CHADEMA msiende Uchaguzi Mkuu kudai katiba mpya, kudai Tume Huru nendeni na ajenda za kutatua shida za watu

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Nimewasikiliza chadema katika mchakato wao wa kupata mgombea wa uraisi. Frankly speaking mna very strong candidate tatizo lenu ni kutokujua audience.

Mkijua audience mtajua mtajua ni mambo yafuatayo

1. Vyama vya siasa vina wajibu gani na changamoto gani
2. Serikali ina wajibu gani na changamoto gani
3. Wananchi wana wajibu gani na changamoto gani?

Mkiyatambua hayo mtajua yapo mabadiriko ambayo wana jamii wanayatamani katika makundi tofauti hayo ya vyama vya siasa, serikali na wananchi na mabadiliko hayo yana michakato yake.

Tunapokwenda kwenye uchaguzi itakuwa ni makosa makubwa sana kwenda kwa wananchi kudai tume huru ya uchaguzi, kudai katiba mpya n.k

Hayo sio mambo yaliyoko kwenye mamlaka ya wananchi kufanya kwa michakato ya nchi hii.

Uchaguzi huu ni wananchi kutoa madaraka na madaraka haya wanayotoa wananchi wao hawatazami shida za vyama vya siasa, wao wanatizama shida zao.

Swala la Katiba mpya, Tume Huru, Vyombo vya Dola wanaoweza kulisimamia ili likae sawa ni vyama vya siasa. Lakini kutokuwepo uwiano wa kimadaraka, hawa wameshikilia madaraka makubwa na wengine madaraka madogo hamuwezi kusema tukae chini tujadiri.

Kama nguvu zenu za kimadaraka yanayotoka kwa wananchi zingekuwa zinataka kulingana haya ya tume huru, n.k mngekuwa mshayazungumza.

Hivyo basi kwenda kwa wananchi kuwaambia tunataka tume huru, tunataka katiba mpya kama ajenda zenu hamuwezi kushindana na atakayekuja anawaambia watu nataka nimalizie bwawa la umeme ili umeme ushuke, nataka nimalizie standadi geji, n.k

Tafuteni hoja zinazogusa maisha ya watu moja kwa moja ili wawapeni madaraka na mkishapata madaraka ndiyo mfanye kazi yenu ya kutafuta uwanja sawa wa ushindani kisiasa.
 
Ni kweli,

Wananchi wengi hawajui hata mapungufu ya katiba hii.

Wengi hawafahamu tume huru nini.
Vitu vinavyogusa maisha yao ni kama
Kilimo,
Maji
Huduma za afya
Ajira
Stahiki za wafanyakazi
Miundombinu
N.k
 
Iyo kweli mkuu wananchi wengi hawaijui hata iyo katiba ni nini na ukisema tume huru ndo unamchanganya kabisa watanzania ni wavivu kusoma na hivyo vitu vipo kwa maandishi na haviko wazi saana adi uvitafute sasa kutafuta + kusoma apo humpati mbongo ataona unamchezea ndombolo tu labda elimu kuusu haki za wananchi zinazowagusa moja kwa moja kama ilivo kwenye katiba madhaifu ya iyo katiba yanayowagusa moja kwa moja madhaifu ya tume n.k hapo kidgo utawashika sababu unakua umewagusa matatizo yao.
 
Na kweli
Wagombea wajikite ktk kutatua kadhia mbalimbali za watu
mfano kuboresha maisha ya watu kwa ujumla,
kuboresha kilimo,
kushusha bei za vitu muhimu mfano sukari,
kuongeza mbinu za kutatua suala la ukosefu wa ajira kwa vijana,
mishahara kwa watumishi,
kodi na mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na
kurekebisha uvunjifu wa katiba na pale ambapo sheria hazifuatwi basi zifuatwe
 
Na kurudisha furaha;
baadhi ya watu wapo kwenye maumivu makali
Mfano wastaafu na pensheni zao kuchukua muda mrefu kuzipata
Fao la kujitoa hadi miaka 60 inasemekana
Waliofukuzwa vyeti feki bila kitu
Waliofunga biashara
Na wengine wengi wanaokabiliwa na ugumu wa maisha unaotokana na 'systemic' decisions nk
 
Back
Top Bottom