CHADEMA msisuse kuibua madhaifu ya CCM na Serikali yake kama yapo, Pamoja tutaijenga nchi yetu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Ni wazi kuwa baada ya CHADEMA kubakiwa na wabunge 20 tu uwanja wa bunge hautakuwa rafiki sana kwao kutupasha taarifa "nzito nzito" kama ilivyozoeleka.

Hivyo nawashauri CHADEMA kwa haraka watafute njia mbadala za kuhabarisha Umma makandokando ya chama tawala na Serikali yake kama yapo.

Tusisahau kuwa CHADEMA bado ni chama kikuu cha upinzani na vyama vingine vilivyobaki havina historia ya kuikemea CCM na Serikali yake.

Maendeleo hayana vyama!
 
Dhuluma ni mbaya sana.Ni aibu kubwa ile sala mjengoni nashauri ibalike liwekwe jina la mungu wenu wa sasa hadi muda wake uishe kiukweli ndie anaeabudiwa kuliko Muumba.
Dhuluma ya nini bwashee?!
 
Wewe unawashwa sana, nyuzi zako nyingi zinaonyesha kuunga mkono upumbavu wa CCM na Maccm wenyewe sasa unakuja na mpya ya kuitaka CHADEMA kuibua madhaifu ya serikali.
Siasa siyo uadui bwashee.

Anayewashwa ni Robert Amsterdam!
 
Kukaa kimya huku Lema na Lisu kutoroka ni mkakati nafikiri. Ndiyo maana imekua cited kama kiashiria cha ukandamizaji demokrasia na USA.

Pia kuna katazo la rais juu ya nani anatakiwa afanye mikutano ya kisiasa na wapi. Hivyo unachokitaka kuwezekana siyo leo.
 
Mmeshaanza kuona umuhimu wa magunzi. Tatizo ni kuwa mmeshachelewa.
Kule kwetu tunatumia magunzi kuwashia pasi za kienyeji maana umeme haujafika au pengine umekatika. Sasa nguo zimejikunja na umeme hakuna wanaanza kutafuta magunzi wakati waliyatukana sana kipindi umeme unawaka. Sasa wasubiri tena luku ikate na hela hawana mfukoni ndo watajua umuhimu wa magunzi. Mkaa nao umepigwa ban.
 
Ni wazi kuwa baada ya Chadema kubakiwa na wabunge 20 tu uwanja wa bunge hautakuwa rafiki sana kwao kutupasha taarifa "nzito nzito" kama ilivyozoeleka.

Hivyo nawashauri Chadema kwa haraka watafute njia mbadala za kuhabarisha Umma makandokando ya chama tawala na serikali yake kama yapo.

Tusisahau kuwa Chadema bado ni chama kikuu cha upinzani na vyama vingine vilivyobaki havina historia ya kuikemea CCM na serikali yake.

Maendeleo hayana vyama!
Damu mlizomwaga zimeanza kuwalevya, tutasikia mengi
 
Ni wazi kuwa baada ya Chadema kubakiwa na wabunge 20 tu uwanja wa bunge hautakuwa rafiki sana kwao kutupasha taarifa "nzito nzito" kama ilivyozoeleka.

Hivyo nawashauri Chadema kwa haraka watafute njia mbadala za kuhabarisha Umma makandokando ya chama tawala na serikali yake kama yapo.

Tusisahau kuwa Chadema bado ni chama kikuu cha upinzani na vyama vingine vilivyobaki havina historia ya kuikemea CCM na serikali yake.

Maendeleo hayana vyama!
Miaka mitano ijayo ni CCM peke yenu,tunaisubiri kwa hamu kubwa Tanzania kama uraya na Arusha kama karufonyia.
 
Back
Top Bottom