Chadema msiwatumie raia wapenda amani kufanikisha malengo yenu ya kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema msiwatumie raia wapenda amani kufanikisha malengo yenu ya kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ritz, Jun 12, 2012.

 1. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Wanabodi.

  Ninapenda sana hatua ya viongozi wa Chadema kuzunguka mikoani kuimarisha chama chao, ni hatua nzuri ambayo wananchi watapata nafasi kuijua vizuri Chadema ili kufanya maamuzi kama kujitoa ama kubaki ndani ya chama hicho.

  Kila kikundi, chama au taasisi yeyote inapofanya mambo yake bila kuwepo na utaratibu, kuna hatari kubwa ya kutokea fujo.

  Ni hatari kwa kiongozi wa chama kutofuata utaratibu wiki iliyopita Chadema walifanya mkutano wao kule Mtwara, Mbowe alimgomea (OCD) wa Nanyumbu, Mohamed Said, alipokuwa akihutubia eneo la Mangaka, OCD alimtaka Mbowe ashuke jukwaani kwa kuwa muda wa kuhutubia ulikuwa umemalizika saa 12 jioni.

  Mbowe akaanza kusema Jamani OCD anataka niache kuhutubia, sasa nasema wewe OCD mimi ni mbunge na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, hebu sikiliza usitutishe sisi, mimi simuogopi mtu yoyote awe Rais Kikwete, au Waziri Mkuu Pinda, hao nawaheshimu nao wananiheshimu, usitake kujifunzia kazi kwangu, ngoja kwanza niwaulize wananchi, mnasemaje nifunge mkutano nisifunge? Wananchi waliitikia, usifunge.

  Mbowe alichotaka wananchi wamshambule OCD ili fujo itokee watu wapigwe mabomu kisha aseme kuwa polisi wanaonea wananchi, wametumia nguvu nyingi, OCD alikuwa na uwezo wa kuwaamrisha vijana wake kumshusha kwa nguvu.

  Chadema msiwatumie raia wapenda amani kufanikisha malengo yenu ya kisiasa.
   
 2. H

  Hingi Jr Senior Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa!unajua viongozi wa CDM wanajifanya wako juu ya sheria lakini cha moto waliisha kiona hata wenyewe wana kumbukumbu ya yaliyotokea Arusha kwa mbwembwe hizohizo.Sisi wananchi tunajua ni CCM pekee nchi hii inayopenda kudumisha Amani na upendo kwa watanzania.
   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mbowe hakushoka na wananchi waliendelea kumsikiliza hicho ulichokisema kwenye RED mbona hakikutokea? Ama unaota? Riz dont be cheap!
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kwa kubadilisha mada Ritz unafahamu kuliko mtu mwingine yeyote tunasema Mukama kavuliwa nguo jana kwenye msiba wa Mzee Bob kwa kuongea uongo unatuletea mada ya mwezi mmoja ulio pita au hujapewa mshiko karibuni duh
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280

  POMPO.
  Baada ya kauli hiyo ya Mbowe OCD Said alihama kutoka eneo hilo na kusogea eneo lingine na kuondoka kabisa eneo hilo kuepusha shari.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Wki iliyopita ndio hili sakata limetokea kule Mtwara, mwezi haujafika mkuu...tukemee hizi tabia za viongozi wa Chadema.
   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,711
  Likes Received: 12,761
  Trophy Points: 280
  Huo ni uongo,mbowe ni kiongozi makini na hawezi kuwaruhusu wananchi kuvunja amani,ndio maana amani haikuvunjika,.

  Nahiyo imethibitisha kuwa yeye hupenda amani,lakn polisi wa nyinyie ndio huwa chanzo cha uvunjifu wa amani.

  Kweli M4C ni noma inamfanya ritz aweke kambi mtwara na kufuatili mikutano yetu.
   
 8. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  RiZ1 jamaa aliogopa nguvu ya Umma, kumbe wakati mwngine maafande wanakuwa na Busara,
  pamoja na kauli hyo ya mbowe kumbe hakuna Aman iliyovungika tufauti na uluvyothan ingekuwa
   
 9. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo umekosa habari ya kukuingizia chochote mfukoni toka kwa nape unaona uirejee hii zilipendwa
   
 10. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  ritz mbona unazungumzia hisia badala ya uhalisia mbona huhusishi police hao kuwaacha watuhumiwa wa uwizi wa wazi katika halimashauri zetu kama kule sengerema ambao wamekula pesa za dawa watu wanakufa hospitalini kwa kukosa dawa una leta umbea usio na kichwa wala miguu ...yule kakutwa na pesa nyingi kule kwenye kile kisiwa aaa kwako wewe sawa tu au unataka tumchome moto kama wanavyofanyiwa vibaka na police watasema wamechomwa na wananchi wenye hasira kali?
  wacha hizo fikiri kabla ya kuleta hoja sio kwa vile unaweza kuandika.....eti fujo ingtokea umekuwa shehe yahaya wewe

   
 11. i

  ibange JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ni afadhali huyo Mbowe nyie mnapandikiza udini na ukabila usiokuwepo ambao in the long run utaisumbua sana Tanzania
   
 12. mashami

  mashami Senior Member

  #12
  Jun 12, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  movement for changes "Msiogope! msiogope! ukombozi wa nchi umekaribia hakuna nguvu duniani iliyowahi na itakayo shinda NGUVU YA UMMA "MBUNGE WA ARUSHA MJINI GOBLESS LEMA
   
 13. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #13
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  cdm hata wakitawala cjuwi watafanya kazi na nani maana hawa polisi wamewa2ukana mn6
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Wewe kila post yako lazima umtaje Nape...ndio hoja yako kubwa JF.
   
 15. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #15
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  unasema sisi wananchi! Yani una maana ww na nan? Kwani mlishindiwa nini kumbeba tena na ndege za kivita kama kipindi kile? Mnawaacha malaya wakijiuza usiku kucha pale uwanja wa fisi lakini makamanda saa 12 tu mnataka wakalale? Ebooo...!
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280

  TOWNSEND.
  Ebu tujiulize Mbowe anasema hamuogopi Kikwete, sawa hamuogopi kwa lipi? Kwani kuna mtu alimwambia kuwa anamuogopa Kikwete, au Waziri Mkuu Mizengo Pinda?

  Kama hakuna kwa nini basi Mbowe afikie hatua ya kutamka hadharani kuwa hawagopi viongozi hao wa taifa? Kuna nini.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Amani ipi iliyopo Tz? Au hujui kama Tz kuna vita kali kati serikali dhidi ya wananchi wake? Au hujui kama watoto na wajawazito wengi wanavyokufa kutokana na Maralia ugonjwa ambao serikali inaweza kuuzuia? watu wangapi hupoteza maisha kwa kukosa huduma ya kwanza pindi ajali zinapotokea kwani hakuna Ems wakati serikali inao uwezo huo? Hujui watu wangapi hupoteza maisha hospitalini kwa kutokuwa na madawa au uzembe wa madaktari? Au hujui jinsi gani mkulima hawezi safirisha mazao yake kutokana na miundombinu duni au pindi anapo cheleweshewa pembejeo na kwa bei ya juu zaidi? Au hujui milipuko ya bei za vitu hapa Tz? Au hujui bila kutoa kitu kidogo a.k.a Rushwa huwezi kushughulikiwa ktk ofisi za serikali? Tz hakuna amani wananchi tunaburuzwa sana.
   
 18. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #18
  Jun 12, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  mbowe anajuwa police wanatumiwa na viongozi waliopo madarakani ..kumbuka kule kigoma jk alihutubia mpaka saa moja hakuna aliemshusha

   
 19. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #19
  Jun 12, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Toka lini umekuwa msemaji wa umma? OCD alijua alichotakiwa kufanya. ni matokeo ya M4C somo linaeleweka
   
 20. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #20
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  cdm hata wakitawala cjuwi watafanya kazi na nani maana hawa polisi wamewa2ukana mn6
   
Loading...