Chadema msipapatike na wanaotoka ccm - wachunguzwe kwanza.


BLUE BALAA

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Messages
936
Likes
59
Points
45
BLUE BALAA

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2010
936 59 45

Natoa angalizo kwa Chadema. Mmetumia muda mrefu sana katika kukijenga Chama mpaka kufikia hapa kilipo. Sasa hivi ndio chama kikuu cha upinzani kinacho ongoza kwa wanachama wengi nchini, matawi, madiwani na wabunge. Kila mtanzania anaelewa changamoto ambayo Chadema imetoa katika uchaguzi mkuu uliopita.
MAONI:
Binafsi sioni sababu ya kupapatikia viongozi walioshindwa CCM na kukimbilia Chadema ili kupata njia Rahisi ya kwenda bungeni. Kwanini wasikimbilie NCCR, TLP, CUF etc? Wanajua Chadema kina nguvu na itakuwa short cut ya wao kupata wanachotaka. Wengine walidiriki mpaka kuvunja vyama vyao na kuingia Chadema. Mbona Mbowe na wenzake wamevumilia Chadema kwa miaka yote hiyo mpaka chama sasa kimekuwa hivi (Mbowe alijiunga na Chadema akiwa na miaka 30 na mpaka sasa anazeekea huko)
Ushauri wangu tusipapatike na viongozi waliokimbia CCM ila tu groom vijana wetu kama Zitto, Wenje, Halma Mdee, Mr Two, John Mnyika, Lema etc na sio hawa makubuhu ambao wakijiunga wanataka ubunge au uongozi ndani ya chama. Hawa watatuvunjia chama kwani wakikosa walichotaka basi wana anza majungu na hatimae wanaleta mpasuko.
Nalaumu viongozi wa Chadema kwani watu kama hawa wakijiunga tu moja kwa moja wanakuwa na ticket ya kugombea nafasi za juu kama ubunge etc. Kama ni wazalendo wangebaki wanachama kwanza ili watoe mchango kwenye chama na tuutambue.
Karibuni.
 

Forum statistics

Threads 1,237,306
Members 475,501
Posts 29,283,973