mwana wa Tanzania
Member
- Nov 27, 2019
- 35
- 145
CHADEMA MTAFUKUZA WANGAPI? TAZAMENI MLIPO JIKWAA NA SIO MLIPO ANGUKA
Kamati Kuu ya CHADEMA hivi Karibuni imetangaza kuwavua nafasi za Uongozi na Uanachama Wabunge wake Viti maalum (19) kwa tuhuma za usaliti dhidi ya chama kwamba waliamua kwenda kuapa bila kupata bila Baraka za chama.
Orodha ya Wanachama na Viongozi wa CHADEMA waliofukuzwa kwa kisingizio cha kusaliti chama ni Ndefu mno kuanzia kwa Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba, David Silinde, Anthony Komu na Wilfred Rwakatare na sasa Halima na Wenzake (18)
Swali la kujiuliza ni CHADEMA itafukuza wangapi? busara inaitaka CHADEMA kutazama inapojikwaa sio inapoangukia! Kama inaamini wanachama na viongozi ni wasaliti, kinapaswa kujiuliza kwanini kinasalitiwa?
Ukitazama kwa jicho la tatu, fukaza fukaza ya wanachama na viongozi ndani ya CHADEMA ni matokeo ya kukosekana kwa Demokrasia ya Ndani, Uzalendo na Udikteta wa Mwenyekiti wa milele wa chama hicho FREEMAN MBOWE.
Miongoni mwa Wanachama waliofukuzwa kwa sababu ya kukosekana kwa Demokrasia ndani ya CHADEMA ni Zitto ambae umma ulidanganywa alifukuzwa kwa kukisaliti chama, ukweli ni kwamba alifukuzwa baada ya kuonesha dhamira ya dhati ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa wa chama hicho hivyo kabla hajatimiza azma yake akashughulikiwa.
Kufukuzwa kwa Mdee na Wenzake ni uthibitisho wa kukosekana kwa Uzalendo, ubinafsi sanjari na mfumo dume ndani ya CHADEMA, Mbowe na Kamati Kuu iliyosheheni Wanaume, baada ya kukosa ubunge imeamua kuwaadhibu wabunge hao kwa kuwafukuza, yaani ‘Bora wakose wote’
Tathmini ya Mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake kwa upande wa vyama siasa nchini CCM imekuwa kinara ikilinganishwa na upinzani, imechukua hatua madhubuti kwa kuwapa nafasi mbalimbali za uongozi wa kitaifa mathalani imemteua Naibu Spika na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Wanamke ambao ni Tulia Ackson na Samia Suluhu mtawalia.
Kwa kuzingatia Tanzania ni nchi ya Demokrasia ya vyama vingi, inahitaji vyama vya upinzani imara vinavyoweza kutoa mchango katika kuleta maendeleo, ni kiu ya wapenda Demokrasia kuona CHADEMA inatumia muda mwingi kushughulikia kiini cha matatizo yanayokikabili hasa ya kukosekana kwa Demokrasiaya ndani, Uzalendo, Mfumo dume na ubinfsi ili kiweze kutimiza wajibu wake wa kikatiba.