CHADEMA, msifanye kosa kuendelea na ziara kabla ya kumzika marehemu Morogoro

segwanga hiyo namba 3 wamesema uchunguzi unafanyika kubaini kama silaha iliyotumika ni ya polisi, hayo ndio maajabu ya policcm huchelewi kusikia ganda lililookotwa sio lao au uchunguzi ukakamilika baada ya octoba 2015.
 
Last edited by a moderator:
kweli wewe siyo muungwana!!! waungwana hutenda yaliyo mema na kuwasitiri wafu katika nyumba zao za milele ni jambo jema.

Katika dini wanaozika ni watu sio chadema ; na wala watakiwi kuharakisha kuzikwa kwa sababu zao za kisiasa zilizo mfanya auawe; kama ndo sababu za kisiasa CHADEMA Wanausika
 
Mmm tuwashughulikie hawa wasio na utu. Maandamano mamgapi yanafanyika hapa nchini, hawayagu ila ya CDM tu. Mbio za mwenge, timu za mipira, mabondia. Huu ni uwoga tu wa M4C. Chungeni sana maamuziyenu, nyie Polisi sio wanasiasa, wanawatumia halafu watawatosa. take my words.
 
Nami ntashiriki nikipewa ratiba mapema, ofcoz Ally amekuwa shujaa wa mabadiliko mkoan Morogoro, napendekeza hilo tamko litolewe na mnafiki Zitto, ama yeye haguswi? ama ndio kutoikosoa serikali ya JK? anajitega vijana wanakufa?

Zitto ni zaidi ya mnafiki, hafai kwa lolote. CCM wanamtumia kama karai la kokoto. wakiridhika watamtupa mbali. Hiyo kauli, napendekeza aitoe dhidi dhaifu mwenzake JK.
 
Naunga mkono hoja yako. Lazima Dr Slaa naye ashiriki msiba huo. CCM fukuzilia mbali na hapo.
 
Kwa wale wote mnaoweza kuufikisha ujumbe huu kwa Katibu Mkuu Mh DR. SLAA, kulingana na tukio la jana mjini hapa, kuna propaganda nzito sana ilikuwa inajengwa na makada viongozi na wabunge wa CCM hapa mkoani kwa nyakati tofauti wakinyatia kuona kama ushiriki wa CHADEMA kwenye msiba wa marehemu kamanda ALLY ZONA, aliyepigwa risasi na polisi waliokuwa wanazuia maandamano ya amani jana litachukuliwa uzito kama lile la ARUSHA, ama hawa watapewa mtu wa uwakilishi kwa ajili ya chama kujitoa lawama?

Cha msingi hapa na ushauri wangu kama mpenda mabadiliko ni kutowapa nafasi hawa mashetani wa kijani wauwaji kujenga hoja yoyote ya kupumbaza watu.

1. VIONGOZI WA CHADEMA WASHIRIKI KIKAMILIFU AKIWEMO KATIBU MKUU
2. TAMKO ZITO LA KUTOENDELEA KUVUMILIA MAUAJI LITOLEWE
3. IFIKE SEHEMU POLISI WAOMBWE MAJIBU YA SABABU ZA KUUA WANANCHI BILA SABABU

TUANZIE HAPA MOROGORO

AHSANTENI
Nadhani CDM na wapenzi wake ilitakiwa kufikiria kwa kina ili kubaini wakati mwafaka wa kuendelea na Kampeni zake za M4C. Sikutarajia viongozi wake wangeshindwa kufanya tafakuri ya kina na kutambua kuwa Wakati taifa lipo katika wiki ya sensa, hakuna tija kwa chama wala umma kufanya maandamano na mikutano aina hiyo, wakijua wazi kuwa hao wanaotaka kuwahutubia walitakiwa wawe majumbani wakisubiri kuhesabiwa! Kwa kibri hicho imejivunjia heshma na kufifisha mvuto kwa jamii!
 
....[/QUOTE]

Mawazo kama haya hutoka kwa watu wanaojitambua na kufanya siasa safi..nao si wengine ni wana CHADEMA, hata kama ningeamka usiku wa manane na kusema maneno haya ningejua tu uko well upstairs na hauwezi kununuliwa na siasa za maji taka na za vilaza wa CCM.

Naamini viongozi wa CHADEMA pia walikuwa na mawazo haya tangu awali maana CHADEMA ni chama makini
.
 
“Tuko tayari kushirikiana na familia ya kijana huyo kwa ajili ya taratibu zote za mazishi. Tutamzika kishujaa kwa kuwa alikufa akikipigania chama,” alisema Dk Slaa.
Aliwataka wananchi kuonyesha uchungu kwa kifo cha mfuasi huyo kwa kutupa kadi za CCM na kuchukua za chama hicho cha upinzani.

Nakubali Dr.Slaa kanena ya moyoni mwake na mwetu pia.
Hapa morogoro Abood alishaweka utaratibu wa kuratibu mazishi ya wafiwa kila mara, CDM wazike wafu wao, naamini uongozi uko makini tuamini katika hilo watafanya kile kinachotakiwa kufanya pale mwanamapinduzi na mpigania demokrasia anapopatwa na kifo kwa njia ya kiharamia kama ambavyo shilogile amefanya.Kuna kitu inaitwa the HAGUE inamsubiri
 
Hawa policcm wasije wakaiba maiti kama kule tarime.Kuweni makini manake
watajifanya wameumizwa na kifo hicho na wanataka kugharamia mazishi.
 
Msiba wa taifa!... CDM ni majonzi!... Ni pigo kuondokewa na kamanda ALLY!.. Naamini CDM Itafuata ushauri wako kamanda!!.
 
.....[/QUOTE]
Acha utoto, sensa haizuii shughuli yeyote!Unaacha taarifa nyumbani unakwenda kwenye shughuli zako!

SENSA KWA MAENDELEO
JIANDAE KUHESABIWA
 
Acha utoto, sensa haizuii shughuli yeyote!

Unaacha taarifa nyumbani unakwenda kwenye shughuli zako!

SENSA KWA MAENDELEO
JIANDAE KUHESABIWA

Utoto ndio huo: Huyo atakayeachwa nyumbani hatakiwi kuhudhuria mikutano! Kila kitu hufanyika kwa wakati mwafaka sio kukurupuka tu!
 
Back
Top Bottom