Jibaba Bonge
JF-Expert Member
- May 6, 2008
- 1,246
- 402
Napenda kutoa changamoto kwa Chadema na wapenda mabadiliko halisi kwamba msifikiri kwa kupata wabunge 23 wa kuchaguliwa na 25 wa viti maalum ccm wamefurahi au wanaona ni sawa tu, yaani hawajafurahi wala hawajachukia. Mtakuwa mnafanya kosa kubwa sana.
Kwa sasa mkae mkijua kuwa mnao maadui, si maadui wa kawaida wa kisiasa ambao uadui ni kushindana katika medani za kisiasa bali ni maadui wa kutaka kuangamiza Chama kabisa ili ikiwezekana kife kabisa kuondoa ushindani.
Ninasema ccm hajafurahi kwa sababu ndicho chama kilichoathirika kwa 100% na mafanikio ya Chadema. Kutoka wabunge 5 mpaka 23 wa kuchaguliwa na kutoka wabunge 6 mpaka 25 wa viti maalum siyo pigo dogo kwa CCM. Idadi ya wabunge walioongezeka kwa Chadema ndiyo idadi iliyopungua kwa CCM ukiachilia mbali majimbo mane yaliyokwenda CUF; la Lindi mjini na yale ya Unguja.
Kwa mtazamo huu, CCM, in simple terms, itaathirika kwa
1. Kupungua kwa ruzuku,
2. Kupata challenges nyingi wakati wa kupitishwa miswada bungeni hasa ukizingatia mix ya wabunge wa Chadema,
3. Kupungua kwa halmashauri inazoziongoza,
4. Chadema kuongeza nguvu mikoani na kuwa na model classes nyingi (ongezeko la halmashauri inazoziongoza) na kama itaziongoza vizuri ni threat kwa CCM uchaguzi wa 2015
5. Chadema kuongeza nguvu kifedha ongezeko la ruzuku hivyo kuwa na uwezo wa kujijenga na kuwa na mtandao mpana zaidi, another threat.
Katika hali hii chadema isitarajie kipindi hiki cha miaka 5 kitakuwa smooth hata kidogo. Upo uwezekano wa maadui kukivuruga kwa kutumia mbinu mbalimbali za kukihujumu kwa mfano; kuwagombanisha viongozi, kuingiza mamluki ndani ya chama, kutumia fedha ili kuwanunua baadhi ya viongozi au wanachama, inawezekana pia hata kutumia government agents kwa namna moja ama nyingine.
Kutokana na hayo ninaishauri Chadema wawe macho sana hasa katika kipindi hiki. Siri za chama ziendelee kuwa sirini, watu wote wasiwe wasemaji wa chama, viongozi wajitahidi sana kuwa wamoja na wanie mamoja, wasiruhusu mambo wanayotofautiana yakawa open kwa public na tofauti za viongozi zikawa open publicly kama ilivyotokea kwa Zito kuelezea yaliyotokea kwenye kikao cha wabunge wa Chadema kuhusu kutoka nje ya Bunge ama la wakati raisi akilifungua rasmi. Katika kikao hicho kulikuwa na differencies lakini mwishowe msimamo wa pamoja ulifikiwa kwa majority votes. Msimamo huo ndiyo unaotakiwa kujulikana kwenye public siyo zile differencies zilizokuwepo na nani na nani walipinga ama walikubali.
Chadema mmeanza vizuri endeleeni vizuri. Umoja wa kweli na mshikamano wa kweli ndiyo silaha sahihi na kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake. Maslahi ya Taifa yawe mbele ya maslahi binafsi. Katika kila mnayoyaamua au kufanya waangalieni wananchi na umaskini wao ambao hawakujitakia kuwa nao.
Hakuna source ni maoni yangu.