CHADEMA mtafukuza wangapi? Tazameni mlipojikwaa na sio mlipoanguka

Nov 27, 2019
35
145
CHADEMA MTAFUKUZA WANGAPI? TAZAMENI MLIPO JIKWAA NA SIO MLIPO ANGUKA

Kamati Kuu ya CHADEMA hivi Karibuni imetangaza kuwavua nafasi za Uongozi na Uanachama Wabunge wake Viti maalum (19) kwa tuhuma za usaliti dhidi ya chama kwamba waliamua kwenda kuapa bila kupata bila Baraka za chama.

Orodha ya Wanachama na Viongozi wa CHADEMA waliofukuzwa kwa kisingizio cha kusaliti chama ni Ndefu mno kuanzia kwa Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba, David Silinde, Anthony Komu na Wilfred Rwakatare na sasa Halima na Wenzake (18)

Swali la kujiuliza ni CHADEMA itafukuza wangapi? busara inaitaka CHADEMA kutazama inapojikwaa sio inapoangukia! Kama inaamini wanachama na viongozi ni wasaliti, kinapaswa kujiuliza kwanini kinasalitiwa?

Ukitazama kwa jicho la tatu, fukaza fukaza ya wanachama na viongozi ndani ya CHADEMA ni matokeo ya kukosekana kwa Demokrasia ya Ndani, Uzalendo na Udikteta wa Mwenyekiti wa milele wa chama hicho FREEMAN MBOWE.

Miongoni mwa Wanachama waliofukuzwa kwa sababu ya kukosekana kwa Demokrasia ndani ya CHADEMA ni Zitto ambae umma ulidanganywa alifukuzwa kwa kukisaliti chama, ukweli ni kwamba alifukuzwa baada ya kuonesha dhamira ya dhati ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa wa chama hicho hivyo kabla hajatimiza azma yake akashughulikiwa.

Kufukuzwa kwa Mdee na Wenzake ni uthibitisho wa kukosekana kwa Uzalendo, ubinafsi sanjari na mfumo dume ndani ya CHADEMA, Mbowe na Kamati Kuu iliyosheheni Wanaume, baada ya kukosa ubunge imeamua kuwaadhibu wabunge hao kwa kuwafukuza, yaani ‘Bora wakose wote’

Tathmini ya Mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake kwa upande wa vyama siasa nchini CCM imekuwa kinara ikilinganishwa na upinzani, imechukua hatua madhubuti kwa kuwapa nafasi mbalimbali za uongozi wa kitaifa mathalani imemteua Naibu Spika na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Wanamke ambao ni Tulia Ackson na Samia Suluhu mtawalia.

Kwa kuzingatia Tanzania ni nchi ya Demokrasia ya vyama vingi, inahitaji vyama vya upinzani imara vinavyoweza kutoa mchango katika kuleta maendeleo, ni kiu ya wapenda Demokrasia kuona CHADEMA inatumia muda mwingi kushughulikia kiini cha matatizo yanayokikabili hasa ya kukosekana kwa Demokrasiaya ndani, Uzalendo, Mfumo dume na ubinfsi ili kiweze kutimiza wajibu wake wa kikatiba.
 
Kama hivyo ndivyo basi usiinange Chadema ,kufukuza kuko vyama vyote na hakujaanza leo.Mwaka 1968,TANU ilifukuza wabunge kadhaa akiwemo Eli Anangisye mbunge wa Rungwe,Mwakitwange,Bakampenja na Dr.Fortunatus Masha babake Laurence Kego Masha, CCM iliwqfukuza Maalim Seif Sharif Hamad, Shaaban Hamis Mloo na wenzao akina Machano Hamis.

Miaka michache iloyopita iliyopita walifukuzwa Mansoor Yusuf Himid na Marehem Hassan Nassoro Moyo. Cuf ilimfukuza James Mapalala,CCM mwaka huu ilimfukuza Benard Membe,ilishamfukuza Sophia Simba nk.Mwanachama asiye tii mamlaka ni lazima ashughulikiwe.
 
Kwa hiyo kufukuzwa kwa akina Mdee hakuna sababu? Kha! Kumbe Socrates alikuwa sahihi kutembea amewasha taa mchana.

Lazima kuwe na sababu na kipi kimepeleka chama kufikia hapo.lakini chadema kutopenda kutoa sababu wakati wa kutokea mipasuko
 
Lazima kuwe na sababu na kipi kimepeleka chama kufikia hapo.lakini chadema kutopenda kutoa sababu wakati wa kutokea mipasuko
Sababu iko wazi acha kuandika propaganda.Chama hakitambui matokeo ya uchaguzi na msimamo ni kutoshirikiana na waliovuruga uchaguzi, chama hakijapeleka majina ya wabunge wa viti maalum .Halima na wenzake wamekaidi msimamo na kujipeleka kuapishwa na spika wa bunge lililotokana na uchaguzi uliolalamikiwa.

Kamati kuu ikawaita ili iwasikilize kwanini walikiuka misimamo ya chama wao wakakataa kuitikia wito.Ungeshauri chama kifanye nini zaidi ya kuwatimua?
 
Sababu iko wazi acha kuandika propaganda.Chama hakitambui matokeo ya uchaguzi na msimamo ni kutoshirikiana na waliovuruga uchaguzi,chama hakijapeleka majina ya wabunge wa viti maalum .Halima na wenzake wamekaidi msimamo na kujipeleka kuapishwa na spika wa bunge lililotokana na uchaguzi uliolalamikiwa.Kamati kuu ikawaita ili iwasikilize kwanini walikiuka misimamo ya chama wao wakakataa kuitikia wito.Ungeshauri chama kifanye nini zaidi ya kuwatimua?

Kwani chadema hipo aina ngapi na wanawasiliana vipi
 
Sababu iko wazi acha kuandika propaganda.Chama hakitambui matokeo ya uchaguzi na msimamo ni kutoshirikiana na waliovuruga uchaguzi,chama hakijapeleka majina ya wabunge wa viti maalum .Halima na wenzake wamekaidi msimamo na kujipeleka kuapishwa na spika wa bunge lililotokana na uchaguzi uliolalamikiwa.Kamati kuu ikawaita ili iwasikilize kwanini walikiuka misimamo ya chama wao wakakataa kuitikia wito.Ungeshauri chama kifanye nini zaidi ya kuwatimua?
Kwenye kosa tunaangalia,tendo ovu limetendeka( actus reus) je aliyelitenda alikuwa na nia ovu (mens rea)? Tukiridhika kwamba alituhumiwa alitenda na alikuwa na nia ivu,kinachofuata Ni adhabu mujarabu.Mambo ya reform and reconstruction yatafuata baadaye.
 
Kwani kwa akili zako unaona icho chama kinaisha leo?.Uko tunakoenda vyama vya mabadiliko vitakua vingi na imara zaidi kuliko nchi ilikotoka.Kwahiyo kama ilivyo kufa na kuzaliwa ndivyo hali kadhalika itakavyokua kwa chadema,uyu anakufa uyu anazaliwa uyu anafukuzwa uyu anajiunga.Harakati za mabadiliko sio kazi rahisi na lazima wawepo wanaokata tamaa njiani.Ila wale wenye dhamira ya kweli ndio watakao fika nchi ya ahadi.Heshimu maamuzi ya chama.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom