CHADEMA msiwatumie wajumbe wa CCM kwenye mitaa mnayoiongoza

Mzyondi

Member
Nov 24, 2016
40
64
Chama cha mapinduzi ni chama ambacho kimefanikiwa sana kujijenga kuanzia ngazi ya mjumbe wa nyumba kumi hadi ngazi ya taifa, na kimekuwa kikiwatumia wajumbe wa nyumba kumi wakati wa uchaguzi na hata kwenye shuguli za serikali.

Sasa ili kuwanyoosha au kuwadhibiti wajumbe hao ambao wamekuwa msaada mkubwa kwa CCM nawashauri viongozi wa mitaa wanotokana na CHADEMA wasiwatumie wala kuwatambua wajumbe wote wa CCM kwa kufanya hivyo watakuwa wanangoa mizizi ya CCM kuanzia chini kwa kuwa wajumbe hao hutegemea sasa shilingi elfu mbili wanazotoza kwa kila barua ya utambulisho kwenda serikali ya mtaa, Badala yake wawatumie wajumbe wanaotokana na UKAWA.

Kwa kufanya hivyo kutawezesha kukiimarisha chama kuanzia ngazi ya msingi hali itakayoisaidia CHADEMA wakati wa uchaguzi.

Mahali ambako CCM inaongoza huwatumia wajumbe wake pekee , sasa kwanini CHADEMA na UKAWA mkubali kuwatumia wajumbe wa CCM?
 
Unawezaje kuwatumia wasiotambulika kikatiba ?

Kazi kubwa ya mjumbe wa nyumba 10 wa ccm ni kushiriki wizi wa kura na kugawa rushwa ya kilo za sukari kwenye eneo lake , 90% hawajui kusona wala kuandika , hivi ni msaada gani watatoa watu wa hivi ?
 
Wacha kashfa wewe. Kama ni wajinga kiasi hicho mbona wanawagaraza sehemu tele. Kama mtaa unaongozwa na ukawa halafu wajumbe wa ccm wanatumika hapo nani mjanja nani mjinga.
 
Unawezaje kuwatumia wasiotambulika kikatiba ?

Kazi kubwa ya mjumbe wa nyumba 10 wa ccm ni kushiriki wizi wa kura na kugawa rushwa ya kilo za sukari kwenye eneo lake , 90% hawajui kusona wala kuandika , hivi ni msaada gani watatoa watu wa hivi ?
Ingawa hawatambuliki kikatiba lakini ccm inafanyanao kazi bega kwa bega na hauwezi kuandikiwa barua ya kukutambulisha kwenye taasisi yoyote bila kwenda na barua ya mjumbe kwenye ofisi ya serikali ya mtaa.
 
Ndio tatizo la chadema huwa hamfanyi tathmini
Kuna maeneo chadema wameshinda lakini hawana watu! Kura walipewa na watu wa ccm
 
Ingawa hawatambuliki kikatiba lakini ccm inafanyanao kazi bega kwa bega na hauwezi kuandikiwa barua ya kukutambulisha kwenye taasisi yoyote bila kwenda na barua ya mjumbe kwenye ofisi ya serikali ya mtaa.
Barua inayotakiwa ni ya serikali za mitaa , siyo ujinga wa mjumbe wa nyumba kumi , labda kama hiyo ofisi unayoisena inahusiana na mambo ya kimila , jaribu kufanya utafiti 90% ya hao wajumbe hawajui kusoma , how can i trust them ?
 
Umesahau ile operesheni Chadema ni msingi iliyohamasishwa nchi nzima? mimi ni mwenyekiti wa msingi (mjumbe) mtaa wa pugu station DSM kwa hiyo nafahamu umuhimu wa hicho nilichoshauri
 
Mwanzoni walisema Magufuli hawezi sababu tatizo ni mfumo.

Baada ya kuanza kuwatumbua mafisadi wenzao wakasema ni nguvu ya soda.

Baada ya mwaka mzima kuisha huku sindano zikiwaingia kwa kasi ile ile na soda haiishi nguvu, sasa wameanza kupongeza!

Safi sana Yericko, natamani ufipa yote ipokee ubatizo wa moto kama uliopokea wewe na hatimaye kuungana na rais bora kabisa duniani kulijenga upya taifa la Tanzania.
 
Magu ni jipu linalokaribia kuiva , tutalitumbua siku si nyingi 2020 sio mbali
 
Tunaomba Mwenyekiti wa Taifa Mboye atoe agizo la nchi nzima viongozi wa Chadema wasi watambue MABALOZI wa ccm Maana ni Nduli ktk Demokrasia hapa nchini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom