CHADEMA mnatakiwa sana kujifunza na kukubali kuwa kukosoana, kuvumiliana ndo sehemu ya demokrasia

sambulugu

JF-Expert Member
Jun 1, 2021
3,913
7,175
Nalisema hili kutoka na tabia ya baadhi ya CHADEMA kuwa ma mtazamo kama ifuatavyo:

I) Baadhi ya wanaCHADEMA wamekuwa waligombana sana na watu walio kinyume na sera zao! Mfano mtu akitoka wazo tofauti juu ya CHADEMA inachokiamini watu wa chama hiki hujitokeza kuta kejeli na matusi kama kwamba wao ni miungu watu wako sawasiku zote!

II) Jambo jingine inabidi CHADEMA ijue kuwa ili kupata wanachama na kuungwa mkono na makundi yote ni mhimu sana kutambua na kujipambanua kutoa hoja zitakazo wafanya watu wa jamii mbali mbali waweze kuwaamini na kuwaunga mkono!

III) Mjifunze pia kutotukana kila mtu anayetoa mawazo yake ambayo ninyi hamyafurahii Mfano Dr Slaa alipozungumzia mambo ya katiba mpya kuwa sio suluhisho la kila kitu wote mlikuja juu na kutoa maneno makali huku kwa upande mwingine mkijiita wanademokrasia!

IV) Tambue pia ya kuwa kuzungumzia sana watu kwenye ushawishi kwenye jamii kama Dr Slaa na Magufuli na kujikita kutukana mitandaoni huku mkijua kabisa watu hao walishawahi kuaminiwa na jamii fulani fulani za watanzania mnajisababishia kujijengea watu watakao waoana nyinyi kuwa ni wababaishaji, hapa mnachotakiwa kufanya ni kuwafanya wale walikuwa wanamuona Magufuli yuko sawa waone nanyi mkiingia utafanya kipi bora kuliko Magufuli, na hiyo ndo siasa ya kweli.

Mfano unampomkosoa labda Magufuli ambaye kuna kundi lilikuwa linamwamini jiulize wewe utafanya nini zaidi ukipewa nafasi ya uongozi na utoe mawazo yako mapya! Mfano mwingine ni Dr Slaa walikuwa na ushawishi sana ndani ya CHADEMA na chama kilivuta watu wengi! Inapotokealeo anatoa mawazo yake na nyinyi CHADEMA mnamsakama kwa maneno makali ya kejeli halo hamuwezi kuvuta watu maana watawaona nyinyi kama kikundi cha wahuni.

V) Juzi hapa Rais Samia kakutana na Lisu na kukutana pia na Mbowe matukio hayowalikuwa yana nia nzuri lakini nyinyi bado hamtaki kuridhika badala yake ni kejeli kwa serkali na kujiona mnajua kila kitu na mkono sahihi kwa kila kitu! Yaani nyinyi ndo wenye mawazo sawa mda wote!

VI) Mkitaka kufika mbali watafuteni hata wale watu wa mpinzani wako wa kisiasa wawe wako sio ubaki na watu wale wale wa kila siku! Na hali hiyo ikiendelea ya kubaki na watu wale wale chama hugeuka kuwa kikundi cha wanaharakati UCHWARA! na kupoteza mvuto katika jamii.

Tambueni DEMOKRASIA ni watu na watu utawapata utakapokuwa na mawazo mbadala na sera zitakazo gusa mahitaji ya watu! Sio kukejeli na kujifanya mjuaji kwa kila jambo ikiwa ni pamoja na kujiona kuwa wewe ndiye kwenye haki mda wote.

Namalizia kusema chama sio waanzirishi au viongozi lakini chama ni watu tena wale wa kawaida sana ambao watakifanya chama kuwa na nguvu!

Asanteni sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom