Chadema mnatuangusha wakazi wa Manyoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema mnatuangusha wakazi wa Manyoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by man lesha, Oct 17, 2012.

 1. m

  man lesha Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Chadema mbona hatuwaoni uku wilaya ya Manyoni kwani vijana tuko tayari kwa ukombozi na tunahitaji m4c ije iamshe hari kwa baadhi ya watu ambao bado wamelala.

  Uongozi wetu bado hauko sawa wapo kimya sana wanatishwa na magamba, so njoeni mtoe elimu ya uraia na hamasa kwani kwa uwezo wetu baadhi tumejitaidi vya kutosha.

  Msituangushe makamanda wetu.
   
 2. K

  KWA MSISI Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakupongeza kwa ujumbe wako ninaimani kubwa na makamanda nahakika watafanyia kazi ombi lako since I believe that management ta chadema ipo active hapa jf,by the way mimi pia ni kamanda.M4C daima.
   
 3. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Watu wa Manyoni mko kwenye giza totolo, ni vizuri sana muamushwe. wabunge wenu Chiligati ,Lwanji hawana hata dalili ya kuwaamusheni, cha kujivunia Manyoni ni ile kambi ya wakoma iliyopo kenywe kijiji cha Sukamahela.
   
 4. Elba

  Elba JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 383
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bila shaka makamanda mmesikia hili. Ni kweli Manyoni imesahaulika sana katika operation za M4C. Nakumbuka wakati wa uchaguzi, moto wa kutaka mabadiliko ulipowashwa jimbo la Manyoni magharibi watu walipokea kwa mikono miwili, ni uchakachuaji tu ndo uliinusuru CCM na Lwanji wao! Sana vijana wa Manyoni wana kiu ya mabadiliko.
   
 5. m

  man lesha Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Ilikua zaman mkuu, vijana ss wana ari ya mabadiliko kwan wamechoshwa na umaskini uliokithiri so mku uclaumu swala apa ni kujenga.
   
 6. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mara zote nimewaambia cdm, wasikae ofisini, ofisi zao inatakiwa iwe ni mikoa na vijiji mbalimbali wanamozunguka kupata wanachama. Wasijifananishe na ccm hata kidogo, wao ccm wako ikulu!
   
 7. Elba

  Elba JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 383
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  tunaomba mkuu Tumaini Makene utupe mwongozo, nini hatma ya Wanamanyoni kufikiwa na timu ya M4C??
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. p

  pembe JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  nakubaliana na wewe mkuu. Cdm lazima wafanye kazi ya ziada kuwasha moto wa matumaini nchi nzima. Mratibu wa cdm apambane kila kona ya nchi ipate mwakilishi. Sio lazima wakuu wa chama wafike kila mahali bali viongozi wa mikoa wapewe maelekezo jinsi ya kugusa kila kona ya mikoa yao...yes it can be done na wananchi wako tayari kufuata miongozo watakayopewa!!!
   
 9. Magwangala

  Magwangala JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 2,005
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  waambie Samaria,Tambukareli,Misheni wote kuwa tunakuja kuwasha moto wa uhakika huko hivi punde
   
 10. m

  man lesha Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  umenena mkuu, waje uku vjjn wa2 wako tayar kwa mabadlk6
   
 11. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kilimatinde, Nkonko, Sasajila, Heka, Aghondi, Itigi, Rungwa, Kintinku, Chikuyu, Msemembo, Saranda na kwingine koooote inatakiwa paishe jamani. M4C Fanyeni kazi vijana wanawasubiri
   
 12. m

  man lesha Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  makamanda mcsahau na hv vjj, sanza, mgandu, chikola, mpola, sasilo, iseke, mgandu, igwamadete, ikasi, kashangu, doroto, ntumbi, chikombo. Ongeza vya kwako vilivyosahaulika.
   
 13. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Manyoni ina rasilimali nyingi sana jamani wala wakazi wake hawapaswi kuwa maskini.
  1. Mifugo
  -Ng'ombe wengi pamoja na kupunguzwa na ukame wa mara kwa mara, wanaweza kabisa kuimarisha pato la mtu mmoja mmoja na jamii.
  -Kuku wakubwa wa kutosha, hadi Saranda stesheni ikapewa jina Kilimanjaro Hotel.
  2. Madini
  -Dhahabu maeneo ya Iluma na Londoni
  -Gypsum kule Itigi
  -Madini ya vito kama Ruby, Green tomaline kule Saranda, Itaga masili
  3. Kilimo
  -Tumbaku, mahindi maeneo ya Mgandu
  -Ufuta na Alizeti hustawi pia
  4. Asali inapatikana kwa wingi pia
  5. Maliasili na Utalii
  -Hifadhi ya Rungwa
  -Pori la Kizigo
  -Chemchemi za maji moto Londoni
  -Bonde la Ufa la Afrika Mashariki lionekanalo vema pale kwenye Mlima wa Sukamahela (kwenye lami) ambao wengi kimakosa huita Mlima Saranda(wakati Saranda ni kule ilikopita reli)
  -Chuma kilichowekwa na Mjerumani pale Sukamahela, kuonesha kuwa pale ndio katikati ya Tanganyika(wengi hawajui hili)
  6. Mawasiliano na Uchukuzi
  -Mtandao wa barabara ya Lami toka Dar hadi Mwanza umeifanya ifikike vema
  -Reli ya kati inapita eneo kubwa la wilaya, huku ikiunganishwa na ile ya Singida
  -Na sasa Manyoni inaunganishwa kwa lami hadi Kigoma
  (Japo mjini Manyoni kwenye barabara za Halmashauri, hakuna hata meta 1 ya lami)
  -Mitandao ya simu imeenea sehemu kubwa
  7. Huduma za jamii
  -Kuna hosp kubwa ya Rufaa, St. Gasper, inavuta watu wengi Itigi, inaweza kuwa kivutio cha biashara na mapato kule, km ilivyo sekta ya Afya kule India

  Kifupi, wana Manyoni hawapaswi kuwa walipo, wanahitaji uongozi bora wenye kuleta mabadiliko chanya.
   
 14. ABEDNEGO CHARLES

  ABEDNEGO CHARLES JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hayo madongo ndiyo anayotaka mtoa hoja?
   
 15. s

  salehe Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 16, 2008
  Messages: 83
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 15
  Msendekwa uliyoongea yote ni kweli isipokuwa pointi namba 5 kipengele cha mwisho, hata Mkuu wa Mkoa wa Singida aliaibishwa na Afisa Ardhi kaita waandishi wa habari kuelezea chuma hicho hapo Sukamahela kuwa ni katikati ya Tanganyika, hilo sio kweli!!!!!!!!!!!!!!!! hiyo ni pointi ya upimaji, nenda kwenye milima yote mirefu Tz nzima alama hizo zipo, mfano mzuri kwako fika mlima wa Iwelewele mpaka wa Manyoni na Singida juu kabisa utakuta chuka kama hicho so naomba ufute pointi hiyo tu!!!
   
 16. C

  Chibenambebe Senior Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Magamba wanapiga mkwara sana vijana wapenda mabadiliko lakini kwa kuwa viongozi wa chama kitaifa hamuendi kuwapa nguvu mnawafanya wajione kama mayatima. Mtu akiweka bendera tuu ya chadema magamba wanakufanyia kikao na kukuita na kukupa karipio kali mpaka nashanga hiyo mamlaka juu ya demokrasia ya watu wanaitoa wapi hawa jamaa. Na wananchi kwa kutojua sheria zinazowapa uhalali wa kile wanachokifanya unakuta wanaishiwa nguvu hatimaye kunywea.
   
 17. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Agwe, leche ziizo nagwe. Hayo sio madongo ni ukweli mtupu
   
 18. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Agwe, leche ziizo nagwe. Hayo sio madongo ni ukweli mtupu
   
Loading...