Chadema msione aibu kuiga NCCR-Mageuzi kwa kuthubutu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema msione aibu kuiga NCCR-Mageuzi kwa kuthubutu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAFILILI, Dec 27, 2011.

 1. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nachukua fursa hii adimu kutoa hongera kwa viongozi wa NCCR Mageuzi kwa kuonyesha UJASIRI wa kuwaita viongozi na wanachama mbele ya vikao halali na kuchukua maamuzi magumu ya kuwavua uanachama akiwemo mbunge wa Kigoma Kusini, Kafulila.

  Wakati CUF nayo leo wakitarajia kumweka kiti moto mbunge wa Wawi, Hamad Rashidi, CHADEMA wamekuwa butu kumwita mbunge wao, John Shibuda anayeonekana anawasaliti kupitia kauli zake na vitendo vyake vya kutufuata mwenendo wa viongozi wake wa CHADEMA.


  Kulikoni CHADEMA kwa nini mnakuwa wagumu kumweka kiti moto Shibuda????? Mie nafikiri Shibuda kawashika pabaya hivyo mwaogopa mkimpiga chini, atamwaga uozo wenu wote mbele ya jamii.

  Poleni kwa kushindwa kufanya maamuzi dhidi ya Shibuda ama mwaogopa ruzuku kupungua????
   
 2. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hakuna mwenye ubavu ndani ya CDM kumgusa Shibuda, na yeye aliisha sema wao wakimwaga ugali na yeye anamwaga mboga

   
 3. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  MAFILILI,
  Hivi huona uamuzi wa CDM kuendelea kumvumilia Shibuda ni sehemu ya Uamuzi Mgumu ambao NCCR wameushindwa kwa Kafulila na kwamba CUF nao wanapaswa waige mfano huu wa CDM katika kumkabili Hamad Rashid?
   
 4. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2011
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Sio kila kitu akifanya mwenzako na wewe lazima ukiige kizima kizima. Muda mwaafaka ukifika na kama kweli SHIBUDA ataonekana amefanya kosa linalositahili adhabu ya kufukuzwa uanachama nadhani CHADEMA watafanya hivyo . Kwanza wameshafanya hivyo kwa madiwani wake watano huko ARUSHA
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye bold... kulikuwa na madai kwua wajumbe wa kikao kile wengui walichomekwa baada ya wengine wengi kufutwa bila maelezo ya kueleweka. Nina mashaka iwapo tunaweza kukiita kikao kile kuwa ni halali.
  Lakini kwa ujumla wa hoja yako, nitaishangaa sana Chadema iwapo itaamua kuanza kuiga mambo yanayofanywa na vyama vingine
   
 6. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Siyo siri tena, Shibuda akiwa bungeni alitofautiana na hadi leo yupo tofauti na mtazamo wa CDM kuhusu na suala la posho. Itakumbukwa Shibuda tangia siku ya kwanza ya bunge alikuwa tofauti na wenziwe juu ya kumtambua JK. Sina budi kuamini kuwa CDM wakimwaga ugali, Shibuda atamwaga mboga, Kazi ipo kweli kweli CDM wameshikwa pabaya na Shibuda!!!
   
 7. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mimi nafikiri kufukuzana siyo njia pekee ya kumaliza migogoro katika vyama vya siasa,cha msingi ni kukubali kutokubaliana.Kufukuzana kutakuwa na maana pale tu mwanachama atakapokwenda kinyume na sera cha chama.
   
 8. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Maamuzi magumu ni pamoja na kutotoa maamuzi ya kipuuzi kwa kufuata mkumbo.
   
 9. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kawambie magamba wawatimue kwanza el na ec
   
 10. F

  FUSO JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  CDM kuna mambo ya muhimu ya kufanya kwa sasa zaidi ya kumjadili Shibuda - nani asiyemjua shibuda? Leo kaibukia kete ya kuwalaumu viongozi wa dini wasimseme Rais wake kabla hata hajafanya utafiti wowote, tena huku alikoibukia ndiko kubaya zaidi bora livyokuwa anawasema viongozi wake bungeni. kuitisha kikao kumjadili mtu huyu ni gharama ni vyema muda na hela hiyo itumike kuimarisha chama.

  Viongozi wa dini wamefanya mambo mengi sana kuishauri serikali hii hadi wakatoa miongozo - sasa sijui jamaa alikuwa muda wote anafikiria POSHO tu hata hafuatilii jambo hili.
   
 11. K

  Kilindila Rojas Member

  #11
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama kumvumilia mtu ndio uamuzi mgumu, kwanini chadema walishindwa kuchukua maamuzi hayo "uyaitayo" magumu zidi ya madiwani wa Arusha?
   
 12. F

  FUSO JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  kaka CDM ni taasisi makini, haifikiri kwa kiwango chako and who is Shibuda ndani ya CDM?
   
 13. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Time will tell.
   
 14. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  magamba magumu?
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ebu niambie kitu ambacho Shibuda anacho ambacho iwapo atakisema au kikfanya itasababisha Chadema iwe katika hali mbaya
   
Loading...