CHADEMA mnazidi kupoteza dira kwa wananchi

Wadau JF!
Ninalazimika kuyaandika haya ingawa ninaelewa chadema kwa ujumla huwa hawapendi kuambiwa UKWELI.

Nitasema kwa ufupi sana ili nisiwachoshe wasomaji.

La kwanza ni kuhusu kesi iliyoko mahakamani ambapo mwenyekiti Mbowe na wenzake, wanashitakiwa na jamhuri kwa makosa ya ugaidi na uhujumu uchumi.

Imekuwa kawaida kisheria inapotokea mgongano wa mjadala au hoja katika majukwaa ya kiraia na kisiasa kujikuta yanaongelea jambo ambalo tayari liko kwenye mahakama zetu nchini. Na ikawa jambo hilo bado halijatolewa hukumu.basi mihimili mingine hulazimika kutolijadili mpaka pale litakapofikia tamati yake.

Lengo kuu likiwa ni kutovuruga mwenendo wa kesi mahakamani.

Lakini kwa #chadema wao hali imekuwa tofauti, kwani
Sasa hivi kesi ya mbowe ambayo inatajwa mfululizo huko mahakamani, imekuwa pia ndio agenda ya platform zote za chadema, kuanzia Bavicha,Bawacha,wazee wa chadena na uongozi wote wa kitaifa bila kuwasahau na wale wakimbizi walioko ughaibuni.
Kupitia mitandao ya kina Fatuma karume na Maria sarungi.

Sasa suala hili linaleta mkanganyiko kwa sababu linapelekea au linaweza kuvuruga mwenendo wa kesi inayoendelea mahakamani.

Sidhani kama chadema na uongozi wao hawalijui hili au ni kwa makusudi ili kuvuruga mwenendo wa kesi mahakamani?

Jambo lingine ni lugha zisizo na staha dhidi ya uongozi wa kitaifa na pia viongozi mbalimbali wakiwemo majaji, zinazotolewa na viongozi na makada mbalimbali wa chadema wakiongozwa na makamu mwenyekiti Tundu lissu na kada mkorofi Godbless lema.

Jambo hili linawaondolea staha mbele ya wananchi na kupelekea kutowaamini na hivyo kushindwa kuwashawishi kujiunga nanyi katika harakati zenu kwa kuwapuuza na kuwaona wahuni.

Ukiachana na madai yenu ya katiba mpya,tume huru ya uchaguzi na kutaka Mbowe kuachiwa huru kwa matakwa yenu.

Watanzania wanazo kero nyingi ambazo wangependa kusikia zikiongelewa badala ya hizo nilizozitaja hapo juu,ambazo kwa ujumla zina akisi matakwa yenu binafsi ya kusaka madaraka.

Lakini nissishie hapo bila kusema la mwisho.

Matamko yenu yanakinaisha jamii,na kila uchao mnatoa matamko ya kibinafsi, badala ya matamko yenye kubeba madhila halisi yanayowakumba wananchi kule site.
Mfano juzi mmekuja sijui na bunge la wananchi mkimuiga Raila odinga wa Kenya.

Lakini pia watanzania tuna majukumu mengine mengi ya kuendesha familia zetu ambayo sio ya kisiasa.

Hivyo ninapomsikia Lema akishawishi wananchi kuingia mabarabarani kumtetea Mbowe. Ninapata ukakasi.

Mbowe kama mbowe hawezi sababisha watanzania zaidi ya miliomi 46 wasio wanachama wa chadema kuvurugiwa amani na kuachishwa shughuli zao za kukidhi mahitaji ya familia zao kisa Uhuru wa mbowe ambaye hawana uhakika na usafi wake binafsi.

Lema aliekimbia bila kukimbizwa yeye ameweka familia yake nje halafu unachochea walio ndani ya nchi na familia zao, waharibu future zao?

Msitake kitushirikisha kuwasaidia kuusikiliza uchungu wa kukaa benchi next 4years....tutawakemea daima..
HAYA NI KWELI CHADEMA IMEPOTEZA DIRA,..Unalingine na nyongeza.

Kama hakuna jipya lingine wakupe 7000/- ukanunue unga ,nyanya,dagaa na vitunguu mle wewe familia yako,usisahau kumpeleka mama yako anayoumwa kansa ocean road
 
Kama wanapoteza dira hebu tuwe na tume huru ya uchaguzi na katiba mpya hapo ndo uje na hoja zako sio unatoa hoja baada ya kupokea buku 7
 
Nimemnukuu leo kwenye kile kipindi chao online.
Kwa Fatma karume akitamka kwamba watanzania 10000 wakiingia barabarani kwa muda wa saa moja.
Haitamchukua zaidi ya masaa 12kufika Namanga border alipotumia kukimbia.
😂😂😂
 
Watanzania wanazo kero nyingi ambazo wangependa kusikia zikiongelewa badala ya hizo nilizozitaja hapo juu,ambazo kwa ujumla zina akisi matakwa yenu binafsi ya kusaka madaraka.
Kwa andiko lako hili ungetumia muda huo kuainisha kero nyingi za watanzania na kutolea suluhu badala ya kujifanya unawananga CHADEMA
 
Chama kinachojinasibu kuwa kikuu cha upinzani ,kikijibasibu kuwa na vijana wenye vipawa vya ubunifu wa sera.
Mnashindwaje kuliona hilo na kulifanyia kazi.mnasahau kwamba mwisho wa uchaguzi mmoja ndio mwanzo wa uchaguzi mwingine!

Mtakaa mnalalamika mara paap 2025.hamna jipya la kuwaambia wapiga kura na mkipigwa chini mnaanza kulialia tena kuelekea 2030.!
 
Tanzania kuna uchaguzi?, Angalia kuna vijana wangapi waliounga mkono juhudi wamepewa nafasi moja kwa moja wakaachwa wafia chama
 
Back
Top Bottom