CHADEMA mnatakiwa kumuomba msamaha Dkt. Slaa, laana yake inawatafuna kama saratani

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,054
2,000
Kama binadamu mstaarabu pale unapofanya kosa kuomba msamaha huwa ni jambo la kiungwana. Maana utakuwa umejitambua wapi ulikosea.

Mwaka 2015 Chama cha Demokrasia na maendeleo kilifanya kosa kubwa sana. Kwa kumuumiza moyo aliyekuwa Katibu mkuu wa chama hicho.

Kwani ni kwa uroho wa fedha na sifa waliamua kumkaribisha Edward Lowassa awe mgombea kupitia chama chao. Na wao waliona wamepata asset ambayo itawapa kura nyingi na wabunge wengi ili wapate ruzuku za kutosha. Na kwa asilimia kidogo walifanikiwa hasa kwa kuwa na muungano wa Ukawa.

Lakini ikumbukwe Chadema ni Chama ambacho kilipata umaarufu na kuonekana kama chama ambacho kingelikuja kuwakomboa watanzania. Kwani kipindi hicho Ccm ilikuwa imechafuka.

Dk Slaa akiwa mbunge kupitia Chama cha Chadema aliibua kashfa nyingi nzito ambazo ziliweza kukipa imani chama hicho.Mbaya zaidi kashfa hizo na Orodha ya mafisadi waliokuwa wanaliibia taifa letu, Dk Slaa alikuwa anaipata kwa tabu sana. Maana ni watanzania wenye nia njema na nchi hii walikuwa wanaziiba sehemu nyeti na kumpelekea ili aziweke wazi bungeni.

Kwa kufanya haya Dk Slaa alihatarisha maisha yake. Maana hata wazee wa kazi walikuwa wanamuwinda usiku kucha. Mpaka ilifikia hatua kabla ya kulala aliomba Mungu na matokeo yake akawa anaonyeshwa kwa maono vinasa sauti vilivyowekwa chini ya godoro lake kwenye hotel aliyokuwa analala hapo Dodoma.

Akiwa katika harakati za kupambana kwa ajili ya Chama alianguka na kuvunja mkono wake akiwa jijini Mwanza. Lakini yote haya Mbowe na wapiga madili wa Chadema hawakuyaona. Wao walichojali ni kuvuta mpunga na kumuacha solemba Dk Slaa.

Hivyo sababu Laana ya Dk Slaa inawatafuna kwa kasi kama cancer ni vyema mkamuomba msamaha tena hadharani. Ikiwezekana mpige magoti live mbele ya live Tv.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,124
2,000
Dr.Slaa mlimpiga mabomu na virungu yeye na mke wake huku mkimwita ni mwenye kiwanda cha uongo leo kawa lulu!

Kamuombeni kwanza Kolimba msamaha ndio muje na hizi ngonjera zenu.

Wanafiki wakubwa nyie!
 

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,054
2,000
Dr.Slaa mlimpiga mabomu na virungu yeye na mke wake huku mkimwita ni mwenye kiwanda cha uongo leo kawa lulu!

Kamuombeni kwanza Kolimba msamaha ndio muje na hizi ngonjera zenu.

Wanafiki wakubwa nyie!
Unataka kulinganisha 1 na 2 ziwe sawa. Jambo ambalo haliwezekani. Kuomba msamaha ni uungwana.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
3,724
2,000
Lile swali lake sasa linaanza kuleta mantiki wakati huu tunapo elekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwingine!

Lowassa alikuwa ni Asset ndani ya chama au alikuwa ni Liability?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom