakini kuwashawishi watu kuendane na hoja na sio maneno ya chuki na uchochezi. Kuwashawishi watu kwa njia ya kistaarabu ni vizuri kuliko kwa njia zenye kuleta mifarakano. Ahsante kwa kucomment na kuona kuwa sina hoja.
   
 11. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Mohamed Shossi tatizo la mifumo yetu ya sheria ni kuwa haiko fair kwa nini mbunge wa ccm awe na kinga lakini wa chadema au cuf au updp asiwe na kinga hiyo na wote ni wabunge wa bunge moja?
   
 12. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi unaelewa vizuri ni kitu gani kinafanya nchi ziwe na amani? Kwa mtizamo wako Tanzania kuna amani? Haki ndio msingi mkuu wa amani haki inapotoweka hiyo amani haipo tena
   
 13. e

  ebrah JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  think twice!
   
 14. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Shossi anagekamatwa wa CCM wangemfanyia hivi kwanini ikiwa ni CCM kuna kinga lakini kwa CHADEMA inakuwa tofauti??? Why??? Kwa maana hiyo kwenye Sheria pia haina haki
   
 15. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kwa mtu makini yeyote aliyehuru katika mtazamo na maoni hatokubaliana na Kiongozi asiyetii mamlaka na sheria zinaongoza jamii. Hivyo kwangu mie Shosi yuko sahihi kimantiki na kikanuni. Lakini hoja yake ukiipima ktk mizania ya uhalisia, jinsi sheria hizohizo zinavyotumika kidhalimu unakubali kumsamehe Mkosaji Mbowe tena kwa aibu. Tukio kama hili ilikuwa muhimu litokee ili wananchi watambue sheria ilivyo msumeno kwa wapinzani, dagaa na wanyonge na si kwa watawala, mapapa/nyangumi wala wakwasi.
   
 16. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #16
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Najua huna maana ya kunidhalilisha nadhani jina langu linasomeka vizuri tu unless uwe unasababu zako binafsi za kuandika unavyotaka wewe.

  Well maneno yako ni kweli na ndio maana utaona G Lema na girlfired wa Slaa hawakukamatwa na kupelekwa mahakamani japo kuwa na wao hawakuhudhuria mahakani lakini walifuata taratibu za kuwasilisha sababu za kutofika mahakani nasisitiza kwa hili nadhani CDM wameteleza kidogo lakini kuteleza huko haina maana tuhubiri machafuko. Napenda mageuzi lakini sio kwa machafuko ya kijinga kama yanayohubiriwa hapa JF na wapenzi vindakindaki wa CDM. Naomba mnisameh kwa kutokuwa mnafiki kwenu.
   
 17. L

  LAT JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  MS ... hakuna hata chembe moja ya point to discuss .... its sometimes better to remain silence
   
 18. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tanzania bado ina kaaazi saana, tena saaana!,

  Asante kwa Maada Bwana Shosi,

  Asanteni kwa michango yenu wana JF, inatosha!
   
 19. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #19
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Tupinge njia zilizo sahihi kama ile waliyotumia LHCR kuhusu mgombea binafsi sio kwa kutumia uchochezi na vitisho hapo ndio mnapoharibu kuna kundi kubwa sana halishabikii vyama wanaanza kupata wasiwasi na mienendo yenu wanaowaambia wanawatakia mema.
   
 20. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,634
  Likes Received: 1,401
  Trophy Points: 280
  Naomba kuuliza hivi Freeman yuko nje kwa Dhamana Mpya au anaendelea na dhamana ile ile ya kesi ya zamani? waliohudhuria mahakamani nijuzeni kuhusu hili
   
Loading...