Chadema msiyadharau haya tafadhali-kuelekea 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema msiyadharau haya tafadhali-kuelekea 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by commited, Oct 1, 2012.

 1. commited

  commited JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Iko wazi kuwa ccm kama chama tawala, kinafahamu fika kuwa kimeshindwa kuondoa kero muhimu kwa maisha ya mtanzania kwa zaidi ya miaka 50, matatizo hayo makubwa ni rushwa,ujinga, na umaskini. Na chama hiki kinafahamu kuwa watanzania wa miaka ya 1990, siyo hawa wa 2012, na wala hawatakuwa wale wa 2015, zaidi ya yoote chama hiki kinafahamu kuwa wananchi wengi wamekata tamaa ya kusikia ahadi za kila uchaguzi kwa zaidi ya miaka 50 sasa, baadhi ya hila zake zimeanza kufahamika KWA WANACHI WA KAWAIDA na hata kwa vyama pinzani hasa chama kikuu cha upinzani chadema. Hila za ccm ilizozitumia katika kushinda baadhi ya chaguzi zikiwemo zile za uchaguzi mkuu wa raisi 2010, ambapo chama hiki (ccm)kilitumia nguvu nyingi na pesa nyingi sana kuhonga mitandao ya simu kuwachafua wagombea mbalimbali hasa dr Slaa, kutumia tume ya uchaguzi kubadili matokeo, kuwatumia polisi katika kuhalalisha wizi wa kura wa majimbo mbalimbali kama mvomero, shinyanga mjini, ifakara na Kilimanjaro na kadhalika. CCM inafahamu kuwa kwa sasa inakabiliwa na tatizo sugu machoni pa wanachi hasa wa mjini na hata baadhi ya vijijnii juu ya matumizi mabaya ya madaraka, ukiukwaji wa haki za binaadamu, wizi wa rasilimali za taifa(madini,ardhi na kadhalika), wizi wa fedha za uma kama(mabilioni ya shimbo, mabilioni ya Epa, meremeta,kagoda na mengine mengi).MIKAKATI YA CCM KUMALIZA UPINZANI NA HASA CHADEMA KUELEKEA 20151.CCM Kwa ujumla wake kinajua hatari ya anguko kubwa liliyoko mbele yake hasa kuelekea uchaguzi mkuu 2015,na hata sasa kwenye chaguzi zake za nec inapanga watu ambao wanaushawishi mkubwa wa kifedha ili wakati huo wa chaguzi utakapofika rushwa iwe wazi wazi hasa maeneo ya vijijini, ikiwemo ununuaji wa shahada ya kupigia kura lakini pia CCM inajiandaa kugawa pesa kwa wanachi bila kificho,2. zimetengwa bilioni zaidi ya milioni 400 (safety net)" na chanzo cha fedha hizi ni kutoka mifuko ya jamii kama NSSF,na pia zimekusanywa toka kwa wafanya biashara wakubwa ambao wamekuwa na mikutano ya siri na mkuu wa nchi, lengo kuu ni kuhakikisha popote pale patakapooneka kunahatari ya kukosa kura hasa za uraisi( mchuno mkubwa utakuwa kati ya EL, Bilali, na Nchimbi na Membe) pesa hizi zitumike kuwapa wananchi!.3. Kati ya mwaka 2013-2015 Serikali ya sisiemu inajiandaa kutangaza huduma za afya, elimu kuwa bure, lengo ni kujaribu kupunguza nguvu ya chadema katika ajenda hizo, ili wahakikishe vile vitu amabavyo vinawapa nguvu chadema katika majukwaa vinapungua4. Hujuma katika maboresho ya daftari la wapiga kura ( Hili ntalieleza muda utakapofika)5. Pia kunamkakati ambao ulisha sukwa tangu 2009 hasa kwa chadema kuwatumia baadhi ya viongozi ambao ni rahisi kuhongeka, wapewe pesa, na wengine kuelekea uchaguzi mkuu watajitoa chamani na kugombea kama wagombea binafsi, (divide and rule)6. Lakini pia taassisi ya msajili wa vyama vya siasa, imepewa rungu la kuhakikisha anakimonita chadema na hata pale watakapoingia katika kumi na 18 zake akifute, zaidi ya yoote ili kuongeza ugawanyaji wa kura za wapinzani vyama vingi sana vitasajiliwa kuelekea uchaguzi mkuu na vingine vikiwa na mlengo wa kidini wazi wazi. Pia viongozi wa vyama vingi vya upinzani mbali ya cdm wameshapewa maelekezo ya kuwaatack live CDM, na hata kuwahujumu katika mikakati yao (oparesheni mbalimbali mikoani) na matamko yao mbalimbali lengo ni kuhakikisha cdm inapunguzwa kasi na hata kufa kabisa.CHADEMA IJIPANGE SANA, IWE NA PLAN B, C NA D KWANI CCM WANAJUA HATARI ILIYOPO MBELEYAO.. NA HAWAKO TAYARI KUACHIA NCHII HII KIRAHISI, WANAJIPANGA KUTUMIA KILA AINA YA NGUVU, HILA MAUAJI YA VIONGOZI WA CDM& WANAHARAKATI, VITISHO NA KADHALIKA, LENGO NI KUHAKIKSHA CCM INABAKI MADARAKANI.Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. commited

  commited JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mods, samahani naomba minisaidie kuweka aya(paragraph) ili isomeke vizuri kwa wadau , naona kila nikiweka nikisevu inabaki hivyo hivyo. asante
   
 3. MR. ABLE

  MR. ABLE JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,476
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wao wana pesa na dola, SISI TUNA PEOPLE'S POWER NA MUNGU.
  Hili ni kama GAME na sasa tuko final level, ushindi uko mbele yetu, sisi kama CHADEMA yatupasa kukaza buti.

  KIFO CHA NYANI MITI YOTE HUTELEZA.
  Kila hila watakayoitumia kwa lengo la kuivuruga CHADEMA hawatafanikiwa ila watazidi kukiimarisha na kukiongezea mvuto zaidi kwa wananchi.
   
 4. Mhamiaji Haramu

  Mhamiaji Haramu Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm ni magaidi
   
 5. t

  tenende JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hoja nzito, 2015 patakalika kweli hapa?
   
 6. t

  tenende JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Billion 400 sawa, lakini bilioni milioni 400 si sawa. Ni nyingi mno!.!
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  isomeke vizuri kwa faida ya nani? umbeya mtupu mpaka inakugomea wewe mwenyewe. Ondoa hadithi zako za kufikirika hapa!
   
 8. l

  lupasulwisye Senior Member

  #8
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fedha zao tutazichukua tu kwani ni fedha yetu hiyo wameimiliki kwa hila za ufisadi.Lakini kura hawatapewa hata kuchakachua hawataweza na wakijaribu patachimbika kuzilinda.Ushindi ni wa kishindo kikubwa kwani hamwoni kuwa wamebaki wenyewe na watoto wao ambao ni chini ya 'one percent.'Na hii si mjini tu hata vijijini mambo ni hivyohivyo na huko wameonja joto ya kuchakachuliwa hata mbolea,wanajua kuwa shule za kata walizopelekewa bila waalimu,bila vitabu,bila maabala za kujifunza kwa vitendo,wanajua kuwa watoto wametengwa kupata elimu nzuri,wanajua kuwa watoto wao(ccm) wanaandaliwa kuwa viongozi na maana wanapelekwa shule nzuri,wanajua kuwa wamefanywa masikini wakati nchi yao Tanzania ni tajiri,kwa ujumla watanzania wazijua haki zao zote na kuwa kudanganywa tena basi na kwa sasa wanajua mkombozi ni CHADEMA.CCM arobaini yenu ni 2015 tu.
   
 9. A

  Aristides Pastory JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ccm Kudandia hoja za Wapinzani ni Kawaida yao.
  Tutawauliza hiyo ipo kwenye ILANI yao?
  kama hakuna hizo hoja TUTAWASHITAKI kwa UMMA.
  Mbinu mbadala dhidi ya hawa MagaMBA ni kuendeleza kunadi sera za CHADEMA kila Pembe ya nchi halafu kuwahakikishia wananchi kuwa ukombozi wa kweli upo mikononi mwao laiti wakiendelea kuwabakiza cCM madarakani basi WASILALAMIKE.
   
Loading...