CHADEMA Mnaogopa nini kuweka Hotuba ya Wenje kwenye Mtandao wenu?

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Wadau, kama tunavyojua Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekiel Wenje aliwasilisha Maoni ya Kambi ya Upinzani. Miongoni mwa hoja alizozitoa Wenje jana ni kuishutumu Tanzania kuingilia mambo ya ndani ya Rwanda na kuilalamikia Tanzania kwa kitendo chake cha kupeleka majeshi nchini DRC kuwaondoa waasi wa M23, hotuba ambayo imelalamikiwa na kulaaniwa kila kona ya nchi hii na nje ya nchi. Baada ya hotuba hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe aliongea kwa ukali na kuwatahadhalisha Watanzania kutokana na uchochezi unaofanywa na Wenje. Pia Membe alilaani kitendo cha Wenje kuwa msemaji wa Serikali ya Rwanda ndani ya Bunge la Tanzania hali ambayo ameiita ni usaliti mkubwa.

Tumesikia pia utetezi wa Mwenyekiti wa CHADEMA na UKAWA, FREEMAN MBOWE akisema kuwa alichowasilisha Wenje ni Maoni ya Kambi ya Upinzani na kwa hali hiyo yalipata baraka kutoka kwa viongozi wa Kambi hiyo. Baada ya majibu hayo ya Mbowe, nilitegemea kuwa kama kawaida yao wataweka hotuba hiyo kwenye Mtandao wao wa www.chademablog.blogspot.com. Hata hivyo, mpaka sasa hawajaweka hotuba hiyo huku wananchi wengi wakitaabika kuitafuta bila ya mafanikio. Kutokana na hali hiyo nimelazimika kuwauliza CHADEMA, kama mnasema kuwa alichowasilisha Wenje ni maoni ya Upinzani, mbona mnagwaya kuyaweka kwenye mtandao wenu?
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Yamepita hayo Lizaboni,tugange yajayo. Tunahitaji ya leo ya Wizara ya Ardhi ambayo inatugusa sisi walala hoi.
Mkuu, hatuwezi kuachia hili la Wenje linapita kimya kimya. Wengine wanahitaji hiyo Soft copy ya hotuba ya Wenje kwa kumbukumbu
 
Arnold Ringo

Verified Member
Jan 23, 2014
2,319
1,170
Chadema si hao wano kuchua b200 alafu wananyamaza ingekua inaogopwa mitandaoni isingesomwa kabisa bungeni wakati unaweka huu uzi hivi ulikua unaakili timamu kweli Lizabon maana uzi wako hauna Mantiki yoyote pole sana kwa hilo lakini kuishabikia Intarahamwe yaitaji uwe kwanza una akili flani
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Chadema si hao wano kuchua b200 alafu wananyamaza ingekua inaogopwa mitandaoni isingesomwa kabisa bungeni wakati unaweka huu uzi hivi ulikua unaakili timamu kweli Lizabon maana uzi wako hauna Mantiki yoyote pole sana kwa hilo lakini kuishabikia Intarahamwe yaitaji uwe kwanza una akili flani
Umeongea pumba tu hapa. Au ni hasira baada ya Membe kuwapa za uso?
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Mkuu, hatuwezi kuachia hili la Wenje linapita kimya kimya. Wengine wanahitaji hiyo Soft copy ya hotuba ya Wenje kwa kumbukumbu

Lizaboni kuna issue nyingine ziko very sentive ni vyema kama unahitaji copy,M-Pm mtu akutumie.Kama tutashindwa kuidadavua hotuba ile kwa mwelekeo CHANYA hata sisi watanzania tutashindwa kuelewana.Ndiyo maana nasema tugange ya leo yanayohusu hata hao BANANYAMULENGE wa Bukoba ambao kwa kiasi kikubwa watanzania waishio maeneo ya mipakani kati ya Rwanda,Burundi na Uganda maeneo yao yamechukuliwa kwa udanganyifu,rushwa na au kuonewa na mengine yameshirikisha hata viongozi ambao wanaUNASABA na makabila yatokayo nchi hizo.
 
Nakubaliana na wewe kabisa juu ya hili. Ila suala la usalama wa nchi ni muhimu zaidi kuliko hayo masuala mengine. Ni vema likapewa kipaumbele
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
77,564
2,000
naunga mkono hoja ya WAZIRI KIVULI MH WENJE , hakuna sababu yoyote kwa tanzania kujiingiza kwenye mgogoro wa RWANDA , sasa siyo kila wanachotuburuza hawa viongozi wa ccm tukubali , wewe lizabon niwekee hapa sababu hata moja tu ya msingi iliyopelekea TANZANIA kupeleka majeshi DRC .
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Nakubaliana na wewe kabisa juu ya hili. Ila suala la usalama wa nchi ni muhimu zaidi kuliko hayo masuala mengine. Ni vema likapewa kipaumbele

Ninafahamu sana.Hivi wajua nimekaa na wakimbizi kutoka Rwanda na Burundi sana tu.Na watanzania wa Mikoa ya Kigoma,Bukoba na hata Tabora wapo kwenye risk kubwa ya amani?Watu hawa wanachuki za ndani kwa ndani na ni wepesi wakurudisha visasi,hata kama kakitu ni kadogo.Watu hawa wako pia ndani ya serikali yetu kwenye sehemu nyeti kabisa.

Kunaumuhimu wa viongozi wetu wa pande zote upinzani na chama tawala kuondoa sintofahamu hizi,na hasa kuziweka nchi hizi mbili kwenye mahusiano mazuri tena.Watumie njia yoyote ile lakini si ya mauaji au vita kufikia muafaka.Ninafahamu ni jinsi gani Kagame anavyojiona yuko juu ya sheria hata za nchi nyingine,lakini bado tutafute njia mbadala ya kuyaweka haya sawa.Tupo sote kwenye EAC,tufanyeje?tuondoke tu au kukubaliana na kuridhiana na mahasimu wetu hawa.Lizaboni niko KITAIFA zaidi kuliko kichama.Nimedadavua hotuba zote mbili nimeona nafasi ya zote mbili kuwa zinataka USALAMA,AMANI na UHURU wa Taifa letu.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
naunga mkono hoja ya WAZIRI KIVULI MH WENJE , hakuna sababu yoyote kwa tanzania kujiingiza kwenye mgogoro wa RWANDA , sasa siyo kila wanachotuburuza hawa viongozi wa ccm tukubali , wewe lizabon niwekee hapa sababu hata moja tu ya msingi iliyopelekea TANZANIA kupeleka majeshi DRC .
Kwanza utambue kuwa Tanzania haijaingia mgogoro na Rwanda bali Rwanda wamehamaki baada ya Tanzania kupeleka majeshi na kuwaanga,iza waasi wa M23 ambao walikuwa wanasaidia na Serikali ya Rwanda
 
kbosho

JF-Expert Member
Jun 4, 2012
13,026
2,000
Wekeni mikatapa ya UDA kwanza hapa!!!!! vinginevyo acha ungedere!!!!
 
Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Mkuu kwa ile tabia ambayo wenje na ukawa kwa ujumla ya kuungana na kagame kuitukana na kuishambulia tanzania hawataweza kuweka wanajua tutawashambulia.
 
Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
naunga mkono hoja ya WAZIRI KIVULI MH WENJE , hakuna sababu yoyote kwa tanzania kujiingiza kwenye mgogoro wa RWANDA , sasa siyo kila wanachotuburuza hawa viongozi wa ccm tukubali , wewe lizabon niwekee hapa sababu hata moja tu ya msingi iliyopelekea TANZANIA kupeleka majeshi DRC .
Wengi ambao siyo raia halali wa nchi hii mnaunga mkono hizo ishu zenu lakini hamtashinda kwenye hayo malengo yenu ya kuichafua tanzania.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Wenje kaisha hana jipya tena wakiweka watakuwa wamejikaanga wameandika uchafu mwingi sana.
Mkuu, huyu Wenje kila Mwaka huwa anatoa moya. Mwaka Jana aliwashutumu CUF kuwa ni Mashoga na alisababisha bunge kuahirishwa baada ya kukosekana utulivu. Mwaka huu anaungana na Kagame. Hakika huyu ni adui wa taifa hili
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom